NA BASHIR YAKUB -
Masuala ya msingi
yanayohusu ardhi za
vijiji yanasimamiwa na sheria
namba 5
ya ardhi za
vijiji. Sheria hii ilitungwa
mwaka 1999 na
kuanza kutumika rasmi
Mei 2001. Upo
mwamko mkubwa wa wananchi
hasa wa maeneo ya
mijini na wale walio
nje ya nchi wa kununua
maeneo ya vijiji
kwa ajili ya
shughuli mbalimbali za
uwekezaji na uchumi
kwa ujumla.
Hata hivyo wengi
wao wamekumbwa sana
na migogoro huko
wanakonunua. Sababu za
migogoro hii ni
nyingi. Lakini mojawapo ni
kutokuzingatia mambo ya
msingi na ya
kisheria wakati wa
kupata ardhi hizo.
Nani asiyejua
sasa kuwa migogoro
baina ya wawekezaji
na wanavijiji ni janga,hakika hakuna.
Ni aghalabu
kufungulia runinga au
redio usisikie mgogoro wa ardhi
baina ya wanakijiji
na mwekezaji. Ni sababu hii inayopelekea makala
haya na makala
nyingine zilizopita kueleza
japo baadhi ya
mambo ya msingi na ya
kuzingatia unapoelekea
kumiliki ardhi ya kijiji.
1.NANI ANA
HAKI YA KUTOA
UMILIKI WA ARDHI
YA KIJIJI.
Kifungu cha 25
cha sheria ya
ardhi ya vijiji
kinasema kuwa Halmashauri
ya kijiji ndicho chombo chenye mamlaka
ya kutoa umiliki
wa ardhi ya
kijiji. Usikubali kuuziwa ardhi ya kijiji na
chombo kingine chochote
mbali na chombo
hiki.
Wengi wamenunua ardhi
kwa kuuziwa na mtendaji
kata, sijui mwenyekiti,
sijui balozi wa nyumba
kumi na hata wengine wameuziwa na
watu binafsi. Ardhi
ya kjiji hutolewa
na halmashauri ya
kijiji na hii ni kwa mujibu sheria.
Utakapokuwa
umeuziwa na chombo
tofauti , tafsiri yake ni
kuwa hujanunua umegawa
hela.
Maana yake ni
kuwa muda wowote
wanakijiji na serikali
yao wataomba kurudushiwa
ardhi yao. Umakini unahitajika
sana eneo hili
kwakuwa wengi wameuziwa
na mamlaka/watu ambao
hawana uwezo wa
kuuza ardhi ya
kijiji kisheria. Migogoro
mingi ina sura ya mtu
kumiliki ardhi katika
kijiji huku kijiji kikidai
kutomtabua. Sababu ni hii kuuziwa
na watu wasio na
mamlaka.
2. NI
NYARAKA IPI UNAYOIPATA
UNAPONUNUA ARDHI YA
KIJIJI.
Kipo kitu kinaitwa cheti
cha hakimiliki ya kimila( customary right
of occupancy). Hiki ndicho
kitu kinachotakiwa kutolewa
unapokuwa umenunua ardhi
ya kijiji. Cheti
hiki ndicho nilichosema
hapo juu kuwa
kinatolewa na halmashauri
ya kijiji.
Usikubali kuambiwa
umenunua ardhi ya
kijiji bila kupatiwa
cheti hiki. Hii ni
kwakuwa uhalali wa
umiliki wako unategemea hiki cheti.
3. CHETI
CHA HAKIMILIKI KINAKUWAJE ?.
( a ) Kinakuwa katika
mfumo wa fomu maalum.
Ni fomu ambayo
ina kichwa cha serikali ya
kijiji husika.
( b ) Kitakuwa na
sahihi ya mwenyekiti
wa kijiji na
katibu wa halmashauri
ya kijiji. Ni muhimu
ukayazingatia haya ili unapopewa cheti
hiki uhakikishe kiko
hivyo ili kuepuka
ulaghai.
( c ) Lazima kiwe na
sehemu ya sahihi au
dole gumba la mwombaji/anayemilikishwa/mnunuzi.
( d ) Lazima kitiwe
sahihi na kusajiliwa
na afisa ardhi
wa wilaya. Wilaya
inayohusika ni ile
ambayo kijiji husika
kimo.
Kwahiyo ni muhimu
kwako kuhakikisha hakimiliki ya
kimila unayopewa baada
ya kununua ardhi
ya kijiji inakuwa
katika muonekano wenye
maudhui haya .
4. MUDA WA KUOMBA
KUMILIKI ARDHI YA
KIJIJI.
Maombi ya nia
ya kumiliki ardhi
ya kijiji yatawasilishwa mbele
ya Halmashauri ya
kijiji. Usipeleke maombi haya kwa
mtu binafsi, au
kwa mtendaji wa kijiji/kata pekee, au
mwenyekiti pekee, au
balozi pekee. Maombi yanawasilishwa kwa Halmashauri nzima.
Sheria namba 5 ya
ardhi ya vijiji
inasema kuwa utatakiwa
kujibiwa maombi yako
ya kumiliki ardhi
ndani ya siku 90 tokea
siku ulipowasilisha maombi
hayo. Halmashauri ya kijiji
ndicho chombo chenye
wajibu wa kuhakikisha
kinatoa majibu ya
kukubaliwa au kukataliwa
ndani ya muda
huo wa siku 90.
5. NASAHA.
Ni ushauri mujarabu
kuwa ni muhimu
sana kupata mwongozo
wa wanasheria kabla
ya kuingia katika
muamala huu wa
manunuzi. Hii ni kwakuwa zipo
taratibu nyingi hata
ambazo hazijaelezwa humu zinazohitaji ufanunuzi
wa kisheria wakati na kabla ya
kununua ardhi.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI LA HABARI
LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO. 0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
0 comments:
Post a Comment