NA BASHIR YAKUB -
Kawaida wanandoa wengi
wanapoingia katika migogoro
moja ya jambo
wanalokimbilia kama jawabu
la mgogoro ni talaka. Kwa
misingi ya ndoa
za kiislamu talaka
huruhusiwa tofauti na misingi
ya ndoa za kikiristo ambazo talaka
huwa haziruhusiwi. Hata
hivyo hata kama
ndoa ni ya
kikristo ambayo hairuhusu talaka linapokuja suala
la mahakama basi
hata ndoa hizo
nazo hutolewa talaka. Ieleweke kuwa kwa
mujibu wa Sheria Ya Ndoa
ya 1971 suluhu ya
kumaliza utata katika
ndoa si talaka
tu. Na hii ni kutokana na umuhimu
wa ndoa. Katika
hili sheria ya ndoa imetoa chagua
jingine ambalo mtu anaweza kulitumia
kama mbadala wa
talaka. Hili linahusu kutengana
kama tutakavyoona.
1.KUTENGANA KISHERIA.
Kutengana kwa mujibu
wa sheria ni
hatua ambapo watu wawili
mwanamke na mwanaume walio
katika ndoa halali huamua kutoshirikiana katika
mambo kadhaa ya kindoa huku
ndoa ikihesabika kuwa haijavunjika. Katika hili kinachositishwa ni baadhi ya haki
na wajibu wa
kindoa. Lakini kusitishwa
kwa wajibu na haki
hizo
hakuhesabiki kuwa kumevunja ndoa.
2. AINA
ZA KUTENGANA KISHERIA.
Kisheria zipo njia
mbili ambazo wanandoa
wanaweza kutumia ili kutengana. Kwanza
ni kuwa wanandoa wanaweza kutengana
wenyewe kwa hiari
yao . Kutengana kwa
hiari ni kuwa
wanakubaliana kutengana kwa
muda fulani kutokana na
kutoelewana kwasababu mbalimbali
za kifamilia.
Pili wanaweza
kutengana kwa kutenganishwa
na mahakama kwa mujibu
wa kifungu cha 99 cha sheria
ya ndoa 1971. Hii
ni baada ya mmoja
wa wanandoa kuiomba
mahakama iwatenganishe kwa
kipindi fulani na
mahakama kuridhika kuwa
ipo haja hiyo. Mara
nyingi kutengana kwa njia ya
mahakama hutokea baada
ya hatua za
kutengana kwa hiari
kushindikana. Mara kadhaa
hutokea ambapo mmoja wa ndoa
huwa amekerwa na baadhi
ya tabia na
hivyo kumuomba mwenzake
watengane ambapo mwenzake
hukataa. Inapotokea hivyo
ndipo mwanandoa anapolazimika
kukimbilia mahakamani kuomba
kutengana.
3. TOFAUTI YA
KUTENGANA NA TALAKA.
Talaka ni hatua
ambapo ndoa hutangazwa
kuwa imevunjika kabisa
na kila mmoja hutakiwa kuendelea na maisha
yake. Talaka huambatana na haki ikiwemo
ile ya mgawanyo
wa mali. Wakati
kutengana ni hatua
ya kuchana kwa
muda na kurudiana
baadae. Kutengana hakuambatani na haki ya
kugawana mali za
machumo ya wanandoa.
4. UMUHIMU
WA KUTENGANA BILA TALAKA.
Sheria imeelekeza tendo
hili la kutengana
kwa kuzingatia maslahi
mapana ya wanandoa,
familia na jamii
kwa ujumla. Lengo kuu
la hatua ya
kutengana ni kutoa
nafasi kwa walengwa
wanandoa kujirekebisha .
Inaaminika kuwa katika
kipindi ambacho wanandoa
hutengana huwa kuna
mwanya mkubwa ambao
hupelekea kurekebisha baadhi
ya tabia ambazo zilikuwa
kikwazo. Kutengana ni nafasi ya mtu
kujirudi.
5. MATUNZO
YA MWANAMKE NA
WATOTO KIPINDI CHA
KUTENGANA.
Kwa upande wa
mwanaume ni lazima
kwake kuendelea kutoa
matunzo ya mwanamke pamoja na ya watoto kama wapo. Kisheria mwanaume
ndiye huwajibika kutoa matumizi ya
watoto pamoja na
kumtunza mke wake. Katika kipindi
cha kutengana haki
na wajibu huu
huendelea mpaka kipindi cha
kutengana kitakapoisha. Hata hivyo
yapo mazingira ambapo
mwanamke anaweza kutakiwa
kutoa matunzo kwa
mwanaume kama itakavyokubaliwa
katika masharti ya
kutengana.
6. MUDA
WA KUTENGANA.
Kawaida (practice) muda
wa kutengana unaotakiwa
inabidi iwe miaka
miwili na ikizidi
isizidi mitatu. Ikiwa muda
huo utapita bila
muafaka kwa wahusika basi
hatua za talaka
zinaweza kufuata.
7. KUAMUA KUSITISHA MUDA WA
KUTENGANA.
Kifungu cha 113 ( 1 ) kinatoa uhuru kwa
wanandoa kutuma maombi
ya pamoja mahakamani
kuomba kusitishwa kwa amri ya
kutengana. Hii ni ikiwa
kutengana kulitokana na
amri ya mahakama. Ikiwa kutengana hukukutokana
na mahakama ila ilikuwa kwa
ridhaa ya wanandoa basi
wahusika kwa hiari
yao wanaweza kuamua kusitisha
bila kuhitaji amri ya mahakama.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
Kufahamu pia biblia inasemaje kuhusu Talaka na Ndoa fuata link hii >>> https://wingulamashahidi.org/2018/07/17/ndoa-na-talaka/