NA BASHIR YAKUB -
Wako watu ambao
hawajui hatua za
kuchukua iwapo ndugu zao
hawataki kugawa mirathi
ili kila mtu achukue chake. Unakuta ndugu
ni wengi au wachache na marehemu
ameacha mali kwa
wosia au bila
wosia. Miezi inakwenda
miaka inakwenda waliopewa jukumu la
kuangalia mali hizo
hawataki kuzigawa ili
kila mtu apate
haki yake. Wengine mpaka
wamekufa bila kupata
haki yao ya
mirathi na kuwaacha
watoto au bila
watoto. Kisheria nini ufanye
katika mazingira kama
haya.
1.HAKI YA
KUGAWANA MIRATHI.
Mtu anapokufa na kuacha
mali iwe kwa wosia au
bila wosia kisheria
ni haki ya
waliobaki ambao ni warithi
halali kugawana zile mali .
Suala la
kugawana mali sio ombi
isipokuwa ni haki
ambayo ni lazima itekelezwe.
Mara nyingi unakuta
yule aliyepewa mamlaka
ya kusimamia mali
za marehemu awe
kaka, dada, baba mkubwa au
mdogo anakaa na
zile mali miezi na miezi,
miaka na miaka
na hataki kusikia
lolote kutoka kwa mtu
yoyote kuhusu kugawa
mali na kila
mtu kuchukua chake.
Unakuta kila
mara anapoombwa na mmoja
wa ndugu kugawa
zile mali anakuwa
mkali sana,analeta sababu
zisizoeleweka,anakwepakwepa ilimradi tu watu
wasichukue chao. Uzoefu unaonesha kuwa mara nyingi
mtu wa namna
hii huwa kuna namna
anavyofaidika na zile
mali wakati wengine
hawafaidiki kwa namna
yoyote. Unaweza kukuta labda anakusanya kodi
au kama ni mradi
unazalisha basi yeye
ndiye anayefaidika na
mapato huku akiendeshea maisha yake.
Hili si sawa
kwa mujibu wa sheria ya
mirathi sura ya
352. Kwa mujibu wa sheria
hiyo
mirathi ni haki
ya msingi kwa wale
wote wanaotakiwa kufaidika nayo.
Suala la kugawa
mirathi na kila
mtu kupata kilicho chake
si la hiyari
isipokuwa ni lazima. Labda iwe
warithi wote bila kuacha
hata mmoja wawe hawataki igawiwe .
2. SUALA
LA WINGI WA NDUGU
WASIOTAKA MIRATHI IGAWIWE.
Yawezekana ndugu walio wengi
hawataki mirathi igawiwe na
wachache ndio wanataka
igawiwe. Kitu ambacho tunatakiwa
kuelewa ni kuwa
hata iwe wengi
ndio hawataki igawiwe
hilo haliondoi haki
ya wachache. Na
hili hata mtu
akiwa mmoja anataka
igawiwe na wengi
ndio hawataki bado haki yake
inatakiwa ipatikane. Ikiwa walio
wengi hawataki kugawana
basi wao mirathi
yao wasigawane ibaki
hivyohivyo isipokuwa basi
wamtolee fungu lake
huyu mmoja aende zake. Kitu ambacho
hakipo kwenye sheria na ambacho kinatokea
katika familia nyingi
ni ile tabia
ya walio wengi
kusema sisi wengi tumeamua hivi
na hivyo maamuzi
ya wengi ndiyo yanayosimama. Lazima
tujue kuwa suala
la mirathi halitekelezwi
kwa upigaji kura kama ilivyo katika
siasa kwa mtindo wa
wengi ndio washindi (super majority/simple majority).
Suala la mirathi
ni suala linalozaliwa
na haki na
haki haina wingi. Yawezekana ndugu
wakawa hata arobaini
lakini kwakuwa ni
suala la haki
ndugu mmoja tu
akatakiwa kutekekelezewa kile
anachotaka.Kwa ufupi hapa hakuna
wingi , hakuna ukubwa,
hakuna ukaka wala
udada isipokuwa kila
mrithi mdogo au
mkubwa , tajiri au
maskini anatakiwa kupata
fungu lake iwapo atalihitaji.
3. NINI UFANYE
IWAPO NDUGU WAMEKATAA
KUGAWA MIRATHI ILI UPATE
CHAKO.
Ikiwa ndugu wamekataa
kukumegea fungu lako
ili uendelee na
maisha yako tena
bila sababu za
msingi basi una
haki kufungua shauri
mahakamani kuwaita na
kuwauliza kwanini mahakama isiwachukulie
hatua kwa kukataa
makusudi kutoa haki
yako ya kisheria. Ikiwa hawatatoa sababu
za msingi basi
mahakama itaagiza kufanyika mgao na
itatoa muda kwa hilo. Hii
ni namna ya pekee
ya kuwashinikiza watu wa namna
hii kutoa haki za
warithi.
Aidha yafaa tuelewe
kuwa baadhi ya migogoro mikubwa
ya mirathi ambayo
imekuwa ikizikumba familia nyingi inatokana
na tatizo hili
la kutogawana mirathi kwa wakati.
Mtu anakufa anawaacha
warithi, warithi nao
wanaanza kufa mmoja mmoja
wanawaacha warithi wengine. Matokeo yake
warithi wa kwanza ambao
hawajafa na warithi
wanaozaliwa na warithi
waliokufa wanashindwa kuelewana
kuhusu nani anastahili
kupata nini. Hawa wanasema
tunahitaji fungu la
mama yetu au
baba yetu aliloachiwa
na wazazi wake
na hawa wanasema
wajukuu huwa hawarithi. Mgogoro unakuwa
mkubwa bila sababu wakati
kila mtu angepata
chake mapema na
kwa wakati hayo
yote yasingetokea.
MWANDISHI
WA MAKALA HAYA
NI MWANASHERIA NA
MSHAURI WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment