NA BASHIR YAKUB -
1.MIRATHI NI NINI.
Mirathi ni utartibu maalum wa kisheria unaotumika katika kiulipa madeni, kusimamia, na kugawa, mali
yote aliyoacha marehemu
kwa warithi halali.
Hakuna mirathi kabla
ya kifo.
2. JE
NANI HUTAKIWA KUWA
MSIMAMIZI WA MIRATHI.
Msimamizi wa mirathi
sio lazima awe ndugu wa
marehemu kama wengi tunavyojua. Yeyote muadilifu
na muaminifu anaweza
kuwa msimamizi wa mirathi. Hii
ina maana wanaweza
kuachwa ndugu halafu
usimamizi wa mrathi akapewa
mtu mwingine wa
nje kabisa ambaye sio
ndugu.
3. UTARATIBU
WA KUFUNGUA MIRATHI.
Utaratibu wa
kufungua mirathi hutegemea
mambo makubwa mawili ,
kwanza ikiwa marehemu
ameacha wosia na pili ikiwa
hakuacha wosia.
( a ) UTARATIBU
IKIWA MAREHEMU HAKUACHA
WOSIA.
Kitu cha kwanza
kabisa unachotakiwa kufanya
ikiwa marehemu hakuacha
wosia na mnataka kufungua
mirathi ni kuwa
unatakiwa kwenda serikali
za mitaa na
kuchukua barua maalum
ili ukapate cheti
cha kifo. Serikali za
mitaa ukiwaeleza hivyo
wanajua ni aina
gani ya barua waandae.
Cheti cha kifo
hutolewa makao makuu
ya wilaya. Kila makao
makuu ya
wilaya hutoa huduma
hiyo. Kwahiyo hatua ya kwanza
ni kuchukua barua serikali za mitaa
na kuipeleka wilayani
ili kupata cheti
cha kifo. Huwezi kufungua
mirathi bila cheti
cha kifo.
Pili, baada ya kuwa
mmepata cheti cha
kifo ndugu watakaa
kikao kwa ajili ya kumteua
msimamizi wa mirathi. Kwenye kikao
ndugu watajadiliana na
kila mtu atatoa
hoja yake na
msimamizi wa mirathi
atapatikana kwa kupendekezwa
na walio wengi kwa
kuzingatia uadilifu.
Tatu ndani ya
kikao utaandaliwa mukhtasari unaohusu kikao
hicho. Mukhtasari utawaainisha ndugu
wote waliohudhuria kikao
hicho,utaeleza ajenda zilizojadiliwa, mali za
marehemu alizoacha zitaorodheshwa, utaeleza
warithi wa marehemu
waliopo, na utamtaja
msimamizi wa mirathi
aliyeteuliwa. Zingatia
mukhtasari hutakiwa kuandikwa
kwa mkono.
Nne baada ya kuwa na mukhtasari
wa kikao cha familia pamoja
na cheti cha
kifo basi mtarejea
tena serikali za
mitaa kupata barua
ya kuwatambulisha kufungua
mirarhi. Baada ya
barua hiyo basi
mtaenda mahakamani mkiwa
na vitu hivyo
kwa ajili ya
kufungua mirathi.
( b ) UTARATIBU
MAREHEMU AKIWA AMEACHA
WOSIA.
Ni vema tujue
kuwa habari ya
kufungua mirathi mahakamani
inahusu pale marehemu
anapokuwa ameacha wosia
na pale ambapo
hajaacha wosia. Wengi
hujua kuwa marehemu
akiacha wosia na
kumteua msimamizi wa mirathi
basi haina haja
ya kwenda mahakamani.
Tofauti kubwa ya
utaratibu pale marehemu
anapoacha wosia na
pale asipoacha wosia
ni kuwa marehemu
anapoacha wosia huku
akiwa amemteua msimamizi
wake wa mirathi
basi kikao cha
familia hakitahusika na
kuteua msimamizi mwingine.
Isipokuwa kikao cha familia kitahusika
iwapo ameacha wosia
lakini hakutaja nani
asimamie mirathi yake.
Taratibu nyingine ni
zilezile kama nilizotaja
hapo juu. Muhimu ni
kutafuta cheti cha
kifo, barua ya
serikali za mitaa,
mukhtasari wa kikao
cha familia na wosia
kama upo.
4 . MAHAKAMA KUTOA
TANGAZO.
Baada ya kuwasilisha
nyaraka hizo mahakama
itatoa tangazo linaloeleza
fulani kuomba kusimamia
mirathi ya fulani
ili mwenye pingamizi
apinge . Tangazo litadumu siku 90 kabla
ya msimamizi wa mirathi
kuthibitishwa na mahakama. Tangazo hutolewa
kwenye magazeti na kwenye
mbao za matangazo
za mahakama.
Baada ya muda huo
kuisha mahakama itatoa fomu
kumthibitisha aliyeomba kusimamia
mirathi. Na ikiwa kuna
pingamizi basi mahakama
itasikiliza pingamizi hilo
na kulitolea maamuzi
kabla ya kumthibitisha
mwombaji au kumkatalia kutokana na
pingamizi hilo.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO. 0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment