NA BASHIR YAKUB -
Niliwahi kueleza namna ya kuanzisha
kampuni pamoja na
usajili wa jina
la biashara. Katika makala
hayo pia nilieleza
tofauti kati ya
kusajili kampuni na
kusajili jina la
biashara. Hii ilikwenda
sambamba na maelezo ya tofauti za
kiuchumi ya vyote
viwili. Ifahamike kuwa
hizi zote ni
njia za kisasa
za kujitafutia kipato.
Makala ya leo
yanaeleza namna ya
kisheria ya kuanzisha
SACCOS.
Tutaona utaratibu mzima
ambao unaweza kupitia
katika kulifanikisha hili.
Muhimu ni kujua
kuwa SACCOS nayo
ni njia kati
ya njia za
kisasa za kujipatia
na kujiongezea kipato. Aidha utaratibu mzima
wa kuanzisha na kuendesha
SACCOS unaongozwa
na Sheria namba
6 ya 2013
ya vyama vya ushirika
ambayo ndiyo msingi
wa makala haya.
1.SACCOS NI NINI ?
SACCOS ni kifupi
cha neno la
kiingereza lijukanalo kama
Saving And Credit CO-operative
Society. Kwa Kiswahili
kizuri ni chama
cha ushirika cha
akiba na mikopo. Kwa
faida tu ni
kuwa, kwa mara
ya kwanza SACCOS zilianzishwa
Ujerumani na mtu
aitwaye Fredrick Taylor.
Sura ya SACCOS
aliyoanzisha Taylor imekuwa
ikibadilika kadri shughuli
za kijamii na
kiuchumi zinavyokua mpaka
kufikia aina ya
SACCOS zilizopo sasa.
2. SACCOS KIUCHUMI.
Saccos ni asasi
ya kifedha. Ni muungano
wa watu ambao
lengo lao ni
kukusanya fedha na
kukopeshana au kufanya
biashara moja kwa
moja na kugawana
faida. Taratibu za kukopeshana
na kufanya biashara
katika Saccos hufanywa
na watu wenye
msimamo au fungamano
linalofanana. Hii ina maana wanaweza kuwa
watu wanaofanya kazi ya aina
moja kwa
mfano walimu, wafanyabiashara,
wafanyakazi katika ofisi fulani,
vijana wanaoishi eneo
moja mtaani, wanawake walio
katika eneo moja, waumini
wanaosali katika msikiti au
kanisa moja, wakulima,wavuvi,
wafugaji, wanakijiji na watu wote wa
aina hiyo. Watu
walio katika mafungamano
ya aina hiyo ndio
wanaweza kuunda Saccos.
3. LENGO
KUU LA SACCOS.
Lengo kuu la
Saccos ni kuwa,
ni ushirika ambao
lengo lake ni kuondoa umasikini
na kuinua uchumi wa
wanachama na jamii
kwa ujumla. Hii
ndio sababu kubwa
ya kuanzisha Saccos.
Ni kukuza kipato
kwa manufaa ya
kiuchumi .Ni biashara ya
kuongeza kipato kama
zilivyo biashara nyingine
za uanzishaji wa makampuni
n.k.
4. MAMBO
YA KUZINGATIA KABLA YA
KUANZISHA SACCOS.
Kwanza kabisa ni
uwepo wa hiari
ya kila mwanachama. Ni kosa
kumshurutisha mtu kuingia
katika Saccos. Ni lazima
kila anayeingia afanye
hivyo kwa hiari
yake. Pili ni
muhimu wanaoanzisha Saccos
wakawa na matatizo
ya aina moja.
Kama tatizo ni
ajira na Saccos
inaundwa ili kukabiliana
na hilo basi
yapasa hilo ndio
liwe tatizo la
wanachama wote n.k. Kwa ufupi
wanachama wawe ni
watu wanaoshiriki (share) tatizo.
5. TARATIBU
RASMI ZA KUANZISHA
SACCOS.
( a ) Kwanza
kabisa hakikisha hampungui
watu watano. Yaani muwe
watu watano na
kuendelea. Hii ni kwa
mujibu wa kifungu
cha 38(1) cha sheria ya
vyama vya ushirika. Hata
hivyo idadi hii ni
kwa waanzishaji wa
awali. Hii ni kwakuwa
idadi hasa inayotakiwa
ni kuanzia watu
ishirini. Msajili wa vyama
vya ushirika atawapa
maelekezo ya idadi
kwa namna anavyoona
kikundi chenu.
( b ) Baada ya
idadi hiyo kutimia
mtamfuata msajili wa vyama vya
ushirika ambaye hupatikana
katika kila makao
makuu ya wilaya mliyopo. Nenda
makao makuu ya wilaya
na uliza hapo
utampata. Baada ya kusikiliza
maelezo yenu msajili ataandaa mkutao
ambao huitwa mkutano mkuu
wa uanzishaji ambao
msajili mwenyewe ndio
atakuwa mwenyekiti wake. Katika
mkutano huo itateuliwa kamati ya
muda ya uanzishaji
ambayo itakuwa na
wajumbe 5 – 9 akiwemo katibu,
mwekahazina, mwenyekiti na wajumbe
wengine.
( c ) Baada ya
kamati ya uanzishaji
kuundwa itakuwa na kazi
ya kushirikiana na
afisa ushirika kuandaa
katiba za chama, sera,miongozo, miradi ya
kiuchumi, taratibu za viingilio
na taratibu zote
za uanzishaji na uendeshaji.
( d ) Baada ya
kazi hiyo kukamilika
basi maombi rasmi
ya kuomba kusajiliwa
yatawasilishwa kwa huyo afisa
ushirika wa wilaya
yakiambatana na nakala
nne za sera
za chama, kidadisi uchumi, makadirio ya
mapato na matumizi, mikhutasari ya mikutano miwili, na
ada kama itakavyoelekezwa na afisa ushirika.
Tutaeleza katika makala nyingine
umuhimu wa SACCOS,
tofauti za kiuchumi
kati ya SACCOS
na kampuni na kipi
bora kati ya kuanzisha
SACCOS na kampuni.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA
NA MSHAURI WA
SHERIA KUPITIA GAZETI
LA SERIKALI LA
HABARI LEO KILA
JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA
GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment