NA BASHIR YAKUB -
Wote tunajua kuwa
kila atendaye kosa
sharti aadhibiwe. Na
kuadhibiwa huko lazima kuwe
kwa mujibu wa sheria. Pamoja
na kuwa mtenda
kosa hustahili adhabu
bado watenda kosa
hutofautiana hadhi. Hadhi
hapa sio kuwa
fulani ni mkuu wa
mkoa au mkurugenzi na fulani ni
mkulima wa kawaida kijijini Katanakya.
Hadhi ndio kama
hizo zilizotajwa katika kichwa
cha makala. Wapo watenda makosa
lakini wakiwa na umri
mdogo, wapo watenda
makosa lakini wakiwa
hawana akili timamu
halikadhalika wapo watenda
makosa lakini wakiwa
na akili isiyo ya kawaida
kwa maana ya
akili ya ulevi.
Sheria inasemaje kuhusu hawa wote
kuanzia utendaji wao
makosa, kushitakiwa na
kuwajibika kwao. Makala
yataeleza ili tujue
hadhi ya kimashitaka
ya makundi haya.
1.JE MWENYE
UGONJWA WA AKILI
ANAWEZA KUSHITAKIWA ?.
Jibu ni ndiyo sheria
haikatazi kumshitaki
mwenye ugonjwa wa
akili( chizi). Kuna tofauti
kati ya kushitakiwa na
kuwajibika. Kushitakiwa ni kumfungulia mashtaka
na kuwajibika ni
kupata adhabu baada ya
kupatikana na hatia. Kwa
hiyo kushitakiwa
atashitakiwa isipokuwa sheria inatoa
mwongozo kuhusu kuwajibika kwake.
Kifungu cha 13 ( 1 )
cha Kanuni za adhabu sura
ya 16 kinasema kuwa mtu hatawajibika kwa
kutenda kosa
la jinai iwapo
wakati wa kutenda
kitendo hicho alikuwa
katika hali ya ugonjwa wowote unaoathiri akili
yake. Hiyo ni
kanuni ya jumla
iliyowekwa na kifungu
hicho.
Hata hivyo kifungu
hichohicho kimeweka masharti
kuwa yapo mazingira
ambayo mwenye ugonjwa
wa akili atatakiwa
kuwajibika. Kinasema kuwa
mwenye ugonjwa wa
akili hatawajibika kwa
kutenda kosa la
jinai iwapo tu wakati
anatenda kosa alikuwa hajui
anachokitenda, hana uwezo
wa kutambua kuwa
hapaswi kutenda kosa,
na hana uwezo
wa kuzuia kitendo hicho.
Hii maana yake
ni kuwa ikiwa
mgonjwa wa akili
anao uwezo wa
kujitambua wakati akitenda kosa
basi atapatikana na
jinai hata kama ameua
kwa makusudi atahukumiwa
kunyongwa. Maswali ya
kitaalam(examination)
atakayoulizwa mahakamani ndiyo
yatakayotoa majibu ikiwa
alikuwa anajitambua wakati
wa kutenda kosa
au lah. Hii ni kwasababu
akademia ya tiba
inaonesha kuwa machizi
wengi si wakati
wote huwa hawajitambui.
Upo wakati huwa
wanajitambua na upo wakati hawajitambui. Kutokana
na hili isingekuwa
sahihi kuwaacha watende
walitakalo muda wote kwa kinga
ya ugonjwa wa
akili. Kama hili
lingeachwa kungekuwa pia
na uwezekano mkubwa
kwa wenye akili timamu
kutumia nafasi hiyo
kutenda jinai huku
wakitegemea kinga ya utimamu wa
akili.
2. JE
ULEVI NI KINGA
BAADA YA KUTENDA
KOSA ?.
Kifungu cha 14(1) cha
Kanuni za adhabu kinasema
kuwa kulewa hakutachukuliwa kama
kinga dhidi ya kosa
lolote la jinai. Hii ni kanuni
ya jumla. Yumkini yapo
mazingira ambapo ulevi
unaweza kuwa kinga
baada ya kutenda
jinai.
Tunaposema kinga tunamaanisha
kuwa mtu atashitakiwa
lakini atajitetea kuwa nilikuwa
nimelewa au sina akili
timamu na kutokana
na utetezi huo
atatakiwa kuachiwa huru. Hii ndio maana
ya kinga.
3. MAZINGIRA
AMBAYO ULEVI NI KINGA BAADA
YA KUTENDA KOSA.
Ili kulewa iwe
kinga baada ya
kutenda jinai sharti
la kwanza ni
kuwa wakati mlevi
anatenda kosa iwe
kweli ulevi ule
ulimfanya awe hajitambui
kiasi cha kutojua
anachotenda.
Pili ni kuwa
ulevi ule usiwe
umepatikana kwa hiari
yake.Na hili ndio
la msingi sana. Ukienda mwenyewe kilabuni
au nyumbani kwako
ukanywa ukalewa ukawa
hujitambui na hatimaye
kutenda jinai ulevi
haitakuwa kinga kwako abadan. Ili
iwe kinga ni
lazima iwe haukulewa
kwa hiari yako.
Hii
ina maana kuwa
ulilazimishwa kulewa au ulileweshwa. Kuleweshwa
au kulazimishwa kulewa
hapa sio kununuliwa
pombe ukanywa, hapana.
Kuleweshwa au kulazimishwa kulewa
ni kwa mfano
umechanganyiwa pombe kwenye
kinywaji kingine bila
wewe kujua au umewekewa
dawa za kulevya
kwenye chakula,kinywaji bila
wewe kujua. Hapa ndipo
ulevi unaweza kusimama
kama kinga na
hivyo kuondokana na
hatia ya jinai.
Mazingira mengine ambapo
ulevi unaweza kuwa kinga
ni pale ambapo mwenye
ugonjwa wa akili na
kutokana na ugonjwa
huo atajilewesha mwenyewe na
kutokana kulewa huko akatenda
jinai. Ulevi utakuwa kinga
kwake kwakuwa uchizi ndio
ulimsababisha alewe na hivyo
haikuwa katika hiari
ya kawaida. Kwa
ujumla niseme tu
hivi ndivyo ilivyo kwa
hili la ulevi
na kutokuwa na
akili timamu.
NYUMBA HIZI ZINAUZWA.
A. 1. Ina vyumba 3.
2. Uwanja unabaki.
3. Ipo kigamboni, kibugumo.
4. Ni karibu na mji mwema.
5. Mita 300 kutoka barabara kuu ya lami .
6. Bei milioni 30 inapungua kidogo.
0784482959.
B.
NYUMBA MBEZI JOGOO.
1.Ipo Mbezi Jogoo karibu na kiwanda cha COTEX
2. Ina vyumba 3 , bafu 2.
3. Iko kwenye fensi ya kuingia magari 3.
4. Bei milioni 120 inapungua.
0784482959
0 comments:
Post a Comment