NA BASHIR YAKUB -
Hela ya mifuko
ya hifadhi ya jamii ni hela ambayo
mwajiriwa hukatwa kiasi
kadhaa katika mshahara wake na
mwajiri hutoa kiasi
kadhaa na kuhifadhiwa
katika mfuko uitwao mfuko
wa hifadhi ya jamii. Mfuko wa hifadhi ya jamiii ni
kama NSSF, PSPF, LAPF, GEPF n.k.
Hii ndio mifuko ya
hifadhi ya jamii. Ipo
mifuko ya hifadhi
ya jamii ambayo huhudumia
mashirika ya umma
na ipo mingine
ambayo huhudumia mashirika
binafsi, makampuni binafsi na sasa ipo inayohudumia hata wajasiriamali wadogo
ambao sio kampuni
wala shirika.
1.LENGO LA MIFUKO HII.
Lengo kuu ni
kumpunguzia mtumishi au mfanyakazi machungu
ya maisha pindi anapostaafu
au kuacha kazi.
Ni kumwezesha mtu kuweza
kukabiliana na maisha
yake baada ya
kutokuwa na kazi
iliyokuwa ikimwingizia kipato. Ni
kumfanya asikose hata
matumizi ya kawaida
kama chakula, malazi, mavazi na
hata matumizi kama
ada za shule
,matibabu n.k. Mifuko hii
haipo Tanzania tu bali
ni ajenda ya
dunia. Ukienda ulaya, Amerika, Asia na
kote Afrika utaikuta.
2. HAKI
YA MWAJIRIWA KUSAJILIWA
NA MIFUKO HII.
Ni haki ya
kila mwajiriwa kuwa amesajiliwa
na mfuko wa
hifadhi ya jamii. Ni jukumu la
kila muajiri kuhakikisha
kila mwajiriwa wake
amesajiliwa katika mfuko
wa hifadhi ya
jamii. Suala la
mfanyakazi kusajiliwa katika
mfuko wa hifadhi
si hiari au
hisani kwa mwajiri.
Ni lazima afanye
hivyo kwakuwa ni
takwa la kisheria. Wapo
wafanyakazi wengi wameajiriwa
kwa mikataba lakini
hawajasajiliwa na mifuko hii.
Kufanya hivyo ni
kukiuka haki ya
mfanyakazi. Kusajiliwa na
mfuko wa hifadhi
ni katika mambo ambayo
yanatakiwa kufanywa awali
kabisa ajira ya mtu inapoanza.
Ni wajibu wako
mfanyakazi pia kuhakikisha
unamkumbusha mwajiri wako
kufanya hivyo na/au
ikishindikana waweza kumchukulia
hatua.
3. NI KOSA LA
JINAI KUTOMSAJILI MWAJIRIWA
KATIKA MFUKO WA
HIFADHI.
Ukisikia makosa ya jinai ni
yale makosa ambayo
mtu hushitakiwa na Jamhuri. Ni makosa ambayo mnatendeana wawili lakini
anayeshitaki ni Jamhuri/serikali. Ni makosa ambayo
ukipatikana na hatia
adhabu zake huwa
ni vifungo, faini na
wakati mwingine kuchapwa
bakora. Kwa maana
hii mwajiri yeyote ambaye amekataa
kumsajili mfanyakazi wake
katika mfuko wa
hifadhi ya jamii
anakuwa ametenda kosa
la jinai ambapo
anastahili kuadhibiwa. Kosa hili limeingizwa katika
makosa ya jinai
kutokana na umuhimu
wa mifuko hii. Lakini pia ni
kutokana na ukweli
kuwa waajiri wengi
wasingependa kuwasajili waajiriwa
wao kwakuwa wao
hutakiwa kuchangia asilimia
kadhaa ya fedha
kila mwezi . Kwakuwa wasingependa
wachangie fedha hizi
ndio maana ikaingizwa
kwenye jinai ili
wa kuogopa na
aogope.
4. KULIPWA
HELA YA HIFADHI
UNAPOFUKUZWA KAZI.
Wapo wanaojua kuwa
mtu anapofukuzwa kazi
kwa makosa basi
hupoteza haki ya fedha
hizi za mfuko
wa jamii ambao
amekuwa akizichangia. Hili
si kweli. Kuacha
kazi kwa kustaafu,
kufukuzwa kazi, kumaliza mkataba au kuvunjiwa mkataba
vyote kwa pamoja
hutoa nafasi kwa
mwajiriwa kupata haki
yake ya fedha
za hifadhi ya jamii.
Ni wajibu wa
mwajiri kuhakikisha mfanyakazi
kabla ya kuondoka
ofisini kutokana na
sababu nilizotaja anamshughulikia kuhakikisha anapata fedha
zake za hifadhi
ya jamii. Ikiwa fedha hizi
hazikutolewa basi ni
haki ya mfanyakazi
kumfungulia mashtaka mwajiri
kumtaka amlipe fedha
hizo. Fedha hizi
ni moja ya stahili anazostahili
mwajiriwa pindi anapomaliza
kipindi chake cha
utumishi aidha kwa
kufukuzwa kazi, kuvunjiwa
mkataba au vinginevyo. Ni
haki na ni
lazima fedha hizo kulipwa.
5. JE MFANYAKAZI ANA HAKI
YA KUCHAGUA MFUKO
ANAOUTAKA.
Mifuko ya hifadhi
ya jamii ipo mingi
na hutofautiana masharti
pamoja na faida. Hilo linaibua swali la nani ana haki
ya kuchagua mfuko kati
ya mwajiri na
mwajiriwa. Kimsingi sheria haijaweka
wazi nani kati ya
hawa wawili ana
haki ya kuchagua
mfuko. Hii ina maana suala
la mfuko upi utumike laweza
kuwa suala la
maelewano baina ya mwajiri na
mwajiriwa wakati wa kuingia
mkataba. Hata hivyo mazoea(practise) imekuwa
ni mwajiri ndiye
humchagulia mwajiriwa mfuko.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment