NA BASHIR YAKUB -
Mara kadhaa linapoibuka
suala la kugawana
mali pale ndoa
inapohesabika kushindikana masuala
kadhaa ya msingi
na yanayohitaji uelewa
huwa yanaibuka. Moja ya
suala kati ya masuala ambayo
huibuka ni hili la kutenganisha
na kufafanua hadhi
ya mali za
wanandoa ili mgawanyo uweze kufanyika
kwa haki. Yawezekana mwanandoa
akadhani ana haki
katika mali fulani
lakini kumbe kisheria
hana haki hiyo
ni mtazamo wake ndio
unamsukuma kuamini hivyo. Halikadhalika yawezekana
mwanandoa kudhani hana
haki katika mali fulani
kumbe
anayo haki. Ili kujua
una haki ipi
katika mali ipi
na huna haki
katika mali ipi yahitajika kujua
misingi ya kisheria inayotumika
kugawanya mali za
wanandoa.
1.KUGAWANA MALI
ZA WANANDOA.
Ieleweke kuwa tunapoongelea
wanandoa kugawana mali
tunaongelea talaka. Hakuna kugawana
mali bila talaka. Na
kisheria talaka inapotoka
tu swali linalofuata ni
habari ya mali
na watoto kama
wapo. Mali si
lazima magari na
manyumba lakini pia hata
vyombo vya ndani
vikiwemo vitanda, makabati,
sahani n,k nazo
ni mali kwa
mujibu wa sheria. Navyo
huhitaji mgao.
2. JE KUGAWANA MALI
NI NUSU KWA NUSU ?.
Linapokuja suala la kugawana mali wengi
hudhani mtindo unaotumika kugawa ni
ule wa nusu kwa nusu.
Jambo hili si kweli kwakuwa
sheria ya ndoa 1971 iliyofanyiwa marekebisho
2002 haisemi kuwa
utaratibu wa kugawana
mali ni nusu kwa
nusu. Sheria hii imeweka
msingi mkuu wa
kugawana mali ambao
ndio hutumika katika
mahakama zetu katika
kutoa maagizo ya
kugawa mali za
wanandoa.
Msingi uliowekwa
na sheria ni
msingi wa kiwango
cha mchango wa
mwanandoa katika kupatikana
kwa mali husika. Kiwango
alichochangia mwanandoa katika
kupatikana kwa mali hiyo ndicho
kitakachokadiriwa na kiwango
hicho ndicho atakachopewa. Kwa hiyo
kama ni nyumba
ya vyumba sita
mmoja anaweza kupata chumba
kimoja na mwingine akapata
vitano kutegemea na mchango
wake. Na mchango hapa
sio leta ni lete. Mchango sio
hela tu hata
kazi za nyumbani
anazofanya mama wa
nyumbani ambaye haleti
hela nazo huitwa
mchango ambapo hukadiriwa
na kupata kile
anachostahili.
3. MALI
KABLA YA NDOA
NA BAADA YA
NDOA.
Katika
kutenganisha mali za wanandoa huwa
zinatenganishwa katika makundi
makuu matatu. Kwanza kuna mali ambazo
mtu alikuwa nazo
kabla ya ndoa na
wakati anaingia katika
ndoa ameingia nazo. Kwa
mfano mwanamke ameolewa
akamkuta mwanaume tayari
ana nyumba yake. Pili
kuna mali ambazo
zimepatikama wakati wawili
wakiwa katika ndoa . Kwa
mfano ndoa imefungwa
wawili wakaanza kuishi
pamoja na taratibu wakaanza kujenga
na kukamilisha. Na tatu ni
mali ambazo zimepatikana
katika ndoa lakini zikiwa
hazina uhusiano wowote
wa kindoa kwa mfano kurithi au
kuzawadiwa mali. Tutaona hapa
chini mazingatio ya sheria
ya
kila moja katika
haya.
4. JE MALI
ILIYOPATIKANA KABLA YA NDOA
INAHESABIKA NI YA
FAMILIA.
Mali iliyopatikana kabla ya
ndoa na ikaendelea
kuwepo kipindi cha
ndoa inaendelea kuwa ya
huyo mwenye nayo bila
ushirika wa mwenza
wake. Kama ni nyumba
mwanamke alikuwa nayo
kabla ya kuolewa
au ni mwanaume
alikuwa nayo kabla
ya kuoa basi
inaendelea kuwa ya kwake peke
yake na haihusiki
katika mgao suala
la mgao linapojitokeza.
Hata hivyo inaweza
kuingizwa katika mgao
ikiwa kuna mchango
wowote wa kuiendeleza uliotolewa na
mwenza. Kwa mfano kabla ya
ndoa ilikuwa na vyumba viwili
lakini katika kipindi
cha ndoa imepanuliwa
na kufikia vyumba
vitano, au ilikuwa
haina uzio, au haina
madirisha kabla ya
ndoa lakini baadae
vitu hivi vikawepo. Katika hali
kama hiyo itatakiwa
iingizwe katika mgao
na kutazama kiwango cha mchango wa
kila mmoja katika
uendelezaji huo. Ni
hapo ambapo mchanganuo
utafanyika ili kila mmoja
apate haki kutokana
na kiwango cha
mchango wake.
Ikiwa hakuna
uendelezaji wowote uliofanyika
katika mali yaani
labda nyumba ilivyokuwa kabla ya
ndoa ndivyo hivyohivyo
ilivyoendelea kubaki hata
baada ya ndoa
basi mali hiyo
haitatakiwa kuingizwa katika
mali za mgao
bali itabaki mali
ya mwanandoa mmoja
pekee ambaye ndiye
mmiliki wa tangu awali.
Hali ni hiyo
hiyo hata kwa mali
ambayo imepatikana katika
ndoa lakini ikiwa
haina uhusiano na
kipato cha wanandoa,
kwa mfano mali ya urithi au zawadi. Hii
ina maana ikiwa mali
hii itaendelezwa basi mchango
wa uendelezaji utatathiminiwa na ikiwa haitaendelezwa basi
itabaki mali ya
mrithi au mpewa
zawadi pekee na
haitahusu mgao.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment