NA BASHIR YAKUB -
Ni kawaida watu
kukopeshana fedha katika
shughuli za kibinadamu za kila siku hasa
zile za uzalishaji. Ni kutokana
na hili baadhi
ya watu hujikuta
wameingia katika faraka ambazo
hata hivyo zinatatulika
kisheria. Kwa wale ambao
madeni yao hutokana
na taasisi za
fedha kama benki
hawa huwa sio
rahisi kwao kukwepa kutokana na utaratibu makini
wa utoaji wa fedha wa taasisi hizo. Tatizo
kubwa la kutolipana na
kuleteana dharau huhusisha
wadeni binafsi yaani mtu
na mtu. Ni katika
madeni haya ya
watu binafsi ambamo msemo
maarufu wa deni
halifungi husikika. Ni
kawaida kukuta mtu
amekopeshwa na hataki
kurejesha akijiamini kuwa
deni halifungi. Yumkini wapambe nao
husikika wakisema, asikutishe
huyo deni halifungi. Kwa makala
haya tutapata kujua
ikiwa ni kweli
deni linafunga au halifungi.
1.KESI YA
MADAI.
Kesi za madai ni zile
kesi zote ambazo
si za jinai. Kesi
za madai hazihusishi
kudaiana pesa tu
kama wengi wanavyojua. Hata masuala ya
talaka, kudai fidia, mikataba,
madai ya
vitu kama nyumba, magari n.k navyo huingia
katika kesi za
madai. Kwa hiyo tunapojiuliza
swali la ikiwa
deni linafunga au
halifungi tunaongelea hivi vyote.
Hata hivyo tutajielekeza
zaidi katika kudaiana fedha.
2. JE
INARUHUSIWA KUPELEKA KESI
YA MADAI POLISI ?.
Unayo haki ya
kufungua shauri ikiwa kuna mtu unamdai lakini kwa sharti kuwa shauri
lifunguliwe pahala stahiki.
Wapo ambao hupeleka
kesi za namna
hii polisi japo
huko si mahali pa
kesi za namna
hii. Polisi hujitahidi kuzitafutia
ufumbuzi ambapo wakati
mwingine hufanikiwa na
wakati mwingine hushindwa. Ukweli ni
kuwa kisheria polisi
hawana ruhusa ya
kushughulikia kesi za
madai hasa hizi
za kudaiana hela
na hata mali. Ni
basi tu wanaamua
kuzishugulikia lakini si
kazi yao kisheria. Madhara utakayoyapata
utakapomfungulia kesi mdai
wako polisi ni pamoja na kupoteza mda
bila kupata ulichokitaka.
Hii ni kwasababu
mdaiwa atakapokataa kutoa
ushirikiano wowote, polisi hawana
la kumfanya.
Hawawezi kumfunga
kwasababu hairuhusiwi.
Hawawezi kumpeleka mahakamani
kwasababu hawaruhusiwi kupeleka kesi
za madai mahakamani. Kwahiyo mdaiwa uliyempeleka
polisi akiamua kukomaa
hawana la kufanya
utakuwa umepoteza muda
na gharama.
Basi ieleweke
kuwa kesi za
madai kama
haya hutakiwa kufunguliwa mahakamani. Yaweza kufunguliwa mahakama
yoyote kutegemea na
kiwango cha fedha
unachodai. Waweza kufungua mahakama
ya mwanzo, ya wilaya na
hata mahakama kuu. Usipeleke kesi ya
namna hii polisi labda
kama unalenga kumtisha
mdeni na si
kupata haki.
3. JE DENI HALIFUNGI KISHERIA ?
Hapana, deni linafunga. Ikiwa utashitakiwa
kwa kudaiwa fedha
na hukumu ikatolewa
kuwa unatakiwa kulipa
hizo fedha basi
unatakiwa uzilipe. Ikiwa hauna
basi itaangaliwa kama
una mali kama
nyumba, gari au
mali yoyote ambayo inaweza
kukamatwa ili kulipia
deni. Ikiwa hauna nyumba ,
gari au mali
nyingine yoyote inayoweza
kufidia deni basi
itatakiwa ukamatwe ufungwe
kwa ajili ya
deni hilo. Kifungu
cha 44 ( 1 ) cha sheria ya
mwenendo wa mashauri ya
madai kinasema kuwa mdaiwa
anaweza kukamatwa katika
muda na siku
yoyote , na haraka kufikishwa
mahakamani , na kuwa
mahakama inaweza kutoa
amri ya kuwekwa
kizuizini/kufungwa. Kwa hiyo
deni linafunga labda
mdai asiamue kuchukua
hatua.
4. JE
UKIFUNGWA DENI LINAISHA ?.
Hapana ukifungwa deni
haliishi. Kifungu cha 46 ( 2 ) cha
sheria ya mwenendo
wa mashauri ya
madai kinasema kuwa
mdaiwa aliyeondolewa katika
kifungo kwasababu yoyote
ile, iwe kwa kumaliza
muda, ugonjwa au vinginevyo hatahesabika
kuwa ameondolewa katika
deni kutokana na
kuachiwa huko. Hii
ina maana unatumikia
kifungo kikiisha deni
linabaki palepale.
Kifungo hakifuti au
kusimama badala ya
deni isipokuwa ni adhabu
ya ukorofi. Ni
kutokana na mtazamo huo wa sheria
unaolazimisha kutakiwa kulipa deni hata
baada ya kutumikia
kifungo. Ukishindwa mara nyingine tena
kulipa mdai anayo
haki ya kukurudisha
tena mahakamani ambapo unaweza
kufungwa tena. Msimamo wa
sheria ni mpaka
ulipe tu.
5. KULIPIWA
DENI UKIWA JELA.
Muda wowote mdaiwa
akiwa jela anatumikia
adhabu yake ya
deni anaweza kuondolewa
na kufutiwa adhabu
hiyo iwapo kiwango
cha deni analodaiwa
kitalipwa. Mahakama iliyotoa amri ya
kufungwa ndiyo itakayotoa
amri ya kuachiwa baada ya deni kulipwa katika ukamilifu wake.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
Asante Sana Ndugu nashukuru kwa elimu unayotupa kila siku. Mimi ni dalali, madalali wakati mwingine tumekuwa tunadhulumiwa pesa zetu kwa Wale tulioowatafutia wateja wa kununua nyumba ama viwanja vyao, wakidai kwanza hatujasajiliwa ,wakati wanatupa kazi ya kuwatafutia wateja wanaahidi kuwa watatulipa 10% siku biashara ikifanyika wanatupa 2% ama wasitupe kabisa tunaomba elimu kidogo wa Sheria inasemaje kazi njema. .
Nina shukuru nilikuwa sielewi kuhusu kesi ya madai.Maana watu wanadai Deni halifuka kwasababu tulikopeshana kienyeji.
Kwa mtumishi wa serikali anaedaiwa na ameshitakiwa hukumu yake ikoje
Asante