NA BASHIR YAKUB -
Wapo wafanyakazi wengi ambao
wanasumbuliwa na migogoro ya kikazi
maofisini kwao lakini
hawajui nini wafanye. Wengine hufanyiwa
mambo ya ajabu
huko makazini yumkini
wakashindwa kuchukua hatua yoyote kutokana na
kutojua waanzie wapi na waende wapi. Na hizo
ni ajira rasmi tusiongelee hizo
zisizo rasmi. Tusiongelee vibarua
huko viwandani na
kwenye maeneo mbalimbali
ya ujenzi hasa yale
yenye miradi mikubwa
kama ya barabara,
madaraja n.k. Tusiongelee
wafanyakazi wa ndani na kazi
nyingine zinazofanana na hizo. Hawa hupata
shida sana na mbaya
zaidi hukosa msaada hata
wa kujua ni
hatua gani wachukue. Kimsingi unaposumbuliwa na mgogoro wowote
wa kazi zipo
hatua za kuchukua
ambazo zimeainishwa na sheria. Ni hatua
nyepesi tu labda
mtu usipende kuzichukua.
1.KUJIUNGA NA
VYAMA VYA WAFANYAKAZI.
Huwa kuna umuhimu
mkubwa wa kujiunga
na vyama vya
wafanyakazi. Hii ni
kwasababu unapokuwa mwanachama
pindi unapotokea mgogoro
kitu cha kwanza
unatakiwa kutoa taarifa
kwenye chama chako ambapo
uongozi wa chama chako
utawasiliana na waajiri wako kwa ajili
ya kukutetea. Pia ikiwa
mazungumzo kati ya chama chako
na waajiri yatashindikana basi
chama hubeba jukumu
la kwenda mahakamani
moja kwa moja
kukutafutia haki yako. Huu
ndio umuhimu mkubwa wa
kujiunga na vyama
hivi. Unapokuwa unafanya
kazi hebu jaribu
kuuliza kuhusu vyama
hivyo utaelezwa, utajiunga
na kuwa mwanachama
kwa ajili ya maslahi yako kesho.
2. PELEKA
MGOGORO WAKO TUME YA
USULUHISHI.
Tume ya usuluhishi
wa migogoro ya
kazi huitwa MEDIATION. Kisheria tume
hii inaainishwa na sehemu
ya II ya sheria
namba 7 ya
taasisi za masuala
ya kazi ya
2004. Unapokuwa na mgogoro kwa
mara ya kwanza
ni vema ukatafuta
tume hii ilipo
na kupeleka mgogoro wako . Ukifika hapo
utapewa fomu maalum
ya kujaza na
baada ya hapo
mwajiri wako ataitwa
kwa ajili ya
usuluhishi. Kwa walio Dar
es salaam tume
hii ipo jengo
la msalaba mwekundu
eneo la akiba
makutano ya bibi titi
na morogoro.
Mgogoro
wowote unakubalika unaweza
kuwa mgogoro wa
kimaslahi kwa mfano kutaka
kuongezewa mshahara, kutoridhishwa
na mazingira ya
kazi, kufanya kazi
kinyume na mkataba n.k. Pia unaweza kuwa mgogoro wa
malalamiko kwa mfano
kufukuzwa kazi bila
kufuata taratibu, kupunjwa
mafao , kuvunjiwa mkataba kinyume
na sheria n.k.
Hakikisha unapeleka
mgogoro wako ndani ya siku
30 tangu kutokea
kwa mgogoro huo. Hata
hivyo kama zimepita
siku 30 na unazo
sababu za msingi za kwanini hukupeleka
mgogoro ndani ya muda
huo basi
utajaza fomu ya kuomba
kuongezewa muda huku ukitoa
sababu za kwanini
ulichelewa.
3. MGOGORO
KWENDA TUME YA
UAMUZI.
Hapo juu tumeona
kuwa mwajiri wako ataitwa kwa
ajili usuluhishi ili kupata muafaka
wa mgogoro. Hata hivyo usuluhishi unaweza
kushindikana kwa kutoelewana
katika nukta fulani fulani. Ikiwa usuluhishi
utashindikana basi mgogoro
utaenda tume ya
uamuzi. Katika tume hii
kila upande utatoa
maelezo yake na
ushahidi. Upande wa mwajiri
utatoa maelezo na
upande wa muajiriwa
nao utatoa maelezo.
Tume hii itasikiliza
na kutoa maamuzi. Maamuzi
ya tume hii
yana nguvu za
kisheria kama maamuzi
ya mahakama na hivyo
yakitolewa ni lazima
yafuatwe.
Zingatia kuwa katika
hatua zote hizo
juu yaani wakati
wa usuluhishi na wakati
wa uamuzi unaweza kumtafuta
mtu wa kukuwakilisha
ikiwa ni mwanasheria, chama cha
wafanyakazi au mtu unayeamini
anaweza kukusaidia katika
masuala ya kazi. Hili
linaruhusiwa.
4. MGOGORO
KWENDA MAHAKAMA KUU YA
KAZI .
Ikiwa
hukuridhishwa na maamuzi
ya tume ya
uamuzi hapo juu basi
unaruhusiwa ndani ya
siku 30 tangu siku ya kutolewa maamuzi
hayo kupeleka shauri
hilo katika mahakama kuu
ya Tanzania. Utaiomba
mahakama kuu irejee(revise) vipengele
kadhaa unavyolalamikia unavyohisi
tume ya uamuzi
haikutenda haki. Ikiwa
pia haukuridhika na
maamuzi ya mahakama
kuu basi utapeleka
rufaa yako mahakama
ya rufaa ikiwa
suala lako lina
hadhi ya kwenda
huko.
Kubwa na muhimu
kuliko yote kwenye makala haya ni kujua kuwa mgogoro
unapotokea, haraka ndani ya siku 30 upelekwe baraza la
usuluhishi. Kwa walio mikoani
au wilayani kujua ilipo tume
hii nenda makao makuu
ya wilaya au
mkoa ulizia hapo watakuonesha ilipo tume. Hapo
utapata muongozo wa kila
kitu nilichosema humu
na ni bure.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment