NA BASHIR YAKUB -
Wapo mawakala na wapo wanaohitaji
kuwa mawakala. Kwa sasa biashara
ya uwakala ni
kubwa mno, wapo mawakala
mitandao ya simu kama tigo, Airtel, voda n.k, mawakala makampuni ya
usafirishaji kama mabasi, malori n.k , na makampuni
mengine mengi. Mtindo wa
biashara ya uwakala
umekua sana katika
siku za hivi
karibuni.
Ni kutokana na
ongezeko la makampuni
na kukua kwa
biashara. Upo umuhimu
mkubwa wa kuijua
biashara ya uwakala
kwa undani hasa
katika misingi ya
kisheria . Hii itakusaidia kuzijua
haki zako. Usipozijua haki
zako za kisheria
katika biashara kama
hii ni vigumu
kunufaika. Hii ni kwasabbu
hutojua unastahili
nini na nini
hustahili. Ili kuliepuka
hili unajikuta katika ulazima
wa kuzijua taratibu
za kisheria zinazohusu
uwakala. Usiingie katika biashara hii
bila kujua japo mambo kidogo
ya msingi ya kisheria
yanayohusu uwakala.
1.WAKALA NI NANI.
Sura ya 345
kifungu cha 134 cha
sheria ya mikataba kinaeleza
nini maana ya
wakala. Kinasema kuwa
wakala ni mtu aliyeajiriwa
kufanya kazi au
kitu chochote kwa
niaba ya mwingine au
kumwakilisha mtu mwingine
katika shughuli fulani. Kwahiyo
wakala ni mtu
anayesimama badala ya mtu
mwingine.
Huyo mtu mwingine
huitwa mhusika mkuu. Kwahiyo
wakala hufanya kazi kwa niaba ya mhusika
mkuu. Humwakilisha mhusika mkuu.
2. SIFA ZA KUWA WAKALA.
Vifungu vya 135 na 136 vinaeleza sifa za mtu kuwa wakala au kuwa mhusika mkuu. Vinaeleza kuwa mtu yeyote mwenye umri wa mtu mzima yaani mwenye umri wa miaka 18 na kwenda mbele anaweza kuwa wakala. Lakini pia ni lazima awe na akili timamu. Kwa sifa hizi pia unaweza kuwa mhusika mkuu. Hata hivyo hizi ni sifa za jumla za kisheria, yumkini zipo sifa nyingine kutegemea na mhusika mkuu anahitaji wakala wa aina gani kwa ajili ya biashara zake.
3. MAMLAKA ALIYONAYO WAKALA.
Kwa mujibu wa kifungu cha 38 wakala anayo mamlaka makuu ya aina mbili. Kwanza mamlaka ya kutamkwa(expres) na pili mamlaka ya kumaanisha(implied). Mamlaka ya kutamkwa ni yale yote ambayo ameambiwa kwa mdomo au kwa maandishi kuyatekeleza . Ni yale yaliyo katika mkataba wake alioingia na mhusika mkuu.
Pili ni mamlaka ya kumaanisha. Haya hayapo katika mkataba wake na wala hakuambiwa na mhusika mkuu lakini ameyatekeleza. Haya ni yale ambayo wakala huyatekeleza kwa nia nzuri au kwa lengo la kuikoa biashara na jambo fulani ambalo limetokea ama kwa dharula au vinginevyo.
Ikiwa wakala amefanya jambo jema na kwa nia njema hata kama halipo katika makubaliano kati yake na mhusika mkuu basi jambo hilo huhesabika ni sehemu ya mamlaka yake na mhusika mkuu hawezi kukataa kuliwajibikia kwa kisingizio kuwa halipo katika makubaliano.
4. HAKI YA WAKALA KUZUIA MALIPO YA MHUSIKA MKUU.
Ikiwa wakala anafanya biashara ambayo anatakiwa kuwasilisha pesa za mauzo kwa mhusika mkuu na ikatokea kuwa hajalipwa malipo yake basi anaweza kuzuia malipo ya pesa hizo ili kufidia hela anayodai. Muhimu ni kuwa asizuie pesa nyingi zaidi kuliko kiasi anachodai.
Pamoja na hayo kifungu cha 172 kinasema hakutakuwa na malipo kwa wakala kwa kazi aliyoiharibu. Wakala anatakiwa kuwa mwangalifu, mtiifu kwa maelekezo ya mhusika mkuu, na kujiepusha na uzembe au kutojali. Hasara anayoisababisha kutokana na haya itakatwa katika malipo yake.
5. WAKALA KULIPWA PESA ISIYOKUWA KATIKA MAKUBALIANO.
Ikiwa wakala amefanya jambo jema na la faida kwa mhusika mkuu basi wakala anastahili malipo ya jambo hilo hata kama malipo hayo hayapo katika makubaliano. Hii ni kwa mujibu wa kifungu cha 174 cha sheria ya mikataba.
6. FIDIA KWA KUJIONDOA KATIKA UWAKALA.
Yeyote kati ya mhusika mkuu au wakala anaweza kujiondoa katika uwakala. Yeyote atakayejiondoa katika uwakala kabla ya muda wa makubaliano kuisha basi atalazimika kumlipa fidia mwingine. Akijiondoa wakala fidia italipwa kwa mhusika mkuu halikadhalika mhusika mkuu akijiondoa fidia italipwa kwa wakala. Taarifa ya muda wa kutosha ni lazima itolewe kabla ya kujiondoa la sivyo aliyejiondoa atalazimika kulipa fidia nyingine zaidi kwa madhara yaliyotokana na kujiondoa kwake ghafla.
MWANDISHI WA MAKALA HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA SERIKALI LA HABARI LEO KILA JUMANNE , GAZETI JAMHURI KILA JUMANNE NA GAZETI NIPASHE KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE 0784482959.
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE 0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment