NA BASHIR YAKUB -
Ipo namna nzuri
ya umiliki wa ardhi wa
pamoja ambayo huepusha
migogoro hasa kwa
walio katika ndoa. Migogoro ya
ardhi hutokea kwa
namna tofauti. Ipo inayotokea
wakati wa uhai
wa wamiliki na
ile itokeayo baada
ya uhai wa wamiliki
wote au mmoja
wao .
Umiliki kwa mafungu
yasiyogawanyika huwa ni suluhu
kwa yote
haya. Ni suluhu kwa wanandoa
wenyewe wanapogombea mali lakini ni
suluhu wakati ndugu wanapotaka kumpokonya mwanandoa ardhi
iliyoachwa na mwenza
wake baada ya kifo.
Ni vema kujua kuwa sheria
ya ardhi kawaida
inatambua umiliki wa
ardhi wa aina mbili. Tumewahi
kueleza umiliki huo
hapa lakini leo
pia tutaeleza. Upo umiliki binafsi
na umiliki usio
binafsi kwa maana
ya umiliki wa
zaidi ya mtu
mmoja.
1.UMILIKI BINAFSI.
Umiliki binafsi ni
umiliki wa mtu mmoja. Kama
ni nyumba, shamba au
kiwanja kinakuwa chini
ya jina la
mtu mmoja. Huyo
mwenye jina linalosomeka
ndiye huhesabika kama mmiliki wa
pekee. Haki zote zikiwemo zile za
kuhamisha, kuweka rehani, kuuza,
kugawa humhusu mtu
mmoja pekee. Hahitaji ridhaa ya
mtu mwingine katika kutekeleza
muamala wowote katika
umiliki huu labda yawepo
mazingira maalum.
2. UMILIKI
WA PAMOJA .
Huu ni umiliki
wa pamoja kama neno
lenyewe
lilivyo. Kwa jina la
kitaalam hujulikana kama “co-occupancy”.
Watu wawili au
zaidi huweza kumiliki
nyumba, shamba au kiwanja kwa
pamoja. Haki za
msingi kama zile
za kuhamisha umiliki, kuuza, kuweka
rehani,kutoa zawadi
huwahusu wamiliki wote.
3. WANANDOA SAJILI ARDHI
YENU KWA MAFUNGU YASIYOGAWANYIKA KUEPUKA MIGOGORO.
Umiliki wa ardhi
kwa mafungu yasiyogawanyika hutokana
na umiliki wa
pamoja . Yafaa tuelewe kuwa umiliki wa
pamoja umegawanyika sehemu
kuu mbili. Kwanza
ni mafungu yasiyogawanyika na
pili ni mafungu
yanayogawanyika. Mafungu yasiyogawanyika hujulikana
kama “joint occupancy” na yale
yanayogawanyika hujulikana kama“occupancy
in common”.
4. FAIDA KUU YA KUMILIKI KWA MAFUNGU YASIYOGAWANYIKA.
Faida kuu ya
umiliki wa aina
hii ni kuwa endapo mmoja
wa wamiliki amefariki
basi ardhi ile
moja kwa moja ( automatically) huamia
kwa mmiliki anayebaki.
Hii ina maana
kama ni nyumba
au kiwanja na kilikuwa kikimilikiwa
na wanandoa basi
anapofariki baba ardhi
ile huingia katika umiliki
wa mama moja
kwa moja na anapofariki
mama umiliki huingia kwa
baba moja kwa
moja.
Hii ni tofauti kama
usingekuwepo umiliki wa
aina hii ambapo
ingetakiwa kama ni
nyumba au kiwanja
kiingie katika orodha
ya mirathi na kutakiwa
kugawiwa
kwa warithi wote wenye
haki.
Umiliki wa
aina hii huepusha mgogoro
hasa baada ya
kifo kwakuwa mara
nyingi mgogoro wa
mali baada ya
kifo huibuka katika majadiliano
ya nani anapata
nini na hata unapokuwapo wosia.
5. NAMNA YA
KUSAJILI KWA MAFUNGU
YASIYOGAWANYIKA.
Unaponunua ardhi
iwe nyumba au
kiwanja kama kina
hati bila shaka
utahitaji kubadilisha jina. Ni
hapo wakati wa
kubadilisha jina utakapoomba
yaingie majina mawili
kama wanandoa. Lakini
pia ikiwa ardhi
uliyonunua haina hati
basi wakati wa
kuanza kutafuta hati utaeleza bayana
kuwa unahitaji umiliki
wa pamoja wa
mafungu yasiyogawanyika ya
wanandoa.
Mamlaka za ardhi
wanajua nini watakuomba uwasilishe ili kukamilisha usajili wa
aina hiyo.
Usajili kwa mafungu
yasiyogawanyika si kwa wanandoa
pekee bali pia
hata mtu na mtoto wake, mtu
na ndugu, au
rafiki wanaweza kufuata
utaratibu maalum na kufanya usajili huu.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO. 0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment