NA BASHIR YAKUB -
Kesi/shauri
lolote iwe jinai
au madai kuishinda
kwake mara nyingi
hutegemea mambo makuu
mawili. Kwanza mashahidi ,pili ushahidi. Mashahidi siku
zote ni watu.
Hakuna kitu kinaweza
kuitwa mashahidi halafu
kisiwe binadamu. Hii ni tofauti
na ushahidi. Ushahidi si
lazima wawe binadamu.
Vitu hasa vizibiti(exhibit) ndivyo
huitwa ushahidi. Nyaraka, mali, vifaa,
na kila kitu
ambacho mtu anaweza kukitumia mahakamani kuthibitisha kile
anachokisema huitwa ushahidi. Yumkini
yawezekana wakati huohuo
mmoja ukawa na
vyote yaani ushahidi
pamoja na mashahidi hapohapo.
Hii hutegemea namna mtu alivyojiandaa
katika kuwasilisha kesi
yake.
1.SIFA ZA SHAHIDI.
Si kila mtu
ana sifa za
kuwa shahidi. Shahidi hutakiwa
kuwa mtu mkweli , muaminifu na
muadilifu. Lakini pia
sifa kuu ya
shahidi ni kuwa
na akili timamu.
Mtu asiye na
akili timamu hawezi
kuwa shahidi. Lakini pia
mtu mwenye sifa
ya uongo hasa
huko nyuma kama
aliwahi kutoa ushahidi
wa uongo mahakamani
na ikathibitishwa kuwa
alitoa ushahidi wa
uongo basi naye
hupoteza sifa ya
kuwa shahidi.
Pia sifa nyingine
kuu ya shahidi
ni muhimu awe
ni yule aliyeona,
kuhisi kwa kutumia
moja kati ya
viungo vyake, au
kusikia . Hii ina
maana shahidi hutakiwa kuwa yule anayelijua
tukio kwa kulishuhudia
na si vinginevyo
2. IDADI YA
MASHAHIDI INAYORUHUSIWA.
Hakuna idadi ya mashahidi rasmi
inayoruhusiwa kisheria. Idadi
yoyote ya mashahidi inaruhusiwa.
Suala la msingi
hapa ni kuwa
kila shahidi katika
mashahidi hao unaowaleta
awe na umuhimu
katika kesi. Usilete
watu ambao hawahusiki
na kuisababishia usumbufu
mahakama. Hii ni kwasababu
wingi wa mashahidi hauakisi ushindi
katika kesi. Hata shahidi mmoja
tu kama ni wa muhimu anaweza kukufanya
ushinde kesi na kumshinda mwenye
mashahidi ishirini.
3. JE ALIYEAMBIWA ANAWEZA
KUWA SHAHIDI.
Ushahidi wa kuambiwa
siku zote huwa
haukubaliki mahakamani. Inatakiwa yule aliyekuambia
ndiye aje mahakamani na
aseme hicho alichokiona na
kukusimulia wewe.
Aliyeona,kusikia au kuhisi
jambo ndiye aje
mahakamani na sio
amwambie fulani halafu
huyu fulani eti
ndo awe shahidi. Ni
mazingira machache ambapo
ushahidi wa kuambiwa
unaweza kukubalika, kwa mfano iwapo
aliyekwambia amekufa n.k.
4. KUMLAZIMISHA SHAHIDI
KUFIKA MAHAKAMANI.
Kifungu cha 26
cha sheria ya mwenendo
wa mashauri ya madai kinasema
kuwa mahakama inaweza
kutoa wito(summons) kwa
mtu yeyote ambaye
ni shahidi kufika
mahakamani kutoa ushahidi
wake au kutoa (release) nyaraka yoyote
ambayo iko mikononi mwake. Hapa
kuna mambo mawili,
kwanza yeye mwenyewe
kufika mahakamani kutoa ushahidi. Na
pili kutakiwa kutoa ( release) nyaraka
aliyonayo.
Wakati mwingine huwa
inatokea kuwa nyaraka fulani
ambayo ndio ushahidi
wako unaotegemea iko
mikononi mwa mtu mwingine/taasisi/kampuni nyingine
ambayo una uadui
nayo au huna
uadui lakini unajua
kwasababu moja au
nyingine hawawezi kukupa
hiyo nyaraka ukiiomba. Basi
ndio hapo jambo
hilo utatakiwa kulisema
mahakamani ili utolewe
wito wa kuwataka
hao wahusika kuleta
nyaraka hiyo mahakamani
kwa ajili ya
ushahidi.
5. HATUA KWA KUKATAA
KUTOA USHAHIDI .
Kifungu cha 27 cha
sheria ya mwenendo
wa mashauri ya madai kinasema
kuwa iwapo mtu
ameitwa kutoa ushahidi
au kuwasilisha nyaraka fulani na amekataa kufanya
hivyo basi mahakama
itatoa waraka wa
kukamatwa kwake au kukamata
mali yake na
kuiuza au kumtoza faini. Hivyo ndivyo
ilivyo.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment