NA BASHIR YAKUB -
Tulipoandika namna
bora na taratibu
maalum za kufuata unapotaka kununua
ardhi tulisema pia
kuwa taratibu za ununuzi wa
ardhi huwa zinatofautiana kutegenea
na mazingira
ya kila ardhi. Tukasema unaponunua
ardhi kwa msimamizi
wa mirathi ni
tofauti na unaponunua
kwa mmiliki mwenyewe. Unaponunua ardhi
ya familia ni
tofauti na unaponunua
isiyo ya familia. Vilevile unaponunua
ardhi ya kijiji
ni tofauti na unaponunua
ardhi isiyo ya
kijiji. Taratibu hutofautiana
na hasa tofauti
ipo katika nyaraka
ambazo zinatakiwa kuambatanishwa ikiwa
kama ithibati ya
ununuzi. Hata uandishi wa
mkataba wa manunuzi
pia nao huwa na tofauti katika
hili.
1.ARDHI YA
KIJIJI KWA UWEKEZAJI.
Wako watu wamekuwa
wakinunua ardhi hasa
huko vijijini lakini
baadae wamekuwa wakijikuta
katika migogoro mikubwa
na wenyeji. Mwamko wa
kununua maeneo kama
bagamoyo, kisarawe, huko
chanika dondwe na maeneo
mengine umekuwa mkubwa
sana. Hata hivyo mwamko
unavyoongezeka ndivyo na
migogoro inavyoongezeka.
Kubwa katika migogoro
hii ni hatua
ya wanunuzi kutokufuata
utaratibu wa ununuzi aidha
kwa kujua, kutokujua au
kupotoshwa.
Wakati mwingine
ni uelewa mdogo miongoni
mwa wenyeji lakini
zaidi ni hili
la kutofuata utaratibu. Mara zote
huwa tunasema ni
bora zaidi mgogoro
unapotokea halafu ukukute
ulifuata taratibu wakati
wa manunuzi. Bila shaka hautakuwa na
athari kubwa kwako
lakini ni mbaya
zaidi ukitokea halafu
ukukute kuna taratibu hukufuata kwa
bahati mbaya au
bila kujua. Unakuwa katika
hatari ya kupoteza. Unapokwenda kununua
ardhi ya kijiji
kwasababu yoyote ile hasa
uwekezaji upo utaratibu maalum wa kufuata nitakaoeleza.
2. ARDHI
YA KIJIJI NI
NINI.
Ardhi ya kijiji
ni ile ardhi
iliyopo katika mipaka
ya kijiji fulani
ilyoainishwa na mamlaka
za wilaya husika
huku ikiwa na
hati ya usajili wa
kijiji. Ardhi hii hulindwa
kwa taratibu za
kimila za eneo
husika ikiwa ni
pamoja na sheria namba
4 ya 1999.
3. UTARATIBU
WA KUNUNUA ARDHI
YA KIJIJI KISHERIA.
( 1 ) Maombi maalum huandaliwa na
kuwasilishwa kwa mtendaji
wa kijiji ambaye
hupatikana katika kila
kijiji.
( 2 ) Maombi huandaliwa
katika fomu maalum
ambazo hupatikana katika
kila ofisi za
kijiji. Si maombi ambayo
huandaliwa kama barua
za kawaida za maombi.
( 3 ) Ikiwa mwombaji
ni mtu mmoja
basi atasaini sehemu
maalum na ikiwa ni
maombi kwa niaba
ya famliia basi
watu wawili kutoka
ile familia watasaini
na ikiwa ni
ardhi kwa ajili
ya kikundi pia
wawakilishi wasiopungua wawili kutoka
kile kikundi watasaini
kwa niaba ya
wengine.
( 4 ) Kama
mwombaji ni chama
cha ushirika au
kampuni basi inatakiwa
kuwepo wadhamini wawili
kwa ajili ya
shirika au kampuni
hiyo. Wanaweza kuwa zaidi
ya wawili lakini
wasipungue.
( 5 ) Kama
anayeomba ardhi si
mwenyeji wa eneo husika basi
atatakiwa kuwa na
wadhamini wasiopungua watano
ambao ni wenyeji
wa eneo hilo. Sharti
ni kuwa kati ya
hao wadhamini wasiwepo
ndugu wa mwombaji.
( 6 ) Mwombaji atatakiwa
kuambatanisha katika maombi yake
tamko linaloonesha ardhi
nyingine anayoimiliki Tanzania
nje na hiyo
anayoomba.
( 7 )
Ikiwa ardhi inaombwa
kwa ajili ya
makazi basi mwombaji
atatakiwa kuambatanisha tamko
linaloonesha kuwa ataanza
ujenzi wa makazi hayo ndani ya miezi mitatu
tangu siku ya kuidhinishiwa ardhi.
( 8 ) Ikiwa mauzo
ni heka 50 au kuendelea ni lazima
yaidhinishwe na mkutano
mkuu wa kijiji.
( 9 ) Baada ya
kukamilisha taratibu hizo
halmashauri ya kijiji
itakaa vikao na
ndani ya siku
tisini itatakiwa kutoa majibu.
Kamwe usikubali kuuziwa
ardhi ya kijiji
na viongozi wa
kijiji bila kufuata
utaratibu huu. Hii hasa ni
kwa wawekezaji wanaochukua
maeneo makubwa kwa
shughuli za kiuchumi.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment