NA BASHIR YAKUB -
Kama ilivyo makubaliano
katika shughuli nyingine
za kijamii ajira
nayo huwa na makubaliano maalum
wakati inapoingiwa. Makubaliano haya ndiyo
huitwa mkataba na yumkini
huingiwa kati ya
wahusika wawili yaani
muajiriwa na muajiri. Aina
ya mahusiano wanayoingia
wahusika ndiyo huibua
aina za haki na wajibu
kwa pande zote
mbili. Mwenye haki hutakiwa
kutoa haki hiyo
kwa mwenzake naye
mwenye wajibu huwa
hana hiari isipokuwa kutekeleza
wajibu huo kwa
mujibu wa makubaliano. Hapa
Tanzania taratibu za
ajira na mahusiano
kazini huongozwa na
Sheria namba 6 ya
ajira na mahusiano
kazini 2004. Sheria hii
hueleza wajibu, haki,
stahili, kuacha na
kuachishwa kazi na
kila kitu kinachohusu
ajira na kazi
kwa ujumla wake.
1.NANI HUANDAA
MKATABA WA AJIRA.
Mara nyingi waajiri
ndio huandaa mikataba
ya ajira . Kwa
swali la nani
aandae mkataba wa
ajira, sheria Ya ajira
Na Mahusiano kazini
hailazimishi upande wowote
kati ya muajiri
au muajiriwa kuandaa
mkataba. Sheria hii inachotambua
ni kuwa mkataba
wa ajira ni
makubaliano yanayohusisha ridhaa
maalum kutoka pande
mbili zinazoingia makubaliano
hayo. Kwa msingi
huo yeyote kati
ya hao wanaokubalina
anaweza kuandaa mkataba
wa ajira halafu
akahusisha upande mwingine
kupitia kuusoma na
kuridhia au kutordhia. Muhimu hapa
ni kuwa ikiwa
mwajiri ataandaa mkataba
huo basi mwajiriwa
apewe nafasi ya
kuusoma na kuulewa
kabla ya kuusaini. Ikiwa kuna
sehemu angependa liongezwe
jambo au lipunguzwe
hayo yatakuwa ni makubaliano yao. Hata
hivyo kutokana na
changamoto ya ukosefu
wa ajira waajiriwa
wamekuwa wakilazimika kusaini
mikataba ya ajira
yenye masharti magumu
bila kuhoji kwa
kuhofia uwezekano wa
kupoteza nafasi hizo.
2. AINA
YA MIKATABA YA AJIRA.
Kuna aina kuu
mbili ya mikataba
ya ajira. Makubaliano
ya ajira yoyote aliyonayo
mtu yapo katika kundi kati
ya haya makundi
mawili.
( A ) MKATABA WA
MDOMO ( oral contract).
Haya ni makubaliano
ya mdomo kama
jina lenyewe lilivyo. Mwajiri na
mwajiriwa wanakubaliana katika
kutekeleza shughuli fulani
kwa mdomo au
mazungumzo tu. Ajira
zisizo rasmi ndizo
huhusika na mikataba
hii zaidi. Ajira
zisizo rasmi mara
nyingi ni zile ajira zisizo
za kitaaluma kwa
mfano kazi za
ndani, usaidizi katika ujenzi, shughuli ndogondogo
za viwandani na kwenye
makarakana, kuuza kwenye migahawa
na mahoteli ,shughuli nyingine
katika maeneo ya
wajasiriamali na
kazi nyingine zote
zinazofanana na hizo.
Kifungu cha 32
, sura ya
366 cha sheria ya
ajira ndicho kinachotaja aina
hii ya ajira. Mara nyingi ajira
za namna hii huwa
sio za muda mrefu .
Ni ajira ambazo
huwa sio za mwendelezo
ambapo mfanyakazi hufanya
kazi kwa muda
tu na kupangiwa
kazi nyingine au
kuachishwa.
MUDA WA UKOMO AJIRA
YA MKATABA WA
MDOMO.
Ili kulinda maslahi
ya wafanyakazi wanaofanya
kazi katika mikataba
ya ajira ya mdomo
sheria imeweka utaratibu
maalum wa namna ya kulipwa
mishahara yao ikiwa
ni pamoja na
haki nyinginezo. Moja
ya jambo ambalo
limezingatiwa ni muda
ambao ajira ya
mkataba wa mdomo
inapaswa kukoma . Sheria imetoa
kipindi cha mwaka
mmoja tu katika
kudumu kwa kwa
ajira ya mkataba
wa mdomo. Baada ya
mwaka mmoja mfanyakazi
anatakiwa kupewa mkataba wa maandishi
unaofafanua bayana haki
na wajibu wake . Hivyo
ni kosa mfanyakazi
kuendelea na mkataba wa mdomo kwa mwaka
zaidi ya mmoja.
Hili ni kosa
kwa upande wa
mwajiri.
( B ) MKATABA
WA AJIRA WA
MAANDISHI.
Kifungu cha 15,
sura ya 366
cha sheria namba
6 ya ajira na
mahusiano kazini kinaueleza
mkataba wa ajira wa maandishi.
Huu ni
uleule ambao wengi
tumeuzoea ambao huwa
katika maandishi huku ukiwa
umesainiwa na pande
zote mbili yaani
upande wa muajiri
na muajiriwa. Mkataba huu
hueleza muda wa
kazi, kiwango cha mshahara, muda wa
uangalizi na kila
kitu kinachohusu haki
na wajibu wakati
wa kazi. Hizi
ndizo aina kuu mbili za
mikataba ya
ajira.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO KILA JUMANNE
, GAZETI JAMHURI KILA
JUMANNE NA GAZETI
NIPASHE KILA JUMATANO.
0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment