NA BASHIR YAKUB -
Mgawanyo wa mali za marehemu
hutegemea mambo makubwa
mawili. Kwanza ni ikiwa
marehemu ameacha wosia
na pili ni
ikiwa hakuacha wosia.
Ikiwa ameacha wosia basi huwa
ni rahisi sana kwani mali zake
zitagawanywa kwa kufuata
wosia. Ikiwa hakuacha
wosia hapa huwa
si kwepesi sana kwani mali
zake hulazimika kugawanywa
kwa mujibu wa sheria
zilizopo wakati sheria
zenyewe
ziko tatu tofauti. Wakati mwingine ni
kazi kidogo kuamua
sheria ipi itumike katika kugawa
mali za marehemu.
1.SHERIA IPI
ITUMIKE KATIKA KUGAWA
MALI ZA MAREHEMU.
Ikiwa hakuna wosia swali
la sheria ipi
itumike katika kugawa
mali za marehemu
lazima liibuke. Kwa ujumla kuna sheria
tatu
zinazotumika katika kugawa
mirathi.
( a ) Sheria
ya kwanza ni sheria
ya
urithi ya India 1865 .
Hapa kwetu sheria hii hujulikana
kwa wengi kama sheria
ya
mirathi ya serikali.
Sheria hii hutumika
kwa marehemu ambaye hakuishi maisha
ya kiislam
na hakuishi maisha
ya kimila.
Zaidi tunaweza
kusema kuwa sheria
hii hutumika kwa
wakristo na madhehebu
mengine ambayo sio
ya kiislam.Hata hivyo
hata muislam ambaye
itathibitika kuwa hakuishi maisha ya kiislam
wala ya kimila sheria hii itatumika
kugawa mali zake.
( b ) Pili
ni sheria ya kiislam.
Sheria hii hutumiwa
na waumini wa dini
ya kiislamu. Lakini haitoshi
kusema inatumiki kwa waislam
isipokuwa inatosha kusema itatumika kwa waliokuwa wakiishi maisha
ya kiislam. Sheria hii hufuata
misingi ya Quran
tukufu na Sunnah.
( c ) Tatu
ni sheria za
kimila. Sheria hizi hutumika
iwapo marehemu aliishi
maisha ya kimila. Mfano
wake ni kama
tunavyoona kwa wamasai,
wahadzabe, na makabila
mengine hasa vijijini
ambao huishi maisha yao
yote pasi na kufuata
dini yoyote isipokuwa
mila tu. Sheria hii
imo katika kanuni
za urithi, tangazo la
serikali namba 436
la mwaka 1963.
Kwa ujumla swali la sheria
ipi
itumike kugawa mali za
marehemu pale ambapo
hakuacha wosia, hujibiwa kwa kuangalia
aina ya maisha
aliyoishi marehemu.
2. KUGAWA
MALI KWA SHERIA
YA SERIKALI.
Tumesema sheria hii inaitwa
Sheria ya urithi ya
India ya 1865 ( India
Succesion Act 1865) ila wengi
huiita sheria ya serikali.
Kwa kutumia sheria hii kama
marehemu ameacha mjane
na watoto, mjane atapata 1/3
na watoto/mtoto 2/3 ya
mali yote.
Kama marehemu hakuacha
watoto basi mjane atapata
½ na ½ inayobaki
huenda kwa wazazi, dada,
kaka wa marehemu.
3. KUGAWA
MALI KWA SHERIA
ZA KIISLAMU.
Warithi wakuu katika
sheria za kiislam
ni mke/wake wa
marehem, watoto na wazazi
wake wawili. Watoto
wa kiume hustahili
kupata mara mbili
zaidi ya wale
wa kike .
Wajane wa marehemu wasiozidi
wanne hutakiwa kupata
1/8 ikiwa marehemu kaacha
watoto. Ikiwa hakuacha watoto/mtoto
wajane
watatakiwa kupata ¼ ya mali yote iliyoachwa.
Baba na mama
hupata 1/6 ya mali
ya marehemu.
4. KUGAWA MALI
KWA SHERIA ZA
KIMILA.
Misingi ya sheria za
kimila imo katika tangazo
la serikali namba
436 la mwaka
1963.
Kwa mujibu wa sheria
hii
ikiwa marehemu ameacha
watoto basi hao
ndio watakuwa warithi
pekee. Kama marehemu hakuacha
watoto basi wazazi , kaka, dada, shangazi, wajomba
wa marehemu huwa
ndio warithi.
Aidha mtoto wa kiume mkubwa
kutoka nyumba ya
kwanza hupata fungu
kubwa akifuatiwa na watoto
wengine wa kiume
na mwisho ni watoto wa
kike kutoka nyumba
yoyote ambao hupata
kidogo. Sheria za
kimila hazitoi haki
kwa mjane kurithi.
Hata hivyo suala
la mjane kutokurithi
linapingana na katiba
pamoja na sheria
nyingine ikiwemo sheria namba
4 na 5
za ardhi..
MWANDISHI WA MAKALA HAYA
NI MWANASHERIA NA MSHAURI WA SHERIA KUPITIA GAZETI
LA SERIKALI LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI KILA
JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA JUMATANO. 0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment