NA BASHIR YAKUB -
Kazi kubwa ya
sheria zote zinazoshughulika na
masuala ya ardhi
ni kuratibu na kutoa
mwongozo katika miamala
mbalimbali ya masuala ya ardhi katika
maisha ya kila
siku. Miamala hiyo ni kama uuzaji
na ununuzi wa
ardhi, masuala ya mikopo
na rehani, upangaji na
upangishaji, masuala ya fidia, kuhamisha umiliki, haki
na wajibu wa mmiliki ardhi, haki na
wajibu wa serikali
katika ardhi yote, upimaji
na ramani, namna ya kutatua migogoro
ya ardhi, n.k.
Makala yatagusa kwa
mtindo wa dondoo
baadhi ya mambo
ya msingi yaliyo
katika sheria ya ardhi namba 4 ya 1999 sura
ya 113.
1.SHERIA NAMBA
4 YA MWAKA 1999.
Sheria hii ilipitishwa na
bunge la Jamhuri
ya Muungano mwaka 1999. Hata
hivyo ilianza kutumika
rasmi mwezi mei
mwaka 2001.
( a ) MDHAMINI WA ARDHI YOTE NI
RAIS.
Sehemu ya pili
ya kifungu cha
3 cha sheria hii
inaanza kwa kueleza
sera ya taifa
ya ardhi. Kubwa linalotajwa ni
kuwa ardhi yote
ni mali ya
umma ambayo mdhamini
wake ni rais
wa Jamhuri ya
Muuungano wa Tanzania. Huu
ndio msingi mkuu
wa ardhi yetu.
( b ) WASIMAMIZI WAKUU WA ARDHI.
Sehemu ya iv kifungu cha
8 mpaka 18
kinaeleza watumishi wakuu
na wasimamizi wa
ardhi kitaifa. Waziri wa
ardhi ndiye mwenye
dhamana kuu akifuatiwa
na kamishna mkuu
wa ardhi kabla
ya kutajwa kamishna
msaidizi na baadae maafisa ardhi . Wajibu, kazi
na majukumu yao
yameainishwa katika vifungu
hivyo. Sambamba na hilo
mipaka katika utekelezaji
wa majukumu yao ni jambo jingine
lililoainishwa.
( c ) KUMILIKI HATI.
Sehemu ya vi kifungu
cha 24 mpaka 30
yameelezwa masuala ya
hakimiliki. Taratibu za
kupata hakimiliki na
umilikishwaji . Wakati huohuo
vifungu vya 31 mpaka
35 vimeeleza vyema masharti
yanayoambatana na hakimiliki ,muda wa hakimiliki
pamoja
na kodi za ardhi.
Kifungu cha 76
mpaka 78 kimeongelea
uuzaji wa ardhi
hasa zenye hati miliki.
( d ) UPANGAJI NA UPANGISHAJI.
Sehemu ya ix kifungu cha
77 mpaka 93 kimeeleza
kwa urefu masuala
yote ya upangaji
katika ardhi. Haki na
wajibu wa mpangaji vimeelezwa. Pia aina
ya mikataba ya
upangaji imeainishwa sambamba na yale mambo
ambayo yakifanyika yanaathiri
upangaji.
( e ) MASUALA YA MIKOPO .
Sehemu ya x
ya sheria hii
ni sehemu muhimu
sana. Ni sehemu
inayoeleza masuala ya
mikopo. Imeeleza haki
na wajibu wa
mkopaji halikadhalika haki za
mtoa mkopo. Eneo hili zimejadiliwa rehani
pia. Rehani zote yaani
zile zitokanazo na
hati za kimila
kwa ardhi za
vijijini na zile
zitokanazo na hati
zisizo za kimila
kwa wenye ardhi
mijini.
Haki za mtoa
mkopo pale pesa
yake inaposhindwa kurejeshwa
imeelezwa. Nini afanye,kwa kutumia
njia zipi na
kwa wakati gani ni
sehemu ya maelezo
hayo. Wakadhalika hatua
anazoweza kuchukua mkopwaji
baada ya kushindwa
kurejesha .
( f ) HAKI YA
NJIA.
Kifungu cha 151 mpaka
156 kimeongelea masuala
ya haki ya
njia. Hii ni hasa
kwa yale maeneo ambayo baadhi
ya watu wamejenga
kwa kuziba njia. Vifungu
vimeeleza haki ya
njia kama haki
ya msingi katika
masuala ya ardhi.
( g ) NGUVU YA MAHAKAMA.
Sehemu ya xiii kifungu
cha 187 sambamba
na kifungu cha
157 na 158 vimeeleza uwezo
na nguvu ya
mahakama katika masuala
ya ardhi. Mahakama inaweza
kutumika mda wowote
kwa yoyote anayehisi
haki haikutendeka katika
ardhi yake. Mahakama ndicho
chombo kikuu cha kufafanua
sheria hii na kutoa mwongozo
kwa pande zinazobishana.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO. 0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment