NA BASHIR YAKUB -
Hati miliki ni mali inayohamishika na
hivyo inaweza kupotea. Kupotea
kwa hati miliki kunaweza
kuwa katika mazingira
mengi. Inaweza kupotea
katika mazingira ya kuibiwa,
kufichwa au kutupwa
kwa makusudi kwa malengo mabaya
na mazingira mengine
yoyote yanayofanana na matukio
hayo. Lakini mara
kwa mara kupotea
kwa hati huhusishwa
na mbinu chafu
za kubadilisha umiliki
pasipo uhalali au
kutumika katika shughuli
za kujipatia mikopo pasi
na ridhaa ya mwenyewe. Makala yataeleza
hatua za haraka za kuchukua iwapo umetokewa
na jambo kama hilo.
1.HATUA ZA
KUCHUKUA HATI INAPOPOTEA.
( a ) KUTOA TAARIFA
POLISI HARAKA
Hii ni hatua
muhimu sana na
ya kwanza kabisa
pale tu hati inapopotea.
Polisi haipo kwa
ajili tu ya kushughulikia kesi
za wizi na
magomvi bali
pia kisheria wamepewa
mamlaka ya kuandikisha
upotevu wa mali. Kituo
cha polisi ambacho
kinapaswa kutumika ni
kile ambacho nyumba/kiwanja husika
kinapatikana. Unapotoa taarifa
polisi hati iliyopotea
huandikishwa na utapewa
namba maalum ya
kupotea. Taarifa ya kupotea huitwa
“lost report”.
Umuhimu wa taarifa
hii ni kuwa ikiwa
hati ile imeibiwa
au imechukuliwa kwa
malengo ambayo si
halali basi itakapotumika visivyo
wewe utakuwa umejitoa
katika uhalifu ule na hutowajibika
au kutambua matumizi
yale yasiyo halali.
Usipotoa
taarifa hii ni
vigumu kujitoa au kutotambua
matumizi iliyotumika hati
yako hata kama
yalikuwa ni ya
kihalifu. Kwahiyo hii ni hatua ya
kwanza, ya muhimu na ya
haraka kabla ya
jambo jingine.
( b ) Ikiwa tayari umetoa
taarifa polisi na
una wasiwasi kuwa
kupotea kwa hati hiyo ni
mpango ambao pengine unalenga matumizi
yasiyo halali basi
unaweza kuweka zuio. Zuio
huwekwa mamlaka za
ardhi zilizokuwa zimetoa
hati . Zuio
huitwa “Caveat”. Ni hatua
ambapo unaandaa maombi
maalum na kuyapeleka
mamlaka za ardhi
kuomba kuzuia kufanyika
kwa aina yoyote
ya mabadiliko katika
umiliki au kuzuia
matumizi yoyote ya kukopea
hati hiyo.
Maombi ya zuio yataambatana na picha ndogo mbili , risiti za malipo
ya ushuru, kodi na
tozo za ardhi.
Lakini kubwa ni
kuwa ni lazima
katika maombi hayo ueleze
sababu ya kwanini unaweka zuio. Katika
hilo sababu itakuwa ni kupotea
kwa hati katika
mazingira yasiyoeleweka. Ili kulithibitisha hilo
kuambatanisha taarifa ya
polisi ya kupotea ( lost report) ni
lazima. Maombi haya
hulipiwa ada maalum.
2. IKIWA
HATI IMEPOTEA NA
UNAHITAJI KUPATA NYINGINE HATUA NI
HIZI.
( a ) Andaa maombi
maalum ya kuomba
kupatiwa hati. Maombi
hayo hufanana na yale
ambayo ulikuwa umeombea
hati ya awali
iliyopotea. Tofauti hapa ni
kuwa katika maombi
mapya utaeleza kuwa
unaomba hati nyingine
baada ya ile ya awali
kupotea.
( b ) Andaa picha
ndogo mbili yaani
passport size ambazo zitatumika
kukaa kwenye nyaraka
mpya za maombi.
( c ) Ripoti ya
polisi ya kupotea (lost
report) ni taarifa
muhimu ambayo ni
lazima iwe imeambatanishwa katika
maombi mpya. Hii itaeleza
mazingira yote ya
kupotea kwa hati na
itakuwa ni taarifa
maalum kuwa hati
hiyo haipo tena.
( d ) Kiapo
cha mmiliki kikieleza
na kuthibitisha kupotea
kwa hati huwa
kinahitajika. Hata hivyo
si wakati wote kiapo
hiki huhitajika. Kwa maana hiyo
kiapo utajiandaa nacho
tu kama dharula ambapo ukitakiwa
kukiwasilisha utafanya hivyo
na kisipohitajika basi haitakuwa na
haja.
( d ) Lazima
uwe na nyaraka
nyingine zinazohusu umiliki
kwa mfano mkataba
wa kununulia, fomu namba
29, 30, 35 na nyaraka
nyingine yoyote ambayo
inaonesha kuwa wewe
ndio ulikuwa unahusika
na umiliki wa
eneo hilo.
( d ) Mwisho risiti
za malipo ya
kodi, ushuru na
tozo za ardhi
ziambatanishwe. Hizi pia pamoja na
mambo mengine husaidia
kuonesha kuwa ulikuwa
mmiliki wa hati
iliyopotea.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment