NA BASHIR YAKUB -
Biashara hufanywa kwa
mitindo ya aina nyingi
kutegemea na mahitaji
ya wahusika. Unaweza kufanya biashara kwa
mtindo wa kampuni,
unaweza kufanya biashara
kwa mtindo wa
mtu binafsi, lakini pia
unaweza kufanya biashara
kwa mtindo wa shirika
( firm)/ubia. Mitindo hii
yote inatofautiana
kiutendaji, kifaida na kiuwajibikaji (liability).
Kuhusu kampuni tumeeleza
mara nyingi faida
zake, aina zake, masuala
ya hisa, mpaka namna
ya kuunda kampuni, ada
zinazostahili na kila kitu. Pia
yapo makala yaliyoeleza
biashara binafsi hasara
na faida zake. Leo katika
makala haya tutapata
kuona biashara ya shirika (firm)/ubia . Tukumbuke kuwa
haya yote ni
mazao ya sheria na
hivyo huwa tunayatizama
kwa mtazamo wa
sheria.
Sheria imeeleza kwa
mapana kabisa aina
zote hizi za
biashara ili kuepusha
migongano baina ya
wahusika. Sura ya
345 ya sheria
ya mikataba iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002
ndiyo inayozungumzia shirika/ubia kama tutakavyoona.
1.SHIRIKA/UBIA NI NINI.
Shirika/Ubia ni uhusiano
uliopo baina ya watu wanaofanya
biashara ya
faida kwa pamoja . Kwa hiyo ili
ubia uwepo ni
lazima watu wawili
au zaidi waungane
na waamue kufanya
biashara kwa pamoja. Hii
ni kwa mujibu
kifungu cha 190
cha sheria ya
mikataba. Kuungana huku ili
kufanya biashara sio
kuunda kampuni.
Ni
kuungana ambako hakuhusishi
kampuni lakini kunakotambulika kisheria. Muungano wa
kufanya biashara kwa pamoja
ndio ubia.
Watu walioingia ubia
kwa umoja wao
wanaitwa shirika ( firm). Kwa
hiyo shirika na ubia humaanisha kitu
kimoja na ndio maana katika
makala maneno haya
yanatumika pamoja. Na
jina wanalotumia wabia linaitwa jina
la shirika ( firm name).
Mifano
ni mingi ila
mojawapo ni yale
mashirika ya wanasheria
yaitwayo law firm, au ya
wahasibu yaitwayo accountant
firm na mengine mengi. Lakini
hata katika biashara
za kawaida za uuzaji
wa bidhaa na
mengineyo nako ubia hufanyika.
2. TOFAUTI YA SHIRIKA
UBIA (PARTNERSHIP FIRM ) NA KAMPUNI (COMPANY).
Tofauti ni nyingi
ila hizi ni
baadhi :
( a ) Katika shirika (firm) ikiwa
kuna mkopo umekopwa
na shirika kwa ajili ya
biashara fulani basi
wanashirika wote wanawajibika kwa
deni hilo kila
mtu mmoja mmoja
kwa nafasi yake.
Na ikiwa shirika litashindwa kulipa
basi mali binafsi
za kila mmoja
ya washirika zinaweza
kukamatwa kulipia deni
hilo. Hii haipo kwenye
kampuni. KatIka kampuni haiwezi
kutumika mali ya
mtu binafsi mwanahisa
kufidia deni ambalo
kampuni imeshindwa kulipa hasa
kama mali hiyo haikutumika kama
rehani. Ni mali ya
kampuni tu itakayotumika.
( b ) Shirika linaposababisha hasara
kwa mtu mwingine ambaye
sio mwanashirika kwa
maana ya mtu
wa tatu basi
wanashirika(partners) wanawajibika
kufidia hasara hiyo kwa
michango
yao. Hii ni tofauti na kwenye kampuni
ambapo wenye kampuni
hawawajibiki kufidia hasara
iliyosababishwa na kampuni
kwa mtu ambaye
si mhusika katika kampuni
hiyo. Kampuni kama kampuni
ndiyo inayowajibika kufidia
hasara hiyo na
si wenye kampuni. Mali
za kampuni ndizo
zitakazotumika na
kama hazipo hilo
ni jambo jingine. Muhimu ni kuwa mali
za wenye kampuni
hazitaguswa.
( c ) Katika ubia hakuna
mtu anaweza kualikwa
kuwa mbia katika
shirika bila ridhaa
ya wabia wote.
Kila mbia ni lazima aridhie
ujio wa mbia
mpya. Katika kampuni hasa
makampuni ya umma (public
company) haihitajiki ridhaa
ya wana hisa wote
ili mtu mpya akubaliwe kuwa
mwanahisa.
3. KANUNI
KUU ZINAZOONGOZA SHIRIKA (FIRM).
Kanuni kuu inayoongoza
shirika ni makubaliano ya kimkataba. Kile mnachokubaliana kimkataba ndicho kinachotakiwa
kutekelezwa. Kama hakuna makubaliano
yoyote basi masharti
yaliyo katika kifungu
cha 194 cha sheria
ya
mikataba ndiyo
yatakayotumika kama makubaliano
yenu. Masharti hayo ni
pamoja na kila
mbia kuwa sehemu
ya uongozi wa shirika,
maamuzi kufanywa kwa kura
za walio wengi, haki
ya kukagua vitabu
vya shughuli za shirika, kugawana faida
kwa usawa, n.k.
4. SHIRIKA (FIRM) HUSAJILIWA WAPI.
Mashirika (firm)
husajiliwa kwa msajili
wa makampuni na
biashara BRELA. Vipo vyeti
maalum ambavyo hutolewa kwa
ajili ya usajili baada ya ada
ya usajili hulipwa. Katika
makala nyingine tutaona kipi
bora kibiashara kati ya
shirika (firm) na kampuni ( company).
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
Nimefarijika Kupata Elimu Katika Mada Zako Pamoja Na Uwasilishaji Wako Unazingatia Mambo Mengi Nikushukuru Na Kukupongeza "hongera Sana" Napenda Kujua Zaidi Ili Niweze Kuishi Kwa Utaratibu Na Jamii Inayo Nizunguka Pia Ningependa Kufaham Mengi Kuhusu Wadhifa Pamoja Na Taaluma Yako Inawezaje Kutukomboa Zaidi Tushiriki Wote Katika Kuleta Mabadiliko Na Tusikate Tamaa. Aksante ACDO GEITA-MBOGWE, ZAWAD MGHERO
Ahsante ndugu kwa elimu hii hakika umeongeza vitu vingi akilini mwetu wafuasi wa blog hii
Nashukuru nimeyafahamu mengi Sana kuhusu sheria ya Ardhi pamoja Na nyinginezo. Mungu akubarikie maisha marefu uendelee kutujuza tusiyoyajua.
Ahsante Sana kwa makala hii imenifundisha, lengo kuu nilitaka kujua kanuni za mikataba ya mashirika ili Mimi na wenzangu tuanzishe biashara ya kushirikiana
mashallah !! special thanks to you !!
🙏🙏🙏