NA BASHIR YAKUB -
Tunapoongelea
upimaji ifahamike kuwa
upimaji upo wa
aina nyingi.Kutokana na hilo
upimaji unaoongelewa hapa
ni upimaji miliki. Lakini pia
tunaongelea upimaji miliki
wa ardhi
mijini na sio vijijini. Upimaji
wa ardhi miliki ni upimaji
ambao lengo lake
ni kummilikisha mtu
ardhi. Kummilikisha mtu ardhi
sio kumuuzia ardhi.
Kummilikisha mtu ardhi
ni kutambua ardhi
yake kimipaka na
kumpatia nyaraka mahsusi(specific) inayohusiana
na umiliki( hati).
Kwa maana hii
wanaomiliki ardhi ambazo
hazijapimwa hatuwezi kusema
wamemilikishwa ardhi .
Haijalishi ardhi hizo
ni za kwao na
wamezinunua kwa pesa zao. Kwa
kusema hivyo haimaniishi
kuwa ambao hawana
hati au hawajapima
ardhi zao basi
sio wamiliki, hapana
isipokuwa ni kuwa tu kwamba hawajamilikishwa kisheria
na mamlaka za
serikali.
Kutokana na hilo ardhi
iliyopimwa na ile
ambayo haikupimwa hutofautiana
hadhi na thamani kwa kiasi kikubwa.
1.NYARAKA ZINAZOHITAJIKA ILI
UPIMIWE ARDHI.
( a ) Barua
kwenda kwa mkurugenzi.
Anayetaka kupimiwa ardhi
anatakiwa kuandika barua
kwenda kwa mkurugenzi wa
halmashauri husika. Barua ni
nyaraka ya kwanza
kabisa ambayo unatakiwa kuwa
nayo. Ni katika barua
hiyo ambamo utaeleza
nia yako ya
kutaka kupimiwa ardhi na
matumizi ya ardhi
yako kama ni makazi,kiwanda n.k.
( b ) Kuambatanisha mkataba
wa mauziano. Katika
hatua hii mkataba
wa mauziano utatambuliwa kama nyaraka ya
umiliki. Mkataba huu ndio
utakaokutambulisha kama mmiliki
wa ardhi husika. Huu
unaambatanishwa kwasababu mmiliki
wa ardhi ndiye
mwenye jukumu la
kuomba kupimiwa.
Hivyo kuambatanishwa kwa
mkataba kunathibitisha kuwa
mmiliki ndiye anayeomba
kupimiwa kwa mujibu
wa sheria. Ni vema
mkataba wa umiliki
ukawa ni ule
mkataba wa kisheria
ulioandaliwa na kushuhudiwa
na mwanasheria.
( c ) Barua iliyotajwa
hapo juu katika
“A” hakikisha ina
muhuri wa mwen yekiti
wa serikali za
mtaa, sahihi pamoja
na mhuri wa mtendaji. Mwenyekiti na
mtendaji atakayetumika sio
wa pale unapoishi
bali pale lilipo
eneo unalotaka kupima.
Kama eneo lipo
unapoishi basi utamtumia
huyohuyo wa eneo
unaloishi.
2. HATUA
ZA KUPIMIWA.
Hatua hizi ni
muhimu kuzifahamu kwakuwa unapokuwa katika mchakato huu
unahitaji sana kujua kazi
yako imekwama wapi
na kwa nani ili
kama kulalamika
ujue pa kuanzia.
Wanaofanya kazi za
ardhi watajua namaanisha
nini.
( a ) Barua niliyotaja
hapo juu itawasilishwa
kwa mkurugenzi wa
manispaa . Barua hiyo
itakuwa imeambatanishwa na nyaraka
nilizotaja hapo juu. Manispaa
inayotumika siyo ile
unayoishi bali ni
ile lilipo eneo
husika.
( b ) Baada ya
barua hiyo kufika
kwa mkurugenzi basi
huwasilishwa kitengo cha
ardhi. Kila manispaa
ina kitengo cha
ardhi. Hapo hushughulikiwa na
afisa ardhi ambae
kazi yake kubwa
itakuwa ni kuthibitisha
uhalali wa umiliki
wa mwombaji.
( c ) Ikitoka hapo kwa afisa
ardhi inaenda mipango
miji. Afisa ardhi huipeleka
kwa afisa mipango
miji kwa fomu
ijulikanayo kama SF 47. Kazi kubwa
ya afisa mipango
miji ni kutizama
iwapo eneo linaloombwa
kupimwa lipo katika
ramani ya mipango
miji.Kama limo katika
ramani basi ataangalia
matumizi aliyoomba mwombaji
kama yanafanana na
yaliyoainishwa katika ramani
walizonazo.
( d ) Afisa mipango
miji akishathibitisha na
kuhakiki basi atatuma fomu
maalum SF 47
kwa afisa ardhi
mteule. Huyu kazi yake
ni kujaza fomu
maalum SF 37 ambayo
ni ya maombi
ya kupimiwa ambayo
ataiwasilisha kwa afisa
upimaji. Atafanya hivyo kwa kuambatanisha
ramani husika.
( e ) Mwisho mpima
ardhi atatoa maelekezo
kwa mpimaji mahsusi
ambaye ndiye sasa
atafanya kazi ya kuja
kufanya vipimo na
utapimiwa ardhi kwa
ajili ya usalama
na kuipandisha thamani
ardhi yako.
Haya yote yatafanyika
kwa kufuata sheria namba
4 ya ardhi
na kanuni zake .
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO.
0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
Ahsante kwa kunielewesha
Je? Kama ardhi husika haijapimwa na bado yalijatengwa kwa shughuli fulani ya manispaa