NA BASHIR YAKUB -
Hati kwa maana
ya hapa ni
hati za nyumba
na viwanja, kwa
ufupi ni hati
za ardhi. Kwakuwa hati ni karatasi
sawa na karatasi
nyingine basi huweza
kuharibka au kuchakaa.
Huweza kuchakaa kwasababu
mbalimbali za kibinadamu Inaweza kunyeshewa na
mvua au kumwagikiwa
na maji kwa
namna yoyote ile,
inaweza kuungua moto
na wakati mwingine
inaweza kuharibika kutokana
na majanga ya ajali za barabarani
n.k. Muhimu ni
kujua tu kuwa
hati huharibika na
ziko sababu nyingi
za msingi ambazo
hulipelekea hilo.
1.SHERIA YA
USAJILI WA HATI.
Ofisi ya msajili wa
hati hutekeleza shughuli
zake chini ya sheria
ya
Usajili wa ardhi
sura ya 334, ( The land registration
Act Cap 334). Ni katika
sheria hii ambamo
habari zote kuhusu
usajili wa hati
hutolewa. Sheria hii hueleza
namna na nyaraka
mbalimbali zinazohitajika katika
kusajili hati. Sheria
hii ndio mwongozo wa
jumla katika masuala
mazima ya hati.
2. FAIDA
UNAZOWEZA KUPATA KUPITIA
OFISI YA USAJILI
WA HATI NA
NYARAKA.
Ofisi ya usajili
wa hati haishughuliki
na usajili wa
hati pekee bali pia
kupitia ofisi hii
nyaraka mbalimbali zinazohusu
masuala ya ardhi
nazo husajiliwa. Unaweza kusajili
maombi ya zuio kwa kuzuia hati
kubadilishwa. Hii hutokea
iwapo una wasiwasi
kuwa kuna mtu
anataka kuuza eneo
lako au pengine mmoja
wa wanafamilia anataka
kuuza bila ridhaa
ya mwingine/wengine.
Pili kupitia ofisi
hizi unaweza kusajili jina jipya. Kwa
wale wanaobadilisha majina
na kupata majina
mapya basi majina
hayo husajiliwa ofisi hizi. Jina
jipya haliwezi kuanza kutambulika
rasmi bila kusajiliwa
katika ofisi hizi.Majina
ni haya ya John
kuitwa Rashid n.k
Tatu kwa wale wenye
taasisi za ndogo za
kutoa mikopo hata
wale wa VICOBA basi
huweza kusajili mikopo
kupitia ofisi hizi. Nasema
wenye taasisi ndogo
kwakuwa wale wenye
taasisi kubwa wanalijua
hili. Mkopo ili
uwe salama zaidi
huwa unasajiliwa, na hivyo
ofisi zinazohusika na
kusajili mikopo ni
hizi. Mkopo husajiliwa chini
ya sheria ya
mikopo ( mortgage financing
special provision) Act no.
18/2008)
Nne ofisi hizi
hutunza kumbukumbu za masuala yote ya
ardhi na hivyo
kwa mwenye kutaka
rejea ya kumbukumbu huweza
kufika ofisi hizi
na kupata rejea
hiyo. Ni vyema
ukitaka kununua ardhi kupata
rejea ya ardhi unayotaka
kununua kupitia ofisi hizi.
Hatua hii huepusha
mgogoro.
Kwa kutaja ni
machache lakini yapo
mengi ambayo unaweza
kupata kupitia ofisi
za usajili wa
hati na nyaraka.
3. NINNI UFANYE
IWAPO HATI IMEHARIBIKA/KUCHAKAA.
Hati inapoharibika katika
mazingira niliyoeleza hapo juu
basi unayo hiari ya
kufuatilia na kupata
hati nyingine. Mamlaka
za ardhi zilizokuwa
zimetoa ile hati ya mwanzo iliyoharibika ndizo
hizohizo zitakazotoa hati
nyingine mpya. Ili usipate
usumbufu katika kukamilisha
muamala huu ni
vema ukandaa nyaraka
zifuatazo kwa ajili
ya kazi hiyo.
( a ) Andaa picha
nne kwa maana
ya pasipoti size. Picha hizo
ziwe za mtu yuleyule
aliyekuwa kwenye ile
hati iliyoharibika.
( b ) Ikiwa hati
imeharibika pamoja na
nyaraka nyingine ulizokuwa
umetumia awali kuombea hiyo
hati basi ni
vema nyaraka hizo
nazo ukaziambatanisha na
ukaenda nazo katika
mamlaka ya ardhi. Nyaraka hizi ni
zile ambazo huitwa
fomu za maombi.
( c ) Hati
iliyoharibika ni lazima
nayo uiambatanishe. Haijalishi
imeharibika kiasi gani
muhimu ni kuwa
unapoenda kuomba hiyo
nyingine basi ambatanisha
na hiyo iliyoharibika.
( d ) Ni
lazima uwe na
risiti za malipo
ya kodi ya ardhi. Hata
kama wakati hati
inaharibika ulikuwa haujalipia
kodi ya ardhi
basi ni bora
kabla ya kuanza
kufuatilia hati mpya
ukahakikisha umelipa kodi
ya ardhi na hudaiwi.
Mchakato hauwezi kufanyika
iwapo unadaiwa kodi
ya ardhi.
( e ) Pia ipo ada maalum ya
usajili mpya ambayo
utatakiwa kulipia. Ada hizi
hubadilikabadilika na hivyo
si vema makala kutaja
kiwango .Hata hivyo malipo
ya ada ni
hatua ya mwisho
kabisa unapokuwa umekamilisha
maandalizi ya hapo
juu. Ukiwa kwa msajili
utaelezwa ni kiasi
gani utatakiwa kulipia
ambapo risiti ya serikali hutolewa.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment