NA BASHIR YAKUB -
Kupitia makala haya
wako Watanzania ambao wanao marafiki
wa kigeni, wanao
wafanyabiashara wenzao wa
kigeni, ndugu wa
kigeni, na wengine wanahisa
wenzao katika makampuni
mbalimbali ambao wangependa
wenzao hao wapate
ardhi ya uwekezaji
Tanzania.
Makala haya
ni nafasi kwao
kujua mambo ya
msingi ya awali
kuhusu namna ya
kupata ardhi kwa
hao wageni.
Aidha mara kadhaa makala
yetu yameeleza taratibu
mbalimbali ambazo Mtanzania
huweza kupitia ili
kupata haki ya
kumiliki ardhi. Sanjari na
hilo imeelezwa mara nyingi pia namna
nzuri ya kuweza kupata
ardhi huku ukiepuka
migogoro ambayo huwaingiza
wengi katika hasara ikiwa
ni pamoja na
kuwapotezea muda.
Iliwahi kuelezwa
hapa kuwa Mtanzania
anaweza kupata ardhi kwa kununua,
kurithi, kuzawadiwa, njia ya fidia,
na kwa kutwaa eneo
lisilo na mmiliki.
Hii ni kwa raia wa
Tanzania. Yumkini raia wasio
watanzania nao wanazo
haki zao katika
ardhi yetu. Raia wasio
Watanzania wanaweza kupatiwa
ardhi kwa ajili ya
matumizi. Kubwa kwao hupatiwa ardhi kwa
ajili ya uwekezaji
kwa manufaa ya
taifa.
Kupitia hili zipo
namna tano ambazo
raia wasio Watanzania wanaweza
kupitia hadi kupatiwa ardhi.
1.SHERIA ZINAZOWARUHUSU WAGENI
KUPATIWA ARDHI.
Sheria kuu inayowaruhusu
raia wa kigeni
kupatiwa ardhi nchini ni sheria
namba
4 sheria ya
ardhi ya mwaka
1999. Kifungu cha
19( 2 ) cha sheria
hii kinasema kuwa mtu au kikundi
cha watu ambacho
kimejiunga kama kampuni
au bila kampuni
ambacho wahusika wake
ni raia wa
kigeni wanaweza kupata
haki ya kumiliki
ardhi kwa ajili
ya uwekezaji.
Sheria nyingine inayotoa
mwongozo kwa raia
wa kigeni kupata ardhi
Tanzania ni sura
ya 38 sheria ya
uwekezaji ya mwaka
1997. Sheria hii hueleza
namna ya kumpatia mwekezaji ardhi,
matumizi, na muda wa mwekezaji
mgeni kutumia ardhi
hiyo.
2. NAMNA
MGENI ANAVYOOMBA KUMILIKI
ARDHI.
( a ) Anachotakiwa kufanya raia
asiye Watanzania anayetaka
ardhi ya Tanzania
kwa shughuli za
uwekezaji ni kuomba ardhi hiyo
kupitia kituo cha
uwekezaji Tanzania. Hii itakuwa
ni njia ya
kwanza kabisa. Maombi
yake ya awali
hatatakiwa kuyapeleka kwingine
kokote isipokuwa kituo
cha uwekezaji Tanzania.
Maombi hayo huwasilishwa
kwa kujaza fomu
maalum zinazopatikana hapohapo
kituo cha uwekezaji. Pamoja na
mambo mengine mgeni
atatakiwa kujaza eneo
linaloonesha anahitaji ardhi kwa uwekezaji
wa aina gani.
Baada ya kuwasilisha
maombi hayo itakuwa
sasa ni kazi ya
kituo cha uwekezaji
Tanzania kuwasiliana na Wizara ya
ardhi ambayo itatafuta
ardhi hiyo kwa ajili
ya mwekezaji. Baada ya
kupatikana ardhi hiyo
wizara itatangaza ardhi
hiyo kwenye gazeti
la serikali kuhusu
hatua hiyo.
Baada ya tangazo wizara
itakimilikisha kituo cha
uwekezaji ardhi hiyo . Wizara
inakimilikisha kituo cha
uwekezaji na kituo
cha uwekezaji kinatoa
hati mbadala ya matumizi ya
ardhi kwa mgeni.
( b ) Kupangisha kutoka
sekta binafsi( sub-lease from private
sectror). Sekta binafsi
wana umoja wao
ambao hujumuisha wawekezaji
wa kigeni pia. Kupitia
sekta binafsi wamo wawekezaji ambao
humiliki ardhi ambayo
huruhusiwa kutolewa kwa
wawekezaji wengine kupitia
kupangisha.
Upangishaji
kupitia njia hii waweza kuwahusu
hata watu wengi
zaidi kwa maana kuwa
A anaweza kumpangisha
B na B akampangisha
C. Kubwa ni kuwa
wasivunje masharti ya matumizi
bora ya ardhi kwa
mujibu wa kituo
cha uwekezaji na wizara.
( c ) Kununua kutoka
kwa wamiliki wengine. Mgeni hazuiwi
kununua ardhi kutoka
kwa watu wengine. Sharti ni
kuwa awasiliane na
kituo cha uwekezaji
kwa ajili ya
taratibu za mgeni
kupata ardhi.
( d ) Kuomba moja
kwa moja ardhi kwa
kamishna wa ardhi. Hapo juu
tumeona mwekezaji ataomba
kupitia kituo cha uwekezaji. Hapa
mgeni anaweza kuomba moja
kwa moja ardhi
wizarani badala ya kupitia
kituo cha uwekezaji.
Sharti kubwa ni
kuwa awe na cheti cha
uthibitisho(certificate of approval) kutoka
kituo cha uwekezaji.
( e ) Tano
na mwisho ni
kuwa mgeni anaweza
kupata ardhi kwa
kupatiwa tu leseni
kutoka serikalini kwa
ajili ya matumizi
maalum. Kwa ujumla hizi
ni namna tano
ambazo mwekezaji mgeni
anaweza kupata ardhi.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO. 0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment