NA BASHIR YAKUB -
Makosa ya jinai
ni makosa yote
yaliyoorodheshwa katika sura
ya 16 ya kanuni za
adhabu pamoja na
yale yaliyo katika sheria nyingine
kama ile ya
uhujumu uchumi. Pamoja
na kuwapo sheria nyingine ambazo huorodhesha makosa
ya jinai bado
Kanuni za adhabu
inabaki kuwa sheria
kuu inayoorodhesha makosa
ya jinai. Kwa
ujumla katika sheria tunayo makosa makuu
ya aina mbili.
Kwanza ni
hayo ya jinai
na pili ni
ya madai. Kwa kusema makosa
ya jinai na madai unajikuta
umeongelea karibia makosa
yote unayoyajua na usiyoyajua. Kila
kosa unalolijua kichwani
mwako lipo katika
moja ya makundi haya.
Kwa mifano tu makosa ya jinai ni kama kupiga, kutukana, kuendesha kwa uzembe( ulevi, kuongea na simu, mwendo kasi,kuzidisha abiria n.k), kudhalilisha, kuiba, kubaka, kuua, utapeli, kughushi, ufisadi, rushwa, matumizi mabaya ya ofisi ya umma, kulawiti, kumiliki madanguro, ukahaba, dawa za kulevya( kutumia au kuzimiliki), kuzuia mahakama au mamlaka za kisheria kutekeleza wajibu, kuharibu mali ya mtu, kuvamia eneo la mtu kwa nia ovu, manyanyaso ya jinsia na mengine mengi.
1.KUJIKUTA UMETENDA
JINAI.
Wakati mwingine suala kutenda jinai
halitokei kwa makusudi. Unaianza
siku vyema lakini bahati
mbaya katika muamala usiotarajia unajikuta umeingia katika
jinai. Kutenda jinai
kwaweza kusababishwa na
mambo matatu kwanza
nia/makusudi ya kutenda
jinai, pili kutenda jinai kwa
bahati mbaya au kushurutishwa , tatu kutenda
jinai kwa uzembe. Kutokana na
haya ni vema basi
kujua jinai imetokea
vipi na vipi
waweza kujinasua nayo.
2. MAMBO
MATATU YATAKAYOKUONDOLEA JINAI
MAHAKAMANI.
( a ) Kudai haki
kwa nia njema( bonafide claim of right). Kifungu cha 9
cha Kanuni ya
adhabu sura ya 16
kinasema kuwa mtu
hatawajibika na kosa
la jinai kwa kosa linalohusiana
na mali iwapo
kitendo kilichofanyika au
kufanywa na huyo
mtu kilifanywa kwa nia
njema ya kudai
haki na si kwa
nia ya kuiba.
Mfano wa hili ni kuwa imetokea kuna mtu unamdai na hataki kukulipa, ukamzuia na kumnyaganya mali yake iwe gari, baiskeli , redio au chochote, basi mtu huyo hawezi kwenda kufungua kesi ya jinai ya kumvamia, au kumuibia. Kifungu hiki kitakulinda kwakuwa umefanya hivyo kwa nia njema ya deni lako kwake. Kwahiyo katika hili hautakuwa na jinai.
Mfano wa hili ni kuwa imetokea kuna mtu unamdai na hataki kukulipa, ukamzuia na kumnyaganya mali yake iwe gari, baiskeli , redio au chochote, basi mtu huyo hawezi kwenda kufungua kesi ya jinai ya kumvamia, au kumuibia. Kifungu hiki kitakulinda kwakuwa umefanya hivyo kwa nia njema ya deni lako kwake. Kwahiyo katika hili hautakuwa na jinai.
( b ) Kujilinda,kulinda mtu
au mali( defence of
person or property). Kifungu
cha 18 cha
kanuni za adhabu
kinasema kuwa mtu
hawezi kuwajibika kijinai
kwa kitendo alichokifanya
wakati wa kutimiza
haki yake ya kujitetea/kujilinda,
kumtetea mwingine, kutetea mali
yake au ya
mwingine. Mfano wa hili
ni kuwa imetokea
mtu au watu
wanataka kukufanyia fujo
kwa namna yoyote
ile. Katika kujitetea
wasikudhulu ukamuumiza au
hata kumuua mmoja.
Kwa mazingira haya hautawajibika kwa
jinai. Au umemkuta
mtu akiharibu mali yako
au ya mtu
mwingine.
Katika kumzuia asifanye
hivyo ukamuumiza mtu
mwingine, ukaharibu mali nyingine
au ukajikuta umetenda
jinai nyingine yoyote. Basi hautawajibika na
jinai hiyo kwakuwa
ulikuwa ukilinda mali
au ukijitetea.
Muhimu ni kuwa usitumie nguvu zaidi kujitetea au kujilinda kuliko nguvu inayoshambulia. Kiwango cha kujilinda na madhara yaliyotokana na hilo yasizidi kiwango cha shambulio na mazingira yake kwa ujumla.
( c ) Dhania isivyo
kweli( mistake of fact). Kifungu cha 11
( 1 ) kinasema kuwa mtu
ambaye anatenda kitendo
kwa nia njema
lakini kwa kukosea
kwa kuamini kuwepo
kwa hali fulani ambayo
kumbe haipo hatawajibika
kwa kosa la
jinai kwa kitendo
hicho. Mfano wa hili
ni pale ambapo
unaweza ukampiga mtu katika mazingira
ya kujihami usidhurike
ukidhani ni mwizi
lakini baadae unagundua
kuwa hakuwa mwizi.
Au unamdhuru mtu
kwa kudhani ni mgoni wako
kumbe ni mtu
mwema aliamua kumsaidia
mke wako baada
ya kuzidiwa ghafla. Ni
mazingira kama hayo
ambapo utaondolewa katika
jinai. Makala nyingine tutaangalia
matendo mengine yanayoweza
kukuondolea jinai.
NYUMBA HIZI ZINAUZWA.
A. 1. Ina vyumba 3.
2. Uwanja unabaki.
3. Ipo kigamboni, kibugumo.
4. Ni karibu na mji mwema.
5. Mita 300 kutoka barabara kuu ya lami .
6. Bei milioni 30 inapungua kidogo.
0784482959.
B.
NYUMBA MBEZI JOGOO.
1.Ipo Mbezi Jogoo karibu na kiwanda cha COTEX
2. Ina vyumba 3 , bafu 2.
3. Iko kwenye fensi ya kuingia magari 3.
4. Bei milioni 120 inapungua.
0784482959
0 comments:
Post a Comment