NA BASHIR YAKUB -
1.LESENI HUTOLEWA KWA NAMNA MBILI.
1.LESENI HUTOLEWA KWA NAMNA MBILI.
Unapohitaji leseni ya kutafuta
madini unapaswa kujua
kuwa leseni hizi
hutafutwa kwa namna
mbili tofauti. Kwanza kwa maombi
maalum
na pili kupitia
zabuni. Sheria mpya ya
madini sheria namba
14 ya 2010 ndiyo
kiini cha makala
haya.
2.LESENI KWA MAOMBI MAALUM.
Kwa maombi maalum
ni hatua ya
kawaida ya kuomba
kama ambavyo unaweza kuomba kazi
au tenda yoyote
ambayo haijatangazwa na serikali.
Hatua hii huja
baada ya mjasiriamali
kuliona eneo la
madini na kuamini
kuwa anaweza kuwa
sehemu ya biashara
ya eneo hilo.
Maombi hufanywa katika
fomu maalum ambazo
hupatikana kwa kamishna
wa madini. Makamishna
wa madini hupatikana
hata wilayani au
mikoani hivyo inategemea
ni sehemu ipi unataka
kutafuta hayo madini.
Kubwa ni
kuwa utatakiwa kutumia
wilaya au mkoa husika katika
kupata fomu hiyo
kwa ajili ya
kutuma hayo maombi.
( a ) ILI KUPATA
LESENI SIO LAZIMA
UMILIKI KAMPUNI.
Ipo dhana inayofifisha
jitihada za baadhi ya
wajasriamali wenye ndoto na biashara
hii kwa kudhani kuwa
leseni hutolewa kwa
makampuni tu, tena
makampuni yenyewe makubwa.
Hii si kweli
kwani hata mtu
binafsi anaweza kuomba
leseni.
Hii ni kwa
mujibu wa kifungu
cha 28 ( 1 ) cha sheria
ya
madini. Kwahiyo inafaa
sana kueleweka kuwa
suala la utafutaji wa madini halihusu
makampuni bali hata
watu binafsi wanaweza
kuomba leseni hizo
na kupata.
( b ) TAARIFA
VIPI ZINAHITAJIKA KWA
MTU BINAFSI NA
KAMPUNI.
Unapotuma maombi ukiwa
kama mtu binafsi utatakiwa
kuainisha majina matatu
kamili, uraia wako, anuani
ya posta ikiwa
ni pamoja na
anuani kamili ya
makazi, sambamba na hilo
iandaliwe picha ya
sasa ya pasipoti.
Na kama ni jina la
kampuni kitahitajika cheti cha
usajili, majina ya wakurugenzi
na uraia wao. Pia kwa
wote muombaji binafsi
au kampuni atatakiwa
kuanisha aina ya
madini anayoomba kutafuta,
ikiwa ni madini
ya malighafi ujenzi,
madini ya viwandani, almasi, madini
chuma n.k.
3. LESENI KWA
ZABUNI.
Maombi kwa njia
ya zabuni yameainishwa
katika kifungu cha 29( 1 )
cha sheria ya
madini. Mchakato wa wa kawaida
wa kumtafuta mzabuni ndio utakaohusishwa katika
maombi haya.
Mamlaka husika zitatangaza tenda na
washindani watajitokeza kwa
njia ya maombi. Hapa
maombi yataandaliwa kwa
kufuata utaratibu wa
jumla utakaokuwa umeelekezwa
kwenye tangazo la
tenda hiyo.
Kwa mujibu
wa kifungu hicho
maombi yatawasilishwa kwenye
bodi ya ushauri
wa madini.
Bodi ya ushauri
wa madini ni
chombo kinachoanzishwa na kifungu
cha 23 ( 1 ) ambacho jukumu
lake kubwa ni kumshauri waziri
mwenye dhamana ya madini masuala
yanayohusu madini.
4. WAJIBU
KWA ALIYEPATA LESENI.
( a ) Kwanza ni kuanza
utafutaji wa madini
mapema ndani ya miezi mitatu tangu
kupata leseni.
( b ) Kuzingatia mpango
wa utafutaji ulioanishwa
kwenye leseni, na
( c ) Utafutaji usiwe
chini ya kiwango kwa
mujibu wa leseni
husika.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO. 0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment