NA BASHIR YAKUB -
Kutoa ushahidi wa uongo
ni kosa. Ni
kosa lenye adhabu kisheria. Ushahidi wa
uongo ni pamoja
na kupanga au
kupangiwa la kusema
mahakamani wakati mkijua
kuwa sio la
kweli. Kosa hili ni moja ya
makosa yanayotendwa mno
tena kiholela. Ni kawaida
watu kupanga waseme
nini mahakamani huku
wakijua wanachopanga sio cha
kweli.
Suala la ushahidi
wa uongo halijalishi kesi
ni ya aina
gani. Iwe jinai
au madai shahidi
anawajibika kuwa mkweli
daima. Kisichotakiwa ni kusema
uongo ambao hupotosha
usimamizi bora wa haki.
1.NAMNA YA KUWACHUKULIA HATUA
SHAHIDI WAONGO.
Ni wajibu wa
mtu wa upande
wa pili katika
kesi kuchukua hatua dhidi
ya shahidi msema
uongo. Ikiwa uko upande
wa pili wa kesi na
shahidi wa upande
mwingine anatoa ushahidi
wa uongo dhidi
yako ni wajibu
kwako kuchukua hatua
haraka sana.
Hatua inayofaa ni
hii ya kutoa
taarifa polisi au kwa
hakimu/jaji husika ili kumfungulia mashtaka
shahidi kwa kusema uongo.
2. KOSA LA KUTOA USHAHIDI WA
UONGO KATIKA SHERIA.
Kifungu cha 102
cha Kanuni za
adhabu kinasema kuwa
mtu yeyote wakati
wa kufungua shauri au
wakati shauri likiendelea, kwa
kujua akatoa ushahidi
wa uongo kuhusu suala lolote katika
kesi atakuwa ametenda
kosa.
Hiki ndicho kifungu
cha sheria kinacholitangaza tendo
la kutoa ushahidi wa
uongo kuwa kosa( perjury).
3. HAIJALISHI
USHAHIDI ULITOLEWA KWA KIAPO
AU BILA
KIAPO.
Kawaida upo ushahidi
unaotolewa kwa kiapo na
upo usiotolewa kwa
kiapo. Ushahidi kutolewa
kwa kiapo ina maana
shahidi ataapa kabla
ya kusema lolote
kama shahidi. Na bila
kiapo shahidi hataapa.
Kwahiyo iwe ushahidi
ulitolewa kwa kiapo au bila
kiapo ikiwa ni wa
uongo hakuna kinga
isipokuwa litakuwa kosa
tu. Wapo wanaodhani
ukitoa ushahidi bila
kiapo basi hata
uwe wa uongo
itakuwa haina shida.
Si kweli kosa
linabaki palepale.
4. USHAHIDI
UWE WA MDOMO
AU MAANDISHI BADO
NI KOSA.
Ushahidi waweza kutolewa
kwa namna mbili. Unaweza kutolewa
kwa mdomo au kwa maandishi.
Ushahidi kwa mdomo
ni pale mtu
anapohojiwa na akazungumza
mbele ya mahakama.
Wakati ule wa
maandishi ni ule unaotolewa kwa kuandika.Shahidi anaweza kuandika
mwenyewe au wakili wake nje
ya mahakama. Kisheria
huu wote ni
ushahidi na wajibu
wa kusema kweli unabaki palepale.
5. KUSAIDIA AU KUSHAURI
KUTOA USHAHIDI WA
UONGO NALO NI
KOSA.
Kifungu cha 102 ( 2 )
cha kanuni za adhabu kinasema
kuwa mtu yeyote
ambaye atasaidia , atashiriki, atashauri,
atatuma au kushawishi
mtu mwingine kutoa
ushahidi wa uongo
atakuwa ametenda kosa
la kushawishi kutoa ushahidi
wa uongo.
Huyu hatashitakiwa
kwa kutoa ushahidi
wa uongo bali
kushawishi kutoa ushahidi
wa uongo.
6. ADHABU
YA KUTOA USHAHIDI
WA UONGO.
Kifungu cha 104
cha kanuni za
adhabu ndicho kinachotoa
adhabu kwa yote
mawili, yaani kutoa ushahidi
wa uongo na kushawishi
kutoa ushahidi wa
uongo.
Kinasema kuwa mtu
yeyote ambaye atatenda
kosa la kutoa
ushahidi wa uongo au kushawishi kutoa
ushahidi wa uongo atawajibika
kwa adhabu ya
kifungo cha miaka
saba.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO. 0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment