NA BASHIR YAKUB -
Kisheria haizuiwi kuweka
rehani nyumba ya
makazi kwa ajili
ya kupata mkopo
kutoka taasisi yoyote
ya fedha. Jambo la msingi sana
ni kuwa watoa
mkopo wajiridhishe na
umiliki wa nyumba
hiyo hasa kwa kuangalia
ikiwa ni
mali ya familia
au hapana ili wachukue hadhari
za kisheria.
Nyumba ya makazi
ni ipi. Nyumba ya
makazi ni ile
nyumba ambayo inatumiwa
na binadamu kuishi
lakini zaidi wanaoishi
mle ndani iwe
ni familia ya mchukua mkopo.
Yawezekana
nyumba ikawa ni ya makazi
kwa watu
wengine lakini ni
ya biashara kwa
mchukua mkopo. Kwa mfano
nyumba za kupanga
ambapo mwenye nayo
anaishi kwingine na nyumba
iko kwingine ikiwa na watu wengine. Nyumba ya
namna hii haitaingia
kwenye nyumba ya
makazi kwa tafsiri
hii. Hata hivyo
haitarajiwi mchukua mkopo
kuhamia kwenye nyumba
ambayo sio ya makazi kwa
makusudi na kuifanya ya
makazi akilenga kuhadaa
ili kupata upendeleo
wa mahakama. Akifanya
hili atakuwa amedanganya
na ni kosa
kama tutakavyoona.
1.MAKOSA YA
KISHERIA KWA MKOPAJI.
( a ) Sheria ya masuala ya
rehani ya 2008
inamtaka mkopaji kutofanya
udanganyifu wa aina
yoyote kwa taasisi inayotarajia kumpa mkopo. Moja ya
udanganyifu ni kama
ilivyoelezwa hapo juu
lakini pia upo
udanganyifu mwingine mwingi
ambao hufanywa na wakopaji. Kwa
mfano kuweka rehani
nyumba moja kwa
taasisi tofauti, kudanganya
nyumba sio ya
familia wakati ni
ya familia na udanganyifu mwingine
mwingi ambao hulenga
kumnufaisha mkopaji.
2. ADHABU YA
KUTENDA KOSA LA UDANGANYIFU KATIKA KUCHUKUA MKOPO.
Kisheria tendo likishakuwa
kosa ni lazima
iwepo adhabu yake. Vivyo
hivyo mkopaji kumdanganya
mkopeshaji nalo ni
tendo ambalo huadhibiwa. Sheria inasema
kuwa hatia ya udanganyifu wa mkopaji
inapotangazwa basi adhabu
yake ni kulipa
faini ambayo ina
thamani ya nusu ya
mkopo aliokuwa amechukua. Hii ina
maana kuwa, kama alichukua
mkopo wa milioni
200 basi faini
yake ni milioni 100 halikadhalika
kama alichukua milioni
kumi basi faini
yake ni milioni tano.
Ikiwa hana hizo
hela basi itatakiwa
kwenda jela kutumikia
kifungo kisichopungua miezi
kumi na mbili. Kifungo kisichopungua
miezi kumi na mbili
maana yake kinaweza kuzidi miezi
kumi na mbili kutegemea na
ukubwa wa tatizo lenyewe. Hivyo wakopaji wajihadhari
na kutoa taarifa
za uongo hasa
kudanganya kuwa mali si ya
familia au kutumia
mali moja kuchukulia
mkopo sehemu zaidi
ya moja n.k.
3. UPENDELEO
KWENYE NYUMBA YA
MAKAZI
( a ) Sheria inasema
kuwa iwapo itabainika
kuwa nyumba iliyowekwa
rehani ni ya makazi
na mkopaji analeta
zuio la kutouzwa nyumba
hiyo basi mahakama
ikijiridhisha na hilo
inaweza kukubali ombi
hilo.
Mahakama itakubali ombi
hilo la kuzuia
nyumba kuuzwa kwa
kuzingatia kiwango cha
hela kilichosalia yaani kile kiasi ambacho mkopaji ameshindwa
kulipa. Mara kadhaa hutokea
kuwa mkopaji amelipa
kiasi kikubwa na
kusalia na deni la kiasi
kidogo ambacho kwa
akili ya kawaida
tu na kutokana na
mazingira yaliyopo akipewa
muda mwingine anao uwezo wa
kulipa na kumalizia
kabisa deni. Ni katika
mazingira haya zuio
la kutouzwa nyumba
ya makazi litakubaliwa.
( b ) Hili
litakwenda sambamba na
kuangalia iwapo wajibu
wa mkopaji uliowekwa
katika mkataba wa
mkopo unaweza kuzungumzika. Ikiwa mkopaji
alikuwa mgonjwa sana
na ushahidi upo
na hivyo alishindwa
kuendelea na biashara
na hivyo kutokurejesha, na sasa ana
afya njema na
anaweza kufanya biashara
na kurejesha, basi wajibu
wake ikiwa unaweza kurekebishika kwa
namna hiyo au
namna nyingine mahakama
inaweza kutoa zuio
ili kutoa nafasi
nyingine kwa mkopaji.
( c ) Pia
ikiwa mahakama itajiridhisha kuwa
nyumba husika ina
thamani kubwa kiasi kwamba hata
mkopaji akiongezewa muda
mwingine bado akishindwa
kulipa huko mbeleni nyumba
husika ikiuzwa mtoa
mkopo hatakuwa na
hasara ataweza kurejesha
hela yake yote pamoja
na riba, basi
zuio la kutouza
linaweza kutolewa kwa kulizingatia hilo.
Izingatiwe kuwa zuio
katika mazingira haya niliyoeleza linawezekana
ikiwa nyumba ilyowekwa rehani ni ya makazi.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment