NA BASHIR YAKUB -
Makala haya yanaeleza wakati
ambapo ndugu anafariki
huku akiacha shauri
mahakamani ambalo alikuwa
akidai kitu fulani kama haki
yake. Yaweza kuwa
alifungua kesi kudai
ardhi, nyumba, mirathi,
mgogoro wa kimkataba, fidia, na
madai mengine yote. Makala
yatatizama uwezekano wa ndugu
kuendeleza madai haya
ili kuona namna ya kupata
kile alichokuwa akidai
marehemu.
1.ISEMAVYO SHERIA.
Amri ya 22 kanuni
ya 1 – 12 Sheria
ya mwenendo wa
mashauri ya madai
ndiyo inayozungumzia jambo
hili. Katika kanuni
hizo si tu
imezungumzwa haki ya
marehemu mlalamikaji bali
pia haki ya
marehemu mlalamikiwa/mdaiwa.
Kanuni ya 1 inasema
kuwa kifo cha
mlalamikaji/mdai au mlalamikiwa/mdaiwa hakiui shauri
ikiwa haki ya kulalamika
bado haijafa.
Maana yake ni
kuwa kuna wakati
mdai anakufa lakini
haki yake ya
kuendelea kudai alichokuwa
akidai inaendelea kuishi
na kuna wakati
akifa anakufa na haki yake
ya kudai. Ni wakati
gani akifa anakufa
na haki yake ya
kudai na ni wakati
gani akifa haki yake inaendelea
kuishi tutaona hapa
chini.
2. KUENDELEA KUISHI
KWA HAKI YA
MADAI NA KUFA
KWA HAKI YA
MADAI.
Kuendelea kuishi kwa
haki ya madai maana
yake ni kuwa
ndugu wa marehemu
hasa msimamizi wa
mirathi anapata haki
ya kuendeleza shauri
na kudai kilekile
alichokuwa akidai marehemu.
Na kufa kwa
haki hiyo maana
yake ni kuwa
hakuna ndugu yoyote
kutoka upande wa
marehemu akiwemo msimamizi
wa mirathi atayekuwa na
haki ya kudai
au kuendeleza shauri
ili kupata kile
alichokuwa akidai marehemu.
Hali ni hiyohiyo kwa
upande wa mlalamikiwa/mdaiwa aliyefariki. Kwani kuna
wakati ndugu watalazimika
kurithi shauri ambalo
alikuwa ameshitakiwa nalo
na kuna wakati
hawatalazimika.
3.WAKATI NDUGU
WA MAREHEMU MDAI/MLALAMIKAJI WANAPORUHUSIWA KUENDELEZA
MADAI.
Ili kujua kama
ndugu waendeleze shauri
au lah kinachoangaliwa ni aina ya shauri alilokuwa amefungua marehemu. Ikiwa alifungua
shauri binafsi( personal) au
lenye viini vya
ubinafsi(individuality) basi
shauri hilo haliwezi
kuendelezwa na ndugu
wa marehemu.
Lakini kama shauri
sio binafsi basi
ndugu wataliendeleza na
hatimaye kupata alichokuwa
akidai marehemu. Mashauri
ambayo sio binafsi
ni kama kudai
ardhi, nyumba, mirathi,
madai yatokanayo na
mikataba, na madai
mengine ya kudai
mali.
Haya ndugu wa
marehemu wanaruhusiwa kuyaendeleza
ili kupata alichotakiwa
kupata marehemu.
4.WAKATI NDUGU
WA MAREHEMU MDAI/MLALAMIKAJI WANAPOZUIWA KUENDELEZA MADAI.
Hapo juu tumeona ndugu
wa marehemu wakiruhusiwa
kuendeleza madai na
sasa hapa tunaona
wanapozuiwa kuendeleza madai. Tumesema
hapo juu kuwa
ikiwa mlalamikaji/mdai ambaye
sasa ni marehemu
alifungua shauri binafsi( personal) au lenye
viini vya ubinafsi(individuality) basi
ni wakati huo
ambapo ndugu wa
marehemu wanakosa haki
ya kuendeleza shauri
kama hilo.
Mashauri binafsi au yenye viini
vya ubinafsi ni
kama mashauri ya
fidia labda kudai fidia baada
ya kupigwa, kutukanwa,
Kudhalilishwa, kufunguliwa mashtaka ya
hila, kusababisha kufungwa
bila sababu za
msingi na
mashauri mengine yanayofanana na hayo.
Mashauri ya namna hii hufa baada
ya mdai kufa. Hayana
uhai baada ya
uhai wa mdai na hivyo
ndugu hawawezi kuyaendeleza.
Hata hivyo ikiwa
shauri la namna
hiyo lilikuwa limesikilizwa
tayari na inasubiliwa
hukumu halafu ndio
mdai akafa basi
hukumu itatolewa na
ndugu wa marehemu
watatakiwa kulipwa kile alichostahili kulipwa
marehemu ikiwa ameshinda.
Pia ikiwa marehemu
atakufa baada ya hukumu kutolewa
na kabla ya
utekelezaji(execution) napo ndugu watendeleza kupata
kile alichostahili kupata
marehemu.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO.
0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment