NA BASHIR YAKUB -
Mara kadhaa mkopaji
anaposhindwa kulipa mkopo
hukimbilia mahakamani ili
kuona kama anaweza
kupata unafuu hasa linapokuja suala
la wakopeshaji wake
kutaka kuuza nyumba/kiwanja alichoweka
rehani. Ni ukweli
usiopingika kuwa hatua
hii imewasaidia wengi
hasa wale wanaowahi.
Yapo makala tuliwahi
kuandika kuhusu hatua za kuchukua
hasa inapotokea kuwa
nyumba yako inataka
kuuzwa.
Makala yalieleza
namna na hatua za kufuata ili
kuokoa nyumba. Kwenda
mahakamani kuzuia nyumba
isiuzwe baada ya
kushindwa kurejesha kiasi
cha rejesho sio ukorofi
isipokuwa ni kutekeleza lililo
ndani ya sheria hasa pale panapo sababu
za msingi za
kufanya hivyo.
Mahakama
za ardhi za
wilaya na mahakama
kuu hasa ya
ardhi ndizo mahakama
zenye mamlaka katika
kutoa mazuio haya
kutegemeana na thamani ya
nyumba/kiwanja na kiasi cha
deni kilichohusishwa katika
muamala huo. Swali kwetu ni
kama baada ya
kuwa umeenda mahakamani
na kubahatika kupata
zuio la kutouzwa nyumba yako, je
upande wa wakopeshaji
wanaweza kukata rufaa kupinga
amri hiyo na kufanikiwa. Majibu ya
swali hili ndio makala
ya leo.
1.HAKI YA RUFAA.
Kifungu cha 74 cha
sura ya 33 Sheria
mwenendo wa madai kinaeleza rufaa
katika amri mbalimbali
za mahakama. Kifungu
kilieleza wazi kuwa
kutakuwa na rufaa
kutoka mahakama za
wilaya na zile
za hakimu mkazi
ambapo rufaa hizo
zitatakiwa kwenda mahakama
kuu. Kwa wasiojua maana
ya rufaa, hii ni hatua
ya kupeleka malalamiko
mbele zaidi baada
ya kuwa hukuridhishwa
na uamuzi wa
mahakama iliyoamua shauri
lako katika hatua za
awali.
Nje ya hilo kifungu
cha 78 cha sheria
hiyohiyo
kiliruhusu pia kufanyika kwa
marejeo iwapo mtu
hakuridhika na maamuzi
ya amri ya
mahakama. Marejeo ni hatua ya
mahakama kuitisha faili
tena na kupitia
kilekile ilichoamua ili
kujiridhisha na uhalali
wake. Hii hutokea
baada ya upande
wa pili kuomba
hilo kufanyika. Kwahiyo ilikuwa
ikiwezekana kutolewa amri ya
kuzuia nyumba kuuzwa
halafu baadae faili
likaitishwa tena na kurudiwa na kutolewa amri
nyingine ambayo inaweza
kuwa ileile ya kutouzwa au ikabadilishwa
ikawa amri mpya
ya kuuza.
2. SHERIA
YA UKOPAJI FEDHA
NA KUWEKA REHANI.
Mwaka 2008 ilikuja
sheria ambayo iliitwa
kwa jina la sheria
ya ukopaji fedha
na kuweka rehani.
Sheria hii inazungumzia
masuala yote nyeti
yanayohusu kukopeshwa fedha
na kuweka rehani
mali . Ni sheria inayoratibu
masuala yahusuyo kuuzwa
kwa mali zilizowekwa
rehani na kutouzwa kwake. Inazungumzia haki
za mkopaji na
mkopeshaji halikadhalika wajibu
wao wote katika
nafasi zao. Kutokana na ujio
wa sheria hii
masuala kadhaa katika
sheria ya ardhi
ya 1999 sambamba na sheria
ya
mwenendo wa madai sura ya
33 zimelazimika kufanyiwa
marekebisho ili kukidhi
malengo kadhaa .
3. AMRI
YA KUTOUZA NYUMBA
YA MKOPO HAIKATIWI
RUFAA.
Hapo juu tuliona
kuwa awali ilikuwa
ni ruhusa kwa mtu
kukata rufaa hata kwa
amri iliyotolewa kuzuia
nyumba/kiwanja cha mkopo
kuuzwa. Mahakama ya
wilaya ingeweza kutoa
amri kuwa nyumba
fulani isiuzwe hata kama
mkopaji yuko nje
ya makubaliano kwasababu
kadha wa kadha. Hata
hivyo ilikuwa
ni haki ya mkopeshaji ambaye ndiye
hutaka kuuza nyumba
kukata rufaa na kupinga amri
hiyo. Kama amri hiyo
ingetolewa mahakama ya
wilaya au ya hakimu
mkazi basi mkopeshaji angeweza
kukata rufaa kwenda
mahakama kuu. Na
huko ingewezekana kutolewa
uamuzi uleule au
uamuzi mpya ambapo
pengine amri ya
kutouzwa ingebatilishwa na
kuruhusu uuzaji kuendelea.
Kwa sasa kutokana
na sheria hii ya masuala ya
ukopeshaji fedha na rehani kifungu
hiki kimefanyiwa marekebisho
na sasa ni
kuwa amri ya mahakama iwe ya
wilaya
au mahakama kuu
ikishapita na kutoa
zuio la kutouzwa
nyumba ya mkopaji
basi huwezi tena kukata rufaa
kupinga jambo hilo. Amri
hiyo ikishatolewa basi
inakuwa imetolewa. Ni kutokana
na hilo kichwa
cha makala haya kimekuwa , amri ya kutouza
nyumba ya mkopo
haikatiwi rufaa.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment