NA BASHIR YAKUB -
Masuala yanayohusu ardhi
ni masuala nyeti
sana. Unyeti wa
masuala haya unatokana
na ukweli kuwa maisha
yote yamejengwa juu ya
ardhi. Hakuna kilichowahi
kufanywa, kinachofanywa na kitakachofanywa nje ya
ardhi. Iwe kutembea, kuendesha
kipando, kula, kulala, maendelezo
yoyote ya teknolojia, ujenzi, maji
safi na salama, kupata chakula, hata
unaporuka hewani iwe
kwa ndege au
kifaa kinginecho huwezi
kusema sijatumia ardhi kwakuwa hata mruko
wenyewe(take off) huanza na ardhi.
Lakini pia hata
uruke na ukae
huko miaka 200 bado utatakiwa
kurejea ardhini. Ardhi ni kila kitu kwa
maana ya kila kitu. Kupitia
msingi huu tunapata
umuhimu mkubwa wa
kueleza kila lililo
la msingi kuhusiana na masuala ya ardhi
hususan umiliki wake.
Kupitia makala hizi
yalishaelezwa mengi kuhusu namna
ya kununua ardhi,
namna ya kuepuka
migogoro wakati wa
ununuzi, namna ya
kubadilisha hati na
mengine . Fursa ya leo
itaeleza umuhimu na faida za
kuwa na hati.
1.NINI MAANA
YA HATIMILIKI .
Hati miliki ya
ardhi hujulikana pia kama “Title
Deed”. Hatimiliki ya
ardhi ni nyaraka
maalum inayotolewa na
wizara ya ardhi ikionesha mwenye
haki ya umiliki wa ardhi, eneo
na kiasi anachomiliki
huku ikiainisha wajibu
na haki alizonazo
mmiliki huyo.
Wajibu katika hatimiliki
ni yale unayotakiwa
kutekeleza kwa mfano
malipo ya kila
mwaka, matumizi yaliyopangwa, na kila
sharti analotakiwa kutekeleza
mmiliki.
Haki katika hatimiliki
ni yale yote anayostahili kupata mmiliki
wa ardhi husika
ikiwemo taarifa ( notice)
rasmi panapo mabadiliko yoyote katika
matumizi na umiliki, haki
ya fidia, na
haki ya kuwa
huru katika matumizi
halali.
2. TOFAUTI
YA HATI, LESENI ZA
MAKAZI, NA MIKATABA
YA KUNUNULIA.
Wengi wanajua tofauti
ya vitu hivi lakini pia
wengi hawajui tofauti
ya vitu hivi. Wapo
wanaofikiri mkataba wa
kununulia ni hati na hati ni
leseni ya makazi
na leseni ya
makazi ni hati.
Tujue kuwa hati ni
waraka ambao hutolewa
na wizara ya ardhi
katika maeneo yaliyopimwa
wakati leseni ya
makazi ni nyaraka
ambayo hutolewa na
manispaa hata katika maeneo ambayo hayajapinwa. Maeneo ambayo
hayajapimwa huitwa “ squarters”, na
kwa
kiswahili kizuri huitwa maeneo/makazi
holela.
Hapo hapo mkataba wa
kununulia sio hati
wala sio leseni
ya makazi isipokuwa
ni hivyohivyo tu
kama jina lilivyo
ni mkataba wa
kununulia(sale agreement). Ni muhimu
ijulikane kuwa hivi
ni vitu vitatu
tofauti.Mazingatio katika
vyote hivi ni kuwa hati
ni nyaraka kubwa kuliko hizi
nyingine zote.
3. FAIDA
KUU NNE ZA KUWA
NA HATI.
( a )
Faida ya kwanza kabisa
ni usalama. Nenda popote
iwe wizara ya
ardhi, mahakama kuu ya ardhi,
mabaraza ya ardhi na
kila mamlaka inayohusiana
na ardhi utaambiwa
usalama wa ardhi
upo kwa mwenye
hati.
Zawadi pekee unayoweza
kuipatia ardhi yako
ni ulinzi, na
ulinzi pekee ni kuitafutia hati. Hii
ni kusema kuwa
ardhi salama ni
ardhi yenye hati. Hii
ni faida kuu
ya kwanza unayoweza
kupata baada ya
kuwa unamiliki hati.
( b ) Hati
hupandisha thamani ya
ardhi haraka mno.
Hii ni faida
nyingine kubwa. Unaweza kununua
ardhi isiyo na
hati kwa milioni
mbili na ukaiuza
milioni hata 20
baada ya kuitafutia
hati. Wanaofanya biashara za ardhi hutumia
njia hii kujipatia
faida kubwa.
Hununua maeneo makubwa yasiyo na
hati kwa bei
ndogo huyapimisha,huyakatakata viwanja,
na kuyatafutia hati
halafu huyauza tena
kwa bei kubwa
zaidi. Ardhi yenye hati
ina thamani kubwa
mno.
( c ) Hati
ya ardhi hutumika kama
dhamana mahakamani . Unapokuwa
na hati
si tu unamiliki
ardhi bali pia
unamiliki mdhamini. Matatizo yapo
mengi ambayo mtu
hujikuta amefikishwa mahakamani. Wakati mwingine
kufikishwa mahakamani ni
jambo ambalo laweza
kukutokea bila hata
kutarajia wala kufikiri kama
kuna siku utafika huko.
Hatimiliki ni
nyaraka inayoweza kukusaidia
usiingie korokoroni .
Mara nyingi dhamana
huwa inahitaji mali isiyohamishimika ambayo
ni ardhi. Na
kitu pekee kinachothibitisha kumiliki
mali isiyohamishika ni
hati. Kupitia hati unaweza
kujidhamini mwenyewe au
kumdhamini ndugu, jamaa na rafiki.
( d ) Kupata
mkopo ni faida
nyingine ambayo sote
twaijua. Zipo taasisi za
fedha zinazokubali hata
nyaraka nyingine ambazo
sio hati lakini
kwa mwenye hati
ni uhakika zaidi. Hizi
zi faida chache kati ya
nyingi zilizopo.
ina hat
Mabaraza ya kata yanamalaka kutoa maamuzi/hukumu kwa maeneo yenye hati miliki?