NA BASHIR YAKUB -
Hatua unazopitia unapohitaji
hatimiliki ni tofauti
na hatua unazopitia
unapohitaji kubadilisha jina
katika hatimiliki( transfer). Kutafuta hati
na kubadilisha hati
ni michakato miwili
tofauti. Makala kadhaa
zilizowahi kuandaliwa zilieleza namna
ya kubadilsha hati
na sio namna
ya kutafuta hati mpya. Makala
ya leo yanaeleza
namna ya kupata
hati mpya.
1.TOFAUTI YA
KUTAFUTA HATI NA KUBADILISHA
HATI.
Unapotafuta hati maana
yake ni kuwa
ardhi yako haikuwa
na hati kabisa
na sasa unaanza mwanzo
kabisa kutafuta. Kwa wamiliki wa ardhi
za namna hii
mara nyingi ni zile ardhi
zenye mikataba ya kununulia( sale
agreement),ardhi zenye barua ya
toleo( letter of offer), na
nyingine zinakuwa hazina
waraka wowote. Kwa ardhi
za namna hii unaposema
unahitaji hati ni
lazima uanze mwanzo
kabisa.
Aidha kubadilisha hati maana yake ni kuwa,
hati inakuwepo isipokuwa
inabadilishwa kutoka jina
moja kwenda jingine.
Pengine ni muamala
wa mauziano kwahiyo
jina linatoka kwa muuzaji
kwenda kwa mnunuzi
au linatoka kwa
marehemu kwenda kwa
msimamizi wa mirathi. Kwahiyo kubadilisha
ni kubadilisha tu
na wala sio
kutafuta hati mpya.
2. HATUA
ZA KUFUATA UNAPOTAFUTA
HATI.
( a ) KUPATA COORDINATE.
Hii ni hatua
ya kwanza kabisa.
Coordinate ni kama taarifa
za kipimo maalum
ambacho hufanyika kwenye
ardhi ambayo haikuwahi
kufanyiwa kipimo hicho. Taarifa za
coordinate hupatikana kupitia
kipimo kiitwacho GPS. Kinachofanyika ni
kuwa mtaalam wa
ardhi atafika kwenye
ardhi yako na
kufanya kipimo cha
GPS.
Majibu ya kipimo
hicho atayapeleka wizarani
au manispaa kwenye
“mpango mkuu”( master plan). Master
plan ni ramani
maalum za maeneo
yote . Hivyo kupitia kipimo alichochukua
kwenye ardhi yako
kitalinganishwa kwenye hiyo
ramani ( master
plan) na kupata
taarifa kamili za
ardhi yako.
Hapo kwenye master plan
ndipo matumizi ya
ardhi zote yalipoainishwa. Kwahiyo
jibu litatoka hapo
kuwa ardhi yako
imepangwa kwa ajili
ya matumizi gani. Ikiwa
imepangwa kwa ajili
ya makazi na wewe unatafuta
hati ili ujenge
kiwanda utazuiwa.
Na ikiwa unataka
kuweka makazi wakati
matumizi yanaonesha eneo hilo ni la
makaburi au la wazi, au eneo
la shule hospitali n.k. pia haitakuwa rahisi kwako
kupata hati. Muhimu
hapa ni kuwa
hatua ya awali
ya kipimo cha
GPS ndiyo inayotoa
mwelekeo wa eneo lako limepangwa kwa ajili
ya nini na hivyo
upate hati kwa matumizi yako au
hapana.
( b ) KUPIMIWA.
Baada ya hatua
hiyo itatakiwa eneo
lako lipimwe( survey). Wataalam
wa kupima wapo wilayani
lakini pia wapo watu binafsi
wanaofanya kazi hizi
za kupima. Hakuna gharama
maalum ambayo inaweza
kutajwa hapa kwakuwa kupima ni kazi ambayo hutegemea maelewano ya
mpimaji na mpimiwaji .
( c ) MANISPAA KUTOA
FOMU NAMBA 19.
Baada ya hapo
utahitaji kuandaliwa form
namba 19 pamoja
na barua inayoeleza
historia ya kiwanja/eneo
husika.
Fomu hii pamoja
na barua huandaliwa
na manispaa. Na
manispaa inayohusika ni
ile manispaa lilimo
eneo lako. Sambamba na
hilo utaandaliwa pia barua ya
utambuzi( acknowledgement letter)
kwa
ajili ya malipo
ya ada husika. Katika
hatua hii ni lazima uwe
na cheti cha
kuzaliwa au cha uraia.
( d ) KUANDALIWA RASIMU YA
HATI.
Baada ya hayo
manispaa itaandaa rasimu
ya hati na
kuiwasilisha kwa kamishna
wa ardhi ambapo
ataisaini na kuigonga
muhuri wa moto
kabla ya kuiwasilisha
kwa msajili wa hati.
Inapotoka kwa
msajili wa hati
kwa usajili basi hati inakuwa
imekamilika na sasa
utaweza kupata hati yako
iliyo kamili.
NYUMBA KUBWA INAUZWA.
NYUMBA KUBWA INAUZWA.
1.Ina vyumba 4, kimoja master.
2. Ni nyumba kubwa nzuri.
3. Iko ndani ya fensi Sqm 1200
4. Bafu 2
5. Umeme umo na maji,jiko na public toilet.
6. Ipo mtoni kijichi.
7. Bei milioni 97 inapungua kidogo.
0784482959.
0 comments:
Post a Comment