NA BASHIR YAKUB -
1.JE KITU
GANI KIFANYKE ASKARI
ANAPOKUNYIMA DHAMANA.
Kwanza ieleweke kuwa
dhamana ni haki
yako. Haki ni jambo
la lazima. Haki
ya dhamana inaruhusiwa
kunyimwa katika makosa
machache sana kwa mfano
uhaini, wizi wa silaha,
mauaji n.k. Makosa mengine
madogo madogo hasa haya ya kila
siku ya kutukana,
kudhalilisha, kupigana, ajali
ndogo, wizi usio wa
silaha, na mengine dhamana
ni lazima. Hata
hivyo makosa ambayo hayaruhusiuwi
kwa dhamana ni lazima askari
anapokunyima dhamana aandike
sababu za kukunyima
dhamana.
Na hapohapo yatakiwa
ahakikishe anakufikisha mahakamani
haraka sana iwezekanavyo
hasa ndani ya
saa 24 ili
mahakama ikatizame shauri
lako na haki
unazostahili. Ni makosa makubwa
askari kumnyima raia
dhamana pale anapostahili
na ni makosa
makubwa askari kutomfikisha
mtuhumiwa mahakamani haraka
bila sababu za
msingi. Unayo haki ya kumtaka
askari akufikishe mbele
ya hakimu/jaji haraka
ili ukaombe dhamana
huko na haki zako
nyingine. Katika hili hautaomba ila utamtaka askari kufanya hivyo.
2. JE DHAMANA
NI LAZIMA UWEKE(DEPOSIT) YA KIASI CHA
FEDHA.
Hapana dhamana si
lazima uache pesa. Unaweza
ukapewa dhamana kwa
ahadi ya maandishi
tu. Ahadi ya
maandishi ni masharti
ambayo utayasaini na
kuahidi kuyatekeleza utapokuwa
umeachiwa kwa dhamana.
Moja ya masharti
hayo ni kuahidi
kufika tena kituo
cha polisi au
mahakamani katika muda
utakaopangwa. Dhamana ya kuweka
kiasi cha fedha
huwa inaamriwa iwapo kuna
makosa makubwa yaliyotendeka. Hata
hivyo fedha hizo
hutakiwa kurudishwa ama
baada ya upelelezi
kukamilika na kuonekana
mtuhumiwa hana kosa au
baada ya kuwa
huru kutokana na
amri ya mahakama.
3 JE INARUHUSIWA
KUMKAMATA MWINGINE BAADA YA
KUMKOSA MTUHUMIWA HALISI.
Ni kosa kubwa
askari kumkamata mtu
mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa.
Mara kadhaa hutokea askari
kuondoka na ndugu , mtoto
au mke wa mtuhumiwa baada
ya kumkosa mtuhumiwa
nyumbani. Hii hairuhusiwi
kabisa. Sheria iko wazi
kuwa aliyetenda kosa
ndiye anayewajibika kwakosa. Kama
hayupo na hawezi kupatikana hilo
haliwahusu ndugu, watoto, mke
au mme wa
mtuhumiwa. Kosa ni kwa aliyetenda kosa basi
na si vinginevyo.
4. KUWEZESHWA KUWATAARIFU
NDUGU UNAPOKAMATWA.
Inapotokea
umekamatwa bila ndugu zako
kuwa na taarifa
na ukawa unashikiliwa
kituo cha polisi
basi unayo haki
ya kuwezeshwa na askari waliokukamata
kuwataarifu ndugu, jamaa
na mwanasheria iwapo
unaye ili waweze
kufika kituoni kwa
hatua . Kama huna mawasiliano
ya simu ni
wajibu wa askari
waliokushikilia kukuwezesha kupata
mawasiliano hayo ili
uwasiliane na ndugu
hao.
5. JE INARUHUSIWA
KUKAMATWA BILA KUAMBIWA
SABABU.
Hapana hairuhusiwi. Unapokamatwa ni
lazima kuambiwa sababu
za kukamatwa huko. Ikiwa
umekamatwa katika mazingira
ambayo sio ya vurugu
basi inatakiwa kabla
hujakamatwa askari ajitambulishe
na akwambie kuwa
anatakiwa kukukamata kwasababu
hii na hii. Ikiwa
katika mazingira ya vurugu
kwa mfano ulikuwa
unagombana, kwenye
maandamano haramu , mapambano
ya askari na
wafanya fujo basi
sababu ya kukamatwa
utaambiwa baada ya
kuwa umekamatwa na
sio kabla.
6. JE UFANYE
NINI IWAPO UMETOA LALAMIKO NA
ASKARI WAMELIPUUZA.
Wapo baadhi ya watu
wametoa malalamiko ya msingi kuhusu
kuonewa au kutendewa
jinai lakini askari
polisi wamekataa kusajili
malalamiko hayo wala
kufungua kesi. Hii inaweza
kuwa imesababishwa na
uzembe au rushwa
aliyotoa mtenda kosa
ili asifunguliwe mashitaka. Ikiwa litakutokea
hilo basi waweza
kutoa taarifa kwa
askari wa cheo
cha juu zaidi
ya yule uliyeripoti
kwake na hasa
mkuu wa kituo. Ikiwa
na huko hakuna
msaada basi waweza
kutoa taarifa kwa
hakimu wa mahakama
iliyo karibu ambaye atatoa
amri ya kusajiliwa
shitaka hilo.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment