NA BASHIR YAKUB -
Wakati mwingine kujilinda
waweza kukuita kujitetea,kujiokoa au kujikinga. Ni
hali ambapo mtu
hufanya jitihada za
kujinasua katika tendo
ovu ambalo linatekekezwa na mtu mwingine dhidi
yake.
Mfano wake ni
kama kuvamiwa na
majambazi, kutekwa, kufanyiwa
fujo ya aina
yoyote, kupigwa au kujaribu kupigwa n.k. Matukio ya namna
hii au yanayofanana
na haya ni sehemu
yetu ya maisha. Yumkini
yanapotutokea huw tunachukua
hatua. Na moja ya hatua ya
awali kabisa tunayochukua
huwa ni kujaribu
kujitetea au kujikinga
nayo .
Umevamiwa
nyumbani na majambazi,
umefanyiwa fujo njiani
kwasabasbu yoyote ile
na wewe unaamua
kujitetea ili usidhurike,
na katika kujitetea
huko unasababisha kifo
cha mtu, awe yule aliyetaka kufanya
fujo au mwingine mpita njia.
Sheria inasemaje kuhusu
mkasa wa aina
hii. Makala yataeleza
japo mambo ya
msingi kuhusu hali hii.
1.HAKI YA
KUJILINDA.
Haki ya kujilinda
ni haki ya
kisheria. Ni haki ambayo
ipo kwa kila
mtu. Mbali na
kuwa haki hii ni
ya kisheria pia
haki hii ni ya kuzaliwa. Kuna tofauti
kati ya haki
kuwa kisheria na kuwa ya
kuzaliwa.
Haki za
kisheria ni zile
haki zote ambazo
zimeelezwa ndani ya sheria. Zimekuwepo
baada ya sheria kutungwa na
hivyo kabla ya
sheria kutungwa hazikuwepo. Haki ya
kuzaliwa ni haki ambayo imekuwepo
tangu mwanadamu wa
kwanza alipokuwepo. Ni
haki ambayo mtu
anazaliwa nayo.
Haki hii haihitaji
kuwa ndani ya
sheria ili mtu
awe nayo isipokuwa
tu anapozaliwa nayo
huzaliwa. Hukua nayo na hufa nayo. Kujilinda au
kujitetea pale mtu anapotaka kukudhulu hakuihitaji kuwa
ndani ya sheria
ili ndo umzuie asikudhulu. Isipokuwa
ni jambo ambalo hutokea lenyewe(automatic).Lipo tu hata sheria isiliseme.
Kwahiyo pamoja na kuwa
haki ya kujilinda
usidhurike ni haki
ya kisheria lakini
kubwa zaidi ni kuwa
haki hii ni
haki ya kuzaliwa.
Haki nyingine za
kuzaliwa ni kama haki ya
kuishi, ukishazaliwa haki ya kuishi
inakuwepo sio mpaka iwe
kwenye sheria, haki ya
kuzungumza, ikiwa umezaliwa unazungumza
basi hiyo ni
haki ambayo husubiri
sheria iitoe, haki ya
kutembea n.k. Haki
ambazo si za
kuzaliwa ni kama
hizo za kuchagua au
kuchaguliwa, kupiga kura, haki
elimu n.k.
2. UNAPOSABABISHA KIFO UKIJARIBU
KUJILINDA/KUJITETEA.
Kifungu cha 18 cha
Kanuni za adhabu , sura
ya 16 kinasema kuwa mtu
hawezi kuwajibika kijinai
kwa kitendo alichokifanya
wakati wa kutimiza
haki yake ya
kujitetea, kumtetea mtu mwingine,
au kutetea mali.
Kifungu hiki kinasomwa na
kifungu cha 18c kinachosema kuwa haki
ya kujilinda, kumlinda mtu
mwingine au mali itatumika kwa mtu
yeyote ambaye katika
kutumia haki hiyo
atasababisha kifo au
dhara kubwa kwa
mtu mwingine.
Maana ya vifungu
hivi ni kuwa
haki ya kujilinda itatumika
kama kinga kukuondolea
hatia ya jinai
iwapo umesababisha kifo. Lakini
ili ikubalike kama
kinga na usitiwe
hatiani kwa kosa
la kuua vifungu
hivi vimetoa masharti
yafuatayo.
( a ) Kwanza wewe
uliyesababisha kifo uwe
umesababisha kifo hicho
kwa nia njema
kwa maana ya
kuwa ulikuwa kweli
kabisa ukijilinda usidhulike. Isije kuwa
unatumia nafasi ya
kujilinda kumuua au kumdhulu mtu
mwingine kwa makusudi
ukijifanya ulikuwa ukijilinda. Swali la
ulifanya makusudi au kwa nia
njema ya kujilinda litathibitishwa kitaalam
na mazingira ya tukio
husika.
( b ) Kitendo ulichofanyiwa
kiwe ni kitendo
ambacho kiukweli ulitakiwa
kutumia nguvu kiasi
cha kusababisha kifo. Isiwe
mnatupiana maneno mawili matatu halafu unasababisha kifo
kwa kisingizio kuwa
ulikuwa ukijilinda usidhulike. Kuwe na
mazingira ambayo hata ukiyatizama
yafanane na hatua
ya kujikinga hadi
kusababisha kifo.
( c ) Pia
ikiwa kitendo kinahusu
kubaka au kufanya kinyume
na maumbile kinga ya
kujikinga hadi
kusababisha kifo inaswihi.
( d ) Pia
kujikinga/kujitetea hadi kusababisha
kifo kunakubalika ikiwa
tendo linahusisha kuteka
nyara, au kutorosha.
( e ) Pia
matendo kama kuvunja
na kuingia, unyanganyi,
kuchoma moto, nayo
yanakubalika katika kujikinga
hadi kusababisha kifo.
Kwa kumalizia zingatieni
kuwa ikiwa upo katika mazingira
ambayo unaweza kujikinga/kujitetea bila
kusababisha kifo au
madhara makubwa basi
ni vema kufanya
hivyo. Kujikinga hadi kuua
liwe chaguo la
mwisho pale unapokuwa
huna namna nyingine
yoyote isipokuwa kufanya
hivyo.
NYUMBA HII INAUZWA BOKO.
1.Ina vyumba 3, kimoja master.
2. Uwanja unabaki mkubwa.
3. Umeme umo na maji,jiko na public toilet.
4. Ipo Boko kwa mpemba karibu na darajani.
5. Eneo zuri tulivu kwa makazi.
6. Mita 200 kutoka barabara kuu ya Bagamoyo .
7. Bei milioni 57 inapungua kidogo.
0784482959.
0 comments:
Post a Comment