NA BASHIR YAKUB -
Makala haya yataeleza
tofauti kati ya
kibarua na ajira
ili isiwe unaitwa
kibarua kumbe kisheria
umeajiriwa na unastahili
stahiki zote za
kiajira. Wako watu wengi
wanafanya kazi lakini hawajui
wanafanya kazi katika
mwavuli upi. Yawezekana
mtu akawa amefanya
kazi miaka mingi
lakini bado kazi
anayofanya haitambuliki anaifanya
kama nani. Na
mara nyingi hii
hujitokeza katika kazi
zile ambazo si
za kitaaluma. Kazi
zisizo za kitaaluma
ni kama kufanya
kazi za ndani, kusaidia mashambani,
kusaidia katika ujenzi na
nyingine zinazofanana na
hizo. Lakini pia
siku hizi kutokana
na ongezeko la ukosefu
wa ajira hata kazi ambazo
ni za kitaaluma
nazo zimekumbwa na janga
hili.
Kwa sasa katika ofisi
nyingi wapo watu
wanafanya kazi za
kitaaluma lakini haijulikani
kama wameajiriwa au
ni vibarua. Wapo watu
wamekaa maofisini hata miaka mingi
wakiitwa wafanya mazoezi ( intern). Wapo wahasibu, madaktari, walimu, wachumi, na
wengine wengi. Waajiri
hupenda sana hali
hii kwakuwa huwapatia
faida kubwa. Kwanza
huwalipa kiduchu watu
hawa lakini pili hukwepa
kulipa stahiki zao nyingine
za kiajira kama
malipo ya muda
wa ziada,matibabu, likizo, kuumia kazini
na stahiki nyinginezo.
1.NINI MAANA
YA AJIRA.
Ajira ni mahusiano
ya kikazi kati ya mwenye
kazi na mfanyakazi
ambapo mwenyekazi huwa
na mamlaka ya kutawala,
kudhibiti, na kuelekeza namna ,
jinsi, na wakati gani
kazi husika ifanyike. Wako
watu wanafikiria na
kujua kuwa ili
kazi iitwe ajira
ni lazima yawepo
maandishi ya kimkataba.
Hapana hili si lazima.
Muhimu ni kama
inavyoelekezwa katika
tafsiri hapo juu. Hii ina
maana ili kazi
iitwe ajira vipo vigezo
vinavyozingatiwa na hasa
hivyo nilivyotaja kwenye
tafsiri. Kimsingi yapo
mambo matano ambayo
yakitokea kazi yoyote
unayofanya itaitwa ajira
na utastahili kupata
haki zote za
kiajira kama muajiriwa.
Tutaona mambo hayo hapa
chini.
2. JE
WE NI KIBARUA
AU MUAJIRIWA.
Yapo mambo matano
yatakayokujulisha kuwa we si kibarua
bali ni muajiriwa.
( a ) Kwanza ikiwa
una mkataba maalum
unaoeleza aina kazi
unayofanya, sehemu ya
kazi, pesa unazolipwa, , muda wa
kazi, likizo na mengine usiambiwe
wewe ni kibarua. Makubaliano ya
kimaandishi ya namna
hii yanakupa hadhi
ya muajiriwa na
unastahiki haki zote
za muajiriwa kwakuwa
we utakuwa ni muajiriwa
na si kubarua.
( b ) Pili
ikiwa vitendea kazi
unavyotumia vinamilikiwa na
mwenye kazi, mfano
we ni dereva
na gari si
la kwako ni
la tajiri, unafanya usafi
lakini vifaa vyote
vya usafi ni
vya tajiri, unafanya
kazi za ndani na
kila kitu ndani
ni cha tajiri. Basi
ikiwa hilo liko
hivyo ni kigezo
kuwa hiyo ni
ajira na si
kibarua.
( c ) Tatu
ikiwa mamlaka ya kuamua kazi ifanyike
vipi, kwa namna
gani na kwa wakati
gani anayo yule aliyekupa
kazi basi nacho
ni kipimo kuwa
hiyo ni ajira. Kwa
mfano bosi na
sekretari wake. Kwakuwa
bosi ndiye huagiza
kazi ifanyike vipi, kwa
namna gani n.k bosi
huyo hawezi kusema
kuwa hajamuajiri huyo
sekretari. Hii ni tofauti na
pale unapomleta fundi
ujenzi nyumbani. Utamuonesha
kazi lakini hutakuwa
na uwezo wa
kumuelekeza afanyeje kazi
kwakuwa yeye ndiye fundi na anajua namna ya kufanya
kazi yake.
( d ) Nne
suala la nani
anawajibika na hasara
inapotokea nalo ni kipimo
iwapo umeajiriwa au ni kibarua.
Kwa mfano ukimkodisha
dereva hata kwa
miaka miwili ikiwa
kila gari linapoharibika au
kupata ajali hutengeneza yeye
hawezi kusema umemuajiri,
lakini ikiwa utatengeneza
wewe unayemkodi dereva
basi itakuwa ni kipimo
kuwa yupo katika
ajira.
( e ) Tano ni
faida. Nani hunufaika
na faida nacho
ni kipimo ikiwa umeajiriwa
au ni kibarua.
Haya ndiyo mambo
makuu yatakayokuashiria ikiwa
umeajiriwa au unafanya
kibarua na si
mengineyo.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment