NA BASHIR YAKUB -
Mtu anaposhtakiwa/kulalamikiwa hutakiwa
kufika mahakamani. Lakini
atafikaje mahakamani bila
kujua kama ameshitakiwa. Ni lazima
kuna utaratibu wa
kumjuza mtu kuwa
kuna shitaka dhidi
yako. Na utaratibu ambao
hutumika si mwingine
bali ni kumtumia
mtu wito maalum ambao
hujulikana kama summons.
1.UTARATIBU WA
SUMMONS KWA MAKUNDI
MAALUM.
Wito au summons
ya kuitwa kuhudhuria
shauri baada ya kushitakiwa
hutolewa
kwa namna tofauti
kutegemea na aina
na mazingira aliyomo
muitwaji. Upo utaratibu
wa wa summons
kwa mtu wa
kawaida, utaratibu kwa
mtu aliye nje
ya nchi, utaratibu kwa
mtu aliye nje
ya wilaya au mkoa,
utaratibu kwa watumishi wa
vyombo vya ulinzi, utaratibu kwa
mtu asiyejulikana alipo, n.k. Baadhi ya tofauti hizi
ndizo zitakazotizamwa katika
haya makala.
2. SUMMONS
HUTOLEWA WAKATI GANI.
Summons/wito
haitolewi tu wakati mtu anapofunguliwa shauri .
Bali hutolewa hata
kwa mashahidi, hutolewa kabla
ya hukumu kwa yule ambaye
hakuhudhuria kesi ambayo imesikilizwa
upande mmoja, hutolewa kama
ukumbusho kwa mtu ambaye
alikuwa akihudhuria mahakamani
lakini baade akaacha, n.k.
3. WITO/SUMMONS
KWA ALIYE NJE
YA TANZANIA.
Amri ya “v”
kanuni ya 29 ya sheria
ya mwenendo wa
mashauri ya madai imetofautisha
watu walio nje ya
nchi. Watu walio nchi
za jirani kama Uganda, Kenya, Malawi, Msumbiji, na Zambia
imewawekea utaratibu tofauti
na wale ambao wako nje ya nchi lakini
sio katika hizo zilizotajwa.
Hapa tunaongelea wale
ambao hawako katika
nchi hizi za jirani. Hawa sheria hii
imesema kuwa wanaweza
kuitwa kufika nchini
katika mahakama husika ili
kukabiliana na mashtaka yao.
Sheria imeeleza kuwa
hawa wanaweza kuitwa
kwa njia tatu. Kwanza kwa
njia ya posta ambapo
summons itamfikia moja
kwa moja mhusika
au kupitia mtu
anayetumia naye sanduku
la barua. Hii
ni njia nzuri
na ya uhakika
zaidi.
Pili ni kwa
njia ya wakala.
Hii zaidi ni pale
ambapo mshitakiwa atakuwa
ni kampuni au taasisi.
Ikiwa ana wakala
hapa nchini basi summons hiyo anaweza kupewa wakala
na ikahesabika kuwa
ametaarifiwa na hivyo kuondoa
lawama kwa kinachoweza kutokea
mbeleni.
Tatu ni kwa kutumia
mahakama iliyo katika
nchi ambamo mshitakiwa
anaishi. Kwa mfano
kama yuko Texas marekani basi
mahakama ya Tanzania inaweza
kuitumia summons mahakama
ya Texas ambayo itafanya utaratibu wa kumpatia mshitakiwa. Hivi ndivyo
mshitakiwa aliye nje ya nchi
anavyoweza kupewa wito/summons.
4. WITO/SUMMONS
KWA MWANAJESHI.
Amri ya “v”
kanuni ya 26 ya sheria
ya mwenendo wa
mashauri ya madai inasema
kuwa ikiwa mlalamikiwa/mshitakiwa ni
mwanajeshi wa Jamhuri
ya Muungano wa
Tanzania basi wito
wake unatakiwa kupelekwa
kwa mkuu wake
wa kazi( commanding officer). Hautatakiwa
kumpa yeye moja kwa moja
isipokuwa utapitia kwa
mkuu wake na kumfikia yeye
mlengwa.
Mbali na wanajeshi
sheria hiyo inasema
pia kuwa mtu
aliye katika magereza
anaweza pia kupewa
wito ikiwa analo shauri jingine
la kujibu tofauti
na lile lililomuweka
ndani.
Sheria hiyo inasema
kuwa wito wake
atapatiwa mkuu wa
magereza wa eneo
alipo mshitakiwa. Nakala
zitakuwa mbili ambapo
nakala halisi atapewa
mkuu wa magereza
husika na nyingine atapewa
mhusika mwenyewe lakini
kupitia mkuu huyo
wa magereza.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO.
0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment