NA BASHIR YAKUB -
Mtu mmoja aliyeko
Zurich alipiga simu
akiuliza swali ambalo
ni kichwa cha
haya makala . Yeye
yuko zurich lakini
anataka kufunga ndoa
na mwanamke aliyeko
Tanzania bila kulazimika
kurudi nchini. Anataka afunge
ndoa akiwa hukohuko zurich na
mwanamke akiwa Tanzania .
Alisema huko
aliko jambo hilo linaruhusiwa kisheria ila wasiwasi wake
ni kama hata
Tanzania jambo hilo linaruhusiwa. Kabla
ya kutizama jambo hilo
kisheria upo umuhimu pia wa
kutizama baadhi ya
mambo kuhusu ndoa.
1.NINI MAANA
YA NDOA.
Kwa mujibu wa
kifungu cha 9( 1 )
cha sheria ya ndoa sura
ya 29, ndoa imetafsiriwa kama
muungano wa hiari kati ya
mwanamke na mwanaume wenye
lengo la kudumu
maisha yao yote.
2. SHERIA
INASEMAJE KUHUSU WAZAZI KUCHAGUA
WACHUMBA.
Katika maana ya
ndoa kuna neno
hiari. Hili ni jambo
la kwanza katika
ndoa. Maana yake ni kuwa kusiwe na
kulazimisha, ulaghai, udanganyifu n.k. Hata kurubuni
kunakolenga kuondoa hiari
ya mtu nako
ni kulazimishwa. Pia wazazi
kuwachagulia vijana wao
wachumba na kuwashinikiza
kuwaoa au kuolewa
nao nako ni kuondoa
hiari ya wahusika.
Si kosa
mzazi kuona mchumba kwa ajili
ya kijana wake isipokuwa ni
kosa akitumia nafasi hiyo kulazimisha/kushinikiza kufungwa
ndoa. Haya ni kwa
mujibu wa kifungu
cha 16 cha sheria ya
ndoa.
3. JE NDOA YA
MKATABA INARUHUSIWA ?.
Lengo la ndoa
lazima liwe ni
kuishi wote katika
maisha yao wote. Hii
ni kwa mujibu
wa kifungu cha 9( 1 ). Maana ya
hili ni kwamba kusiwe na ndoa
za mikataba. Ndoa
za mikataba ni
kwamba mnafunga ndoa
kwa muda
maalum mtakaoona unafaa
yaweza kuwa miaka miwili, mitatu, minne
au zaidi kadri
wahusika watakavyokubaliana.
Hapa kwetu ndoa lengo lake
ni iwe maisha
yote. Hata hivyo talaka
inaruhusiwa. Hivyo basi
haiwezekani kufunga ndoa kwa muda
maalum hapa Tanzania.
4. JE SHERIA
INASEMAJE KUHUSU NDOA
ZA JINSIA MOJA.
Kifungu cha 9 ( 1 )
kimesema kuwa ndoa
ni muungano kati
ya mwanamke na
mwanaume. Maana yake
ni rahisi tu kuwa
hakuna ndoa kati ya mwanamke na
mwanamke au mwanaume na mwanaume. Uingereza,
marekani na baadhi
ya nchi za ulaya sheria
zimeruhusu ndoa
za jinsia moja.
Sisi kwetu hilo ni
haramu kabisa.
5. UMRI
WA KUOA NA
KUOLEWA NI UPI.
Kwa ujumla umri
wa kuoa au kuolewa
ni miaka 18.
Hata hivyo mwanamke
mwenye umri chini
ya miaka 18 anaweza
kuolewa ikiwa atapata
ridhaa kutoka kwa baba,
au mama na
kama wote wamefariki
basi ridhaa hiyo itatolewa
na mlezi wake. Hii ni
kwa mujibu wa kifungu
cha 17)( 1 ) cha sheria
ya ndoa.
6. JE YAWEZEKANA KUFUNGA
NDOA PASI NA
KUWEPO MWANAUME.
Ndio inawezekana. Na
si mwanaume tu bali yoyote
anaweza asiwepo kati
ya mwanaume au mwanamke. Inaruhusiwa siku
ya ndoa kuwapo
na mmoja tu kati
ya wanaotarajiwa kufunga
ndoa .Anaweza kuwa mwanaume
au mwanamke. Ndoa
haibatiliki( become void)
kwa kutokuwepo mmoja
wa wahusika. Hili
si katika mambo
yanayobatilisha ndoa.
Kwahiyo
inawezekana mwanaume akawa
Zurich na mwanamke
yuko Tanzania na
ndoa ikafun gwa Tanzania. Sharti
la kisheria la hatua hii
ni kuwa yule asiyekuwepo
awakilishwe( represented) na
mashahidi/shahidi aliyempa ridhaa.
Anachotakiwa
kufanya yule asiyekuwepo
ni kuwapa ridhaa
mashahidi/shahidi ambao ndio
watakwenda kusimama badala yake. Ndoa itafungwa
na kila kitu
kitakuwa halali. Lakini
izingatiwe kuwa mamlaka ya
uwakilishi yanaishia katika kufunga ndoa.
Uwakilishi mwingine
baada ya ndoa
hautaruhusiwa. Haya ni kwa
mujibu wa kifungu
cha 38 ( 1 ) ( j ) sheria
ya ndoa sura ya 29.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO. 0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment