Wednesday 21 October 2015

IJUE NAMNA YA KUKATA RUFAA

Image result for MAHAKA  YA  RUFAA

NA  BASHIR  YAKUB -

Unaposhindwa  kesi  sio  mwisho  wa kusaka  haki. Hii  ni  kwasababu  kushindwa  kesi  kunatokana  na  sababu  nyingi . Si  kweli  kuwa  kwakuwa  umeshindwa  kesi  katika  mahakama  fulani  basi  maana  yake  ni  kuwa  ulikuwa  huna  haki. Yawezekana  kabisa  haki  ilikuwa  yako  isipokuwa  umeshindwa  tu  kutokana  na  sababu  nyingine  za  kiutaratibu na  kimbinu (procedures & technicalities).  Pia  waweza  kuwa  umeshindwa  kutokana  na  uwezo  mdogo  wa  kujieleza  na kushindwa  kugusa  nukta  muhimu  ambazo  kimsingi  ndizo  zilizokuwa zinabeba   shauri  lako. 

Lakini  pia  waweza  kuwa  umeshindwa  kwasababu  ya  hila  na  mbinu  chafu. Na  hii  wakati  mwingine  huwahusisha  hata  waamuzi yaani mahakimu  na  majaji.  Basi  ifahamike  kuwa  ni  sababu  hizi   zilizopelekea  kuwepo  utaratibu  wa  rufaa  ili  yule  anayehisi  kutotendewa  haki  aende mbele  ili  kuona  kama anaweza  kupata  haki  yake  huko.

1.RUFAA  NININI.

Rufaa  ni  hatua  ya  kisheria  ya  kupeleka  malalamiko  katika  hatua  ya  mahakama  ya  juu  zaidi  baada  ya  mmoja  wa  wahusika  katika  kesi  iliyoisha  kutoridhishwa  na  hukumu/maamuzi. Ili  ukate  rufaa  ni  lazime uwe  ulikuwa  mhusika  katika  kesi  iliyoisha  na  uwe  na sababu  za  kwanini  unadhani hukuridhishwa  na  maamuzi.  Sababu  yoyote ya  msingi  inakubalika.

2.     NI  HAKI  YAKO  KUAMUA  KUKATA  RUFAA  AU  KUACHA.

Suala  la  kukata  rufaa  halitegemei hisani  ya  mahakama. Sio  upendeleo  ambao  mtu  anapewa   ili  kuendelea  kusaka  haki. Ni  haki  ya  msingi  na  ya  kisheria  ambayo  hutumiwa  na  yule  ambaye  anahisi kutotendewa  sawa   katika  shauri  la  awali  lililoisha. Pia  ieleweke kuwa  rufaa  tunazoongelea  hapa ni  zile  rufaa  katika  mashauri  ya  madai. Rufaa  katika  mashauri  ya  madai  tunaongelea  mashauri  ya  ardhi,  ndoa,  mikataba, migogoro  ya  biashara  na  mauziano  kwa  ujumla, migogoro  ya  madeni   na  yale  yote  ambayo  sio  jinai.  Kwahiyo  katika  malalamiko  ya  namna  hiyo  ni  uamuzi  wako  ukate rufaa  kwenda  mbele  au  uache  hata  kama  umeshindwa.  Hii  ni  haki  yako  na  katu  haiondolewi  na  yoyote.

3.    HATA  ALIYESHINDA  ANAWEZA  KUKATA  RUFAA.

Hapo  juu  tumesema  rufaa  ni  kwa mtu  ambaye  hakuridhishwa  na  maamuzi   ya  mahakama.  Sio  kwa ajili  ya  aliyeshindwa  bali  ni  kwa  ajili  ya  yule ambaye  hakuridhishwa. Hii  ina  Maana  kuwa  unaweza  ukashinda  lakini  ukawa  hukuridhishwa.  Na  kama  umeshinda  lakini  hukuridhishwa  pia  waweza  kukata  rufaa. Kwa  mfano  ulifungua  kesi  ukiomba  fidia  ya  milioni 50. Hukumu  ikatoka  kuwa  umeshinda  lakini  ikasema  kuwa  utalipwa  milioni  kumi tu. Kwa  mazingira  kama  haya ni  kuwa  umeshinda lakini waweza  kukata  rufaa  kudai  zaidi. Utakata  rufaa  kwakuwa  umeshinda  lakini  hukuridhishwa   na  ushindi. Kinachotakiwa  kueleweka  hapa  ni  kuwa   rufaa  inaweza  kukatwa  hata  yule  aliyeshinda  kesi  na  si  tu  kwa  aliyeshindwa.

4.     NAMNA  YA  KUKATA  RUFAA.

Mara  tu kesi  inapoisha  hakikisha  unafuatilia  na  kupata  nakala  ya  hukumu pamoja  na  tuzo( decree). Fuatilia  kwa  karani wa  hakimu/jaji  aliyesikiliza  shauri  lako na  umwambie  nia  yako  ya  kutaka  nakala  ya  hukumu  na  tuzo  kwa  ajili  ya  kukata  rufaa. Huwezi  kukata  rufaa  bila  nakala  ya  hukumu  kwakuwa   ni  lazima  uipitie  kwa  umakini  na  kuona  ni  wapi  palikuwa  na  tatizo  ili  iwe  ndio  sababu  yako  ya  rufaa.

Ikiwa  hukumu  ilitolewa  na  mahakama  ya  mwanzo  basi  rufaa  itaenda  mahakama  ya  wilaya,  na  ikiwa  ilitolewa  na  mahakama  ya  wilaya  rufaa  itaenda  mahakama  kuu  na  ikiwa  ilitolewa  mahakama  kuu  basi  rufaa  huenda  mahakama  ya   rufaa  ambayo  ni  mahakama  ya  mwisho  kiitifaki. Pia  rufaa  zinazotoka  katika  mahakama  za  hakimu  mkazi kama  ile  ya  kisutu ambazo  baadhi  huziita  mahakama  za  mkoa,   rufaa  zake huenda  mahakama  kuu pia.

Unapokuwa  unaandaa  sababu  za  rufaa  hakikisha  unamuona  mwanasheria  kwa  ajili  ya  kupitia  hukumu  na  kukusaidia  kuandaa  sababu  za  rufaa.  Hii ni kwasababu ipo  namna  ya kisheria ya  kuandaa  sababu  hizi  kwani  haziandaliwi  kama  barua.

Muda  ni  suala  la  msingi  sana  katika  kukata  rufaa. Hakikisha  pale  tu  hukumu  inatolewa  unaandika  barua  mahakamani  ya  kuomba  nakala  ya  hukumu. Hii  itasaidia  hata zile  siku  30  au  45  za  rufaa  zikipita  kabla  hujapatiwa  nakala ya  hukumu  kujitetea  kuwa  ulichelewa kwakuwa  ulikuwa  ukisubiria  nakala  ya  hukumu ambayo  uliiomba  ndani  ya  wakati  stahiki.

MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI  LA  SERIKALI   LA   HABARI   LEO  KILA  JUMANNE  , GAZETI  JAMHURI   KILA  JUMANNE  NA  GAZETI  NIPASHE  KILA  JUMATANO.    0784482959,        0714047241              bashiryakub@ymail.com

                                           TANGAZO   MUHIMU                                                
VIWANJA     NA     NYUMBA          ZINAUZWA.
·        
WANASHERIA   WETU   WATAKUANDALIA   MIKATABA  YOTE  BURE  NA  KUKUSIMAMIA  MPAKA   MANUNUZI    YAKAMILIKE   BURE.
·        
UHALALI   WA  NYARAKA   NA   UMILIKI   UMETHIBITISHWA  NA                  WANASHERIA  WETU.
·        
UTAPEWA  MTU  WA  KUKUSAIDIA  KUFANYA  TRANSFER   KWA HARAKA  BURE.
·        
IKIWA   UTATOKEA   MGOGORO  NDANI   YA  MWAKA  TANGU  TAREHE  YA       MANUNUZI    UTAPEWA   WAKILI   WA   KUSIMAMIA  MGOGORO    BURE
                                                        0784482959.

 KUONA   BOFYA  HAPO  JUU    MWANZO  WA   BLOG.



8 comments:

  • Unknown says:
    12 October 2016 at 23:16

    Nikupongeze kwa kazi nzuri unayoifanya ya kutufumbua macho juu ya haki zetu mbele ya sheria na namna gani tuzitumie.
    Asante sana ninajifunza mengi kupitia makala zako mpaka nahisi nimekua mwanasheria

  • Unknown says:
    12 October 2016 at 23:47

    Nikupongeze kwa kazi nzuri unayoifanya ya kutufumbua macho juu ya haki zetu mbele ya sheria na namna gani tuzitumie.
    Asante sana ninajifunza mengi kupitia makala zako mpaka nahisi nimekua mwanasheria

  • Unknown says:
    13 October 2016 at 05:42

    Kaka nakukubali sn!
    Wanasheria wetu licha ya uchache wao lkn wamekuwa wachoyo wa elimu ya sheria. Mungu akubariki sn kwan unatusaidia sn sisi tulio mambumbu na mara nyingi tunapoteza haki zetu kwa kutozijua sheria. Lkn pia nikuombe uchapishe vitabu vyenye makala km hizi ili ufaulu kuwafikia watanzania wengi,ambao ni dhahiri shayiri wanaihitaji sn elimu hii lkn hawawezi kutumia njia hizi za mitandao. Naitwa Raymond niko Buswelu,Mwanza

  • Unknown says:
    17 April 2018 at 00:13

    Great Job. This is what Literacy mean! Keep it up!

  • Unknown says:
    23 June 2018 at 23:55

    asante kwa elimu dhidi ya rufaa sasa naomba kujua rufaa za uchaguzi muda baada ya uchaguzi pia anae katiwa rufaa atajulishwa ama anatolewa bila hata mahojiano m.b.abdallah mwanza


  • Unknown says:
    26 January 2019 at 23:21

    IPO vema sana. Karibu h/ ya mpimbwe.

  • Unknown says:
    12 March 2019 at 23:56

    unaruhusiwa kukata rufaa mwisho mara ngap

  • Unknown says:
    29 November 2019 at 03:17

    Asante kwa Elimu nzuri na ya maana sana mnayoitoa. Ukweli ghalama ya kupata usaidizi wa kisheria baadhi ya maeneo, ni kubwa mno..,sasa, kuna ndugu yangu aliandika rufaa yeye mwenyewe kwa hakimu mahakama ya wilaya. Lakini imekataliwa mpaka iandikwe kwa kiingerza. Ni kweli? Kutoka mahakama ya mwanzo? Ambako hata kesi iliendeshwa kiswahili?

Post a Comment