NA BASHIR YAKUB -
Wakati nilipoandika kuhusu
talaka
na mambo yanayokubalika kisheria
kama sababu za
talaka nilipata maoni
na maswali mengi kutoka kwa wasomaji wetu. Kati
ya hao ni mmoja
ambaye alijitambulisha kwa
jina na kuwa
ni mkazi wa kinondoni Dar es
salaam. Huyu aliuliza swali
lake ambalo ndilo
kichwa cha makala
haya. Alisema ameziona
sababu nilizoeleza ambazo
zinapelekea mtu kupewa
talaka lakini sababu
inayohusu tatizo lake
hakuiona na hivyo
aliomba nimpatie ufafanuzi. Maelezo yake
kwa ufupi yalikuwa
hivi:
1.KUPATA MIMBA
NJE YA NDOA.
Ndugu huyu alichoeleza
ni kuwa yeye ni
muajiriwa katika jeshi la
Wananchi wa Tanzania.
Na kuwa mwaka
jana alipangiwa safari
ya kikazi kwenda Congo
kwa ajili misheni
maalum ya jeshi
kwa kipindi cha
miezi sita. Anasema
alikwenda na kumuacha mke
wake nyumbani kwake
ambapo amerudi mwaka
huu . Anasema ndani
ya wiki moja
tangu arudi hakuielewa
hali ya mke
wake kitu kilichomfanya achukue
maamuzi ya kumpeleka
hospitalini kwa ajili
ya vipimo. Alifanyiwa
vipimo vyote na
hatimaye kugundulika ana
mimba ya mwezi mmoja. Swali
la ndugu huyu
lilikuwa ni sheria inasemaje
katika hali kama
hiyo.
2. SHERIA
INAVYOSEMA KUHUSU HILI.
Ndani ya sura ya
29 ya sheria ya ndoa
kuna mambo makuu
matatu. Kwanza kuna kitu
kinaitwa ndoa halali ( valid marriage ), pili
kuna kitu kinaitwa
ndoa haramu ( void marriage)
na tatu kuna
kitu kinaitwa ndoa halali
au haramu kutegemea
na uamuzi wa moja
wa wanandoa ( voidable marriage).
Katika hayo matatu
,mawili ya ndoa
kuwa halali na
ndoa kuwa haramu
yanajulikana vyema ambapo
halali ni halali,
ni ile ambayo
haina shida na
haramu ni haramu,
ni ile ambayo
hairuhusiwi. Pengine maelezo
yanaweza kutakiwa katika
hili la tatu
la ndoa kuwa
halali au haramu
kutegemea maamuzi ya
mmoja wa wanandoa( voidable marriage ).
3. UHALALI AU
UHARAMU WA NDOA
KUTEGEMEA NA UAMUZI
WA MWANANDOA.
Kifungu cha 39
cha sheria ya ndoa
kimeeleza mambo
manne ambayo yakitokea
katika ndoa uamuzi
wa ndoa hiyo
kuendelea au kutoendelea
utakuwa katika mikono
ya mmoja wa
wanandoa hao. Hii ina
maana mmoja akiamua
ndoa iendelee hata
kama limetokea jambo
hilo itaendelea halikadhalika akiamua
isiendelee basi taratibu
za kuachana zitafanyika. Mambo
hayo ni kama
yafuatayo :
( a ) Ikiwa mwanaume
au mwanamke ataishiwa
na uwezo wa
kujamiiana. Mara nyingi tatizo
hili hutokea kwa
wanaume ambapo kutokana
na ugonjwa au
sababu nyingine yoyote
anashindwa kabisa kutekeleza
tendo la ndoa tena
kwa muda mrefu. Hii
inaweza kuwa wakati
wa kufunga ndoa au baadae
katika ndoa. Hili
likijitokeza basi mwanamke
atakuwa na hiyari
kutokana na mazingira
aliyoyaona aendelee kukaa
katika ndoa au
amtaliki mwenzake. Ni
uamuzi wake.
( b ) Pili
ni iwapo mmoja
kati ya wanandoa
amepatwa na magonjwa ya
akili ya kuchanganyikiwa na
pengine ni tatizo
ambalo sio rahisi
kutibika. Mwanandoa ataamua kati
ya kuendelea na
ndoa hiyo au kuachana
nayo.
( c ) Tatu
ni iwapo mmoja
wa wanandoa amepatwa
na tatizo la magonjwa ya
kuambukiza kupitia kujamiiana(venereal disease). Kwa mfano
yawezekana mmoja akakutwa
na virusi vya
ukimwi na mwingine
hana japo wote walikuwa
katika ndoa. Ni hiari ya mmoja
ambaye hana au
mwenye navyo kuamua
kumtaliki mwenzake au kuendelea na
ndoa.
( d ) Nne, ndio
hili sasa ambalo
ndio mada yetu. Ikiwa
mwanamke atagunduliwa kuwa
na mimba ya mwanaume mwingine
mbali na yule aliye
naye katika ndoa basi ni
hiari ya mwanaume
huyo kuamua kuendelea
na ndoa hiyo au
kuachana nayo. Hivyo jibu
kwa ndugu yangu ni kuwa ni uamuzi wake
sasa kuachana na
ndoa hiyo au kuendelea nayo, vyovyote
itavyompendeza.
Hata hivyo katika
kuachana na ndoa katika
mazingira yote niliyoeleza
hapa juu taratibu za talaka
za kisheria ikiwemo
kuihusisha mahakama zitahusika.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment