Tuesday 12 January 2016

JE UNAHITAJI “NGO”, UJUE UTARATIBU MZIMA WA KUSAJILI.

Image result for NGO TANZANIA\


NA  BASHIR  YAKUB.

NGO  ni  kifupi  cha  neno  Non  Government  Organisation.  Kwa  Kiswahili  neno  hili  humaanisha  shirika  lisilo  la  kiserikali. Kawaida  serikali  huwa  ina  mashirika  yake, kwa  mfano  shirika  la  bima, shirika  la  nyumba,shirika  la umeme,mashrika ya vyakula n.k. 

Tunapozungumzia  NGO  maana  yake ni  kuwa  ni mashirika  ambayo  kwa  namna  yoyote  ile  serikali haihusiki  na  umiliki  wake. Ni  mashirika ambayo  humilikiwa  na   watu  binafsi.  Serikali huweza kushirikiana  nayo  tu lakini  si  kuyamiliki.

Taratibu  za  uanzishaji,  usajili  na uendeshaji  huratibiwa bayana  na  Sheria  ya  mashirika  yasiyo  ya  kiserikali Na 24, 2002.

1.YAPI  YAWE  MALENGO  YA  KUANZISHA  NGO.

Malengo  makuu  ya  kuanzisha  NGO  yawe  ni  kusaidia  makundi  au  kundi  maalum  katika  jamii.  NGO  sio  shirika  la  biashara.  Sio  kampuni  ambayo  muanzishaji  wake hutaraji  kutengeneza  faida. NGO  ni  shirika  la  hisani.  Ni  shirika  la  kujitolea  kusaidia  makundi  jamii.  Usitegemee  kuanzisha  NGO  kwa  ajili  ya  kutengeneza  faida  ya  fedha.

2.   MGAWANYO  WA  USAJILI  WA  NGO.

Usajili  wa  NGO  umegawanyika  katika  makundi  makuu  manne. Kwa  mujibu  wa  sheria  mgawanyo  huu  umelenga  maeneo  ya  kijiografia. Hata  hivyo  ada  za  usajili  na  mambo  mengine  muhimu  katika  usajili   hutegemea  mgawanyo  huu.  

Kwanza  kuna  mgawanyo  wa usajili  wa  ngazi  ya  wilaya. Usajili  wa  aina  hii  huiwezesha  NGO  kufanya  shughuli  zake  ndani  ya  mipaka  ya  wilaya.  Husajiliwa  hapohapo  wilayani  na  hufanya  kazi  zake  ndani  ya  mipaka  hiyo.

Pili usajili  ngazi  ya  mkoa. Huu huhusisha  usajili ngazi  ya   mkoa na  mipaka ya  kazi  itakuwa  ni  ndani  ya  mkoa  husika.

Tatu  usajili  ngazi ya  taifa  ambao  hufanyika  makao makuu  na  mipaka  ya  kazi  ni  taifa  zima. Nne ni   usajili  ngazi  ya  kimataifa  ambao  huiwezesha  NGO kufanya  kazi  zake katika  taifa  zaidi  ya  moja.

3.  WAPI  UKASAJILI  NGO.

Kwa  ngazi  ya  wilaya  nenda  makao  makuu  ya  wilaya  yako,  na  ulizia  afisa  maendeleo  ya  jamii.  Hawa  ndio  huhusika  na  usajili. Halikadhalika  ngazi  ya  mkoa utaenda  makao  makuu  ya  mkoa  wako   ndipo  usajili  utakapofanyika.

Aidha  kwa  ngazi  ya  taifa  usajili  hufanyika  makao  makuu  ya  wizara  kwa  msajili  wa  NGO. Kwa  sasa  wizara  husika  ni  Wizara  ya  Maendeleo  ya  Jamii,Jinsia  na  Watoto. Wasajili  wa  ngazi  zote  hupata  mamlaka  ya  kusajili kutoka  kifungu  cha  22(1) cha  sheria  ya  mashirika  yasiyo  ya  kiserikali.

4.  VITU  GANI  VINATAKIWA  KATIKA  USAJILI.

( a ) Katiba  ya NGO.  Hizi  hutakiwa  nakala  tatu  zilizojaladiwa( binding).

( b ) Maelezo  binafsi  ya  viongozi  watatu wa  NGO. Mwenyekiti, Katibu, na  mhazini.  Maelezo  binafsi  ni  wasifu( CV) pamoja  na  picha  mbili  za  kila  mmoja.

( c ) Mukhtasari  wa  kikao  cha  kuanzishwa  kwa  NGO  ukienda  sambamba  na  majina na  sahihi  za  waanzilishi.

( d )Fomu  ya  maombi  ya  usajili  iliyojazwa ( NGO FORM NO 1). Hii  hupatikana  kwa  msajili. Itatakiwa  kubandikwa  ushuru  wa  stempu wa  Tshs 1500/=.

( e ) Barua  ya  utambulisho  kutoka kwa  afisa  maendeleo  ya  jamii  wa wilaya, mkoa  husika.

( f  )  Taarifa  nyingine  yoyote  ambayo  msajili  anaweza  kuomba kutoka  kwako.

5.  ADA  ZA  USAJILI  NI  KIASI  GANI.

Ngazi  ya  wilaya 80,000/=,  ngazi  ya  mkoa 100,00/=, ngazi  ya  taifa 115,000/=  na  kimataifa  dola  za  kimarekani 350.

                      NYUMBA  HII  INAUZWA  BUNJU "B".



1. Ina vyumba 3, kimoja master na fremu ya duka mbele.
2. Ipo ndani  ya  fensi  kubwa sana.
3. Umeme, maji vimo ndani, jiko na public toilet.
4. Ipo Bunju B  mkono  wa kulia ukitokea mjini.
5. Eneo zuri tulivu kwa makazi.
6.Ni nyumba yenye eneo kubwa.
7. Mita chache kutoka  barabara  kuu ya  Bagamoyo .
8. Bei milioni  90 inapungua .
0784482959.


13 comments:

  • gmushema says:
    14 September 2017 at 07:50

    JE NI UTARATIBU UPI WA KUSAJIRI VIKUNDI VYA KIJAMII KWA WATU WENYE MALENGO YANAYOFANANA(SOCIAL CLUBS)?

  • Unknown says:
    19 January 2018 at 00:57

    Namna gani ya kusajili Open Schools? Naomba kujua utaratibu wake

  • Unknown says:
    7 June 2018 at 01:45

    kazi nzuri wakuu

  • Unknown says:
    11 August 2018 at 04:53

    Asante nimekuelewa

  • Unknown says:
    1 December 2018 at 13:34

    Asanteni sana ila naomba niulize je kama ni NGO kutoka nje ya nnchi nini inaombwa ili isajili katiba nchini Tanzania.

  • jojooprincess says:
    17 August 2019 at 05:40

    Enter your comment...mm naomb kuuliza Utartbu kwa NGO isiyo ya kikundi cha watu

  • Unknown says:
    5 October 2019 at 03:14

    Naomba kujua faida za NGOs

  • Unknown says:
    27 March 2020 at 21:12

    Je, namna ya kupata wafadhili ni njia ipi niitumie.!?

  • Zephania m mlimangombe says:
    17 October 2020 at 21:02

    Ipo vzur

  • Yunge Nyanda says:
    7 April 2021 at 06:59

    Ili kupata misaada ya kusaidia haya makundi katika jamii nafanyaje kuwapata kwa urahisi

  • Tanzania Motivational Foundation says:
    25 May 2021 at 11:59

    Nimeelewa vizuri

  • Unknown says:
    21 June 2021 at 03:28

    Kwaiyo hakuna shirika la kutengeneza Faida mkuu

  • Unknown says:
    21 December 2021 at 01:00

    Nimekuelewa ntakutafuteni kwa msaada zaidi, kwa sasa ofisi inayohusika na kufungua NGO's iko wapi?

Post a Comment