NA BASHIR YAKUB -
Ni ukweli usiofichika
kuwa kisheria deni
linafunga. Hii ni tofauti
na wengi wanavyoamini.
Wako watu hukopeshwa
hela na hukaidi
kulipa au kulipa
bila kuzingatia makubaliano
kwa kuamini kuwa
mdai wake hatakuwa
na la kufanya kwakuwa
deni halifungi.
Na hii mara
nyingi huwatokea wale
ambao wametoa mikopo
bila hata rehani
yoyote. Mkopo kwa rehani
huwa haumsumbui mtoa
mkopo kwakuwa mrejeshaji
anapokaidi rehani huchukuliwa. Lakini
pasipo na rehani
huwa inahitajika nguvu
za ziada kumfanya
mdeni alipe.
Ni vema kuliweka sawa
hili la deni kufunga ili wale waliodhulumiwa haki
zao wachukue hatua na wale
wenye mpango wa
kudhulumu kwa mgongo
wa deni halifungi waache au wadhulumu
lakini wakijua kuwa
hatua dhidi yao
zaweza kuchukuliwa.
1.KUFUNGWA.
Moja ya tofauti
inayojulikana sana kati
ya kesi za
jinai na mashauri ya
madai ni hii
kuwa kesi za
jinai mtu atakamatwa
atazuiliwa na pengine
baadae akionekana ana hatia adhabu
yake itakuwa kufungwa. Hii
ni tofauti na
zile za madai ambapo
hamna kukamatwa wala
kuzuiliwa na hukumu zake
hazihusu kufunga.
Kwa ujumla(general
rule) kesi za madai
hazifungi isipokuwa yapo mazingira
ambapo zinaweza kufunga. Moja
ya mazingira hayo
ni pale ukaidi wa kutolipa
deni unapojitokeza. Tutaona zaidi
kuhusu hili.
2. NINI
UFANYE KUMFUNGA MDENI.
Kwanza kabisa ni
lazima ufungue kesi ya msingi
ya kudai kile unachodai likiwemo deni. Utadai
kulipwa kutokana na makubaliano uliyonayo
na mdeni. Kesi
itaendelea mpaka hukumu
itakapotolewa.
Hukumu itakapotolewa
ikiwa umeshinda basi
mahakama itaamuru kulipwa
kwa deni lako.
Muda utatolewa ili
mdeni aweze kulipa
deni. Kama mda uliotolewa
utapita bila kutekeleza kilichoamuliwa basi
mdai ana haki
ya kuiomba mahakama
kwa maombi maalum kukamata mali
yoyote aliyonayo mdeni
ikiwa anayo.
Kama hana mali
yoyote inayoweza kukamtwa
na kuuzwa ili
kulipa deni basi hapo
ndipo mdai utaomba
katika maombi yako
kuwa mdeni akamatwe na kufungwa kama
mfungwa wa madai.
3. JE
KUFUNGA KUNAMALIZA DENI.
Hapana kufunga hakumalizi
deni. Kufungwa ni
adhabu kwa ukaidi
wa kutotiii amri halali
ya mahakama iliyotaka
kulipa deni kwa
wakati. Kufungwa sio
mbadala wa deni. Ni
adhabu ya ukaidi. Kutokana na
hilo mtu atafungwa
na akirudi ataendelea
kudaiwa na atatakiwa
kulipa deni lake
kama kawaida.
4. MDENI
KUKAMATWA.
Amri ya xxi
kanuni ya 35 ( 1 ) ya
sheria ya mwenendo
wa mashauri ya madai
inasema
kuwa mdai anapokuwa
ameomba kukamatwa kwa mdeni basi mahakama kabla
haijakamata inaweza kutoa taarifa
ya kumwita mdeni
afike mahakamani kueleza
kwanini asikamatwe na
kufungwa.
Hii ina maana ikiwa
ataitikia wito huo basi
atatakiwa ajibu kwanini asifungwe. Akijibu kuwa hataki
kufungwa basi nafasi ya
kulipa muda huohuo
hutolewa. Na kama hawezi
kulipa muda huo basi
atakamatwa na taratibu
za kifungo cha
madai zitafuata.
Pia kanuni ndogo
ya ( ii) inaendelea kusema
kuwa ikiwa hatatokea
mahakamani siku hiyo
basi mahakama moja
kwa moja itatoa hati
ya kukamatwa kwake ili afungwe.
Pia ukamataji wa mdeni
katika hili utahusika
na polisi na
si madalali wa mahakama(
court brockers) kama ilivyozoeleka
katika mashauri ya
madai. Polisi watahusika
hapa kama wanavyohusika katika
shughuli nyingine za kijinai kwakuwa itakuwa
ni amri ya mahakama.
Kwahiyo deni linafunga na
kesi ya madai
inafunga.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO. 0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment