NA BASHIR YAKUB -
Kisheria yapo mambo
mengi ambayo huweza
kubatilisha mkataba wa
ajira kati ya
mwajiri na mwajiriwa. Mkataba wa
ajira sawa na
mikataba mingine yote huzaliwa, huishi
na hufa. Huzaliwa pale
tu unaposainiwa , huishi
pale unapoanza kutekelezwa
na hufa pale
yanapojitokeza baadhi ya
mambo ambayo yameainishwa
na sheria kama mambo
yanayoua mkataba wa ajira. Aidha zipo taratibu
maalum za kumaliza/kuua
mkataba wa ajira
na hii ni
katika mazingira yote, yaani
mazingira ya kumaliza mkataba
kwa hiari na yale
ya kumaliza kwa kulazimika
kutokana na sababu
mbalimbali. Kumaliza mkataba wa ajira kwa
hiari kumekuwa hakuleti
shida sana kama
ilivyo kumaliza mkataba
wa ajira kwa kulazimika hasa linapokuja suala la sababu za kinidhamu
kama tutakavyoona.
1.KUACHISHWA KAZI
KWASABABU ZA KINIDHAMU.
Ni kweli sababu
za kinidhamu ni
sababu za msingi
zinazoweza kumpelekea mwajiriwa
kupoteza ajira yake. Hata
hivyo sababu hizi
zimekuwa zikitumiwa vibaya
na waajiri. Zimekuwa zikitumika
kama sehemu ya kuoneshana uwezo
kati ya mtu na bosi
wake,kukomoana, hila, pia zimekuwa
zikitumika kama sehemu
ya kulipiziana visasi
na wakati mwingine
hutumika kumwondoa mfanyakazi
mmoja ili mwingine
apate kuajiriwa. Haya ni
makosa makubwa kwa
mujibu wa sura ya 366
Sheria ya ajira 2004. Ikumbukwe sheria inaposema
ni halali kumfukuza
mwajiriwa kwa sababu za
kinidhamu haimaanishi kuwa
mwajiri amtafutie mwajiriwa
kisa. Lazima sababu
hizo ziwe zimejitokeza
kweli na ziweze
kuthibitishwa. Isiwe habari
ya nilisikia au nahisi
au tuhuma tu
zisizo na mashiko.
2. HAIRUHUSIWI
KUMFUKUZA MWAJIRIWA MARAMOJA.
Kwa lugha ya
kitaalam kufukuzwa mara
moja huitwa “summary
dismissal”. Hii ni hatua
ambapo mwajiriwa anaweza
kufika kazini leo na
kuambiwa
hamna kazi kwasababu
hizi na hizi
na hivyo rudi nyumbani na
kuanzia leo usije tena
hapa. Kufukuzwa kwa
mtindo huu humfanya
mwajiriwa kupoteza haki
zake ikiwemo kiinua
mgongo ikiwa ni pamoja na kutopewa taarifa( notice) ya
kisheria. Hata hivyo ni muhimu sana
kueleweka kuwa ufukuzaji wa
namna hii kwasasa hauruhusiwi hasa
baada ya sheria ya
ajira kufanyiwa marekebisho
mwaka 2004 na
2009. Hapo nyuma wapo wengi
wamefukuzwa kwa mtindo
huu lakini kwasasa
kwakuwa kitu hiki hakipatikani
tena katika sheria
hii
maana yake ni
kwamba hakiruhusiwi. Kwahiyo
twaweza kusema kuwa ni
makosa kwa mwajiri
kumfukuza mwajiriwa kwa
mtindo wa mara
moja “summary dismissal”.
Hii ni
hata kama mwajiriwa alitenda
kosa kubwa la
kinidhamu bado utaratibu huu hautaruhusiwa.
3. KULIPWA MSHAHARA
BAADA YA KUFUKUZWA
KAZI KWASABABU ZA
KINIDHAMU.
Katika haki alizonazo
mwajiriwa aliyefukuzwa kazi
kwasababu za kinidhamu
ni pamoja na
kulipwa mshahara wake au ujira
kisheria. Hii ni
kutokana na kifungu
cha 44 sheria namba 6 ya
ajira na mahusiano
kazini. Kwa mujibu
wa kifungu hiki
mshahara hulipwa kwa
kuhesabu kuanzia tarehe
ya mshahara wa mwisho
mpaka siku aliyofukuzwa
kazi mwajiriwa. Hii
ina maana ikiwa
tarehe ya mwisho ya
kupokea mshahara ilikuwa tarehe 31 January 2015 halafu ukafukuzwa
tarehe 21 february 2015 basi
utatakiwa kulipwa kiwango cha
pesa kinacholingana na
hizo siku ulizofanya
kazi yaani siku
21 kuanzia tarehe
1 hadi tarehe
21. Hii ni haki
ya msingi.
4. LAZIMA KUPEWA
NAFASI YA KUJITETEA
JAPO KOSA NI
LA KINIDHAMU.
Haki ya
kusikilizwa ni haki
ya asili. Ni haki
ambayo haiwezi kuondolewa
na mtu. kampuni au taasisi
yoyote. Kwa maana hii hata
kosa la mwajiriwa
liwe kubwa kwa
kiwango gani ni
lazima apewe nafasi asikilizwe
na ajitetee kwanini
asichukuliwe hatua. Hii ni
kwa mujibu wa
kanuni ya 13 ( 3 ) ya
sheria ya ajira na
mahusiano kazini. Ni
makosa kumfukuza mwajiriwa
bila kumpa nafasi ya
kusikilizwa na kujitetea.
Kusikilizwa ni lazima
kuwe kule kulikotekelezwa na
mamlaka husika za ofisi ya mwajiriwa kwa
mfano bodi, kamati
n.k.
Nataka nisisitize hapa
kuwa ukubwa wa
kosa kwa namna
yoyote ile hakuathiri
au hakuingilii haki
za mwajiriwa. Haki zote zikiwemo
hizi nilizotaja hapa ni
lazima apatiwe mwajiriwa bila kujali
ametenda kosa kubwa
kiasi gani. Sio
hiari ya mwajiri
kumpatia mwajiriwa haki
hizi. Hii ni kwasababu
haki hizi zipo
kisheria na kutekelezwa
kwake ni wajibu.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment