NA BASHIR YAKUB -
Hapa kwetu Tanzania
tunazo ndoa za aina
kuu mbili. Kwanza tunazo
ndoa za kiraia au
kiserikali, na pili tunazo
ndoa za kimila. Ndoa
za kiraia au
za kiserikali kama
zinavyojulikana kwa wengi ni
zile ambazo hufungwa chini ya
usimamizi wa mamlaka
za serikali kama ofisi
ya mkuu wa
wilaya n.k. Na kwa upande
wa ndoa za kimila hizi
ni zile ambazo
hufungwa kutokana na
taratibu za watu
wa kabila au
koo fulani kwa
mujibu wa tamaduni na desturi
zao. Ndoa za
kimila hujumuisha pia ndoa
zinazofungwa kwa taratibu
za kidini. Kwa taratibu
za kidini tunapata ndoa nyingi
kwa mfano ndoa
zinazofungwa kwa mujibu
wa mafundisho ya
kiislam, ndoa zinazofungwa
kwa mafundisho ya kikristo,
budha , wahindu na dini
nyingine pia wanazo taratibu zao.
Aidha sehemu za
kufungia ndoa kisheria ni
maeneo ya nyumba za
ibada, kwenye ofisi za serikali,
ubalozini kwa walio
nje ya nchi,
majumbani na sehemu
nyingine ambazo ni
wazi kwa watu
kushuhudia. Pamoja na hayo
yote juu yafaa tujue kuwa
zipo aina za
ndoa au mahusiano
yaliyokatazwa kabisa kuitwa ndoa. Juu
ya hilo sheria
imeainisha mambo ambayo
yakifanywa au yakipitiwa
ndoa inakuwa halali halikadhalika yale ambayo
yakifanywa au kutofanywa
ndoa inakuwa haramu.Haya
ni mengi isipokuwa hapa tutaona
baadhi yake. Pamoja na
hayo kabla ya kuyaona hayo kwanza tuangalie
baadhi ya taratibu
za kupitia kabla ya
kuendea suala la
kufunga ndoa.
1.BAADHI YA
MAMBO YA KUZINGATIA
WAKATI WA KUFUNGA
NDOA.
( a ) Kifungu cha
28 cha sheria
ya ndoa kinasema
kuwa ikiwa ndoa
itafungwa katika ofisi
za wilaya, kwenye
nyumba za ibada
au popote kwenye
jamii basi ni
vema ikawa ruhusa kwa
wanajamii au waumini
wa nyumba hiyo
ya ibada kushuhudia
bila kuzuiwa.
( b ) Pia
taarifa ya siku
21 kabla ya siku
iliyopangwa kufungwa ndoa
huwa inatakiwa kutolewa
na wahusika kwa
msajili wa ndoa. Msajili
wa ndoa yaweza kuwa
kadhi, ofisi ya
kidini kama bakwata, baraza kuu, au ofisi
ya kanisa ambapo
ndoa inatarajiwa kufungiwa.
( c ) Kifungu cha
256 cha sheria
ya ndoa kimeainisha
muda wa kufunga
ndoa ambapo kimesema
kuwa muda wa kufunga
ndoa ni baada
ya siku 21
tangu kutolewa kwa
taarifa ( notice) ya kufunga ndoa.
2. NDOA
ZISIZORUHUSIWA NI HIZI.
( a ) Kama
mwanamke ni mjane
au mtalaka na hajamaliza
mda wake wa eda
na ikiwa alifunga ndoa
ya kiislam basi atakapofunga
ndoa mpya itakuwa
batili na haitatambuliwa kama
ndoa kwa mujibu
wa sheria. Hii ni kutokana
na kifungu cha
38( 1 ) ( j) cha sheria ya
ndoa.
( b ) Ikiwa ndoa
iliyofungwa au inayotarajiwa
kufungwa ina muda
maalum. Wahusika wakisema tunaoana
kwa muda fulani halafu
tutaachana muda fulani ukiisha ndoa
hiyo itakuwa ni
haramu na haitaruhusiwa. Hapa kwetu
tuna ndoa za
maisha na hatuna
ndoa za kimkataba
na hivyo ni
kosa kuwekeana muda
wa kuishi katika
ndoa. Hii ni kwa
mujibu wa kifungu
cha 38 ( 1 ) ( I ).
( c ) Ikiwa mtu atafunga ndoa
huku akiwa na
ndoa nyingine inayoendelea, hii
ndoa ya
pili itakuwa batili. Hili
ni kosa zaidi kwa waliofunga ndoa
kwa taratibu za kikristo
ambao hutakiwa kufunga
ndoa moja tu. Lakini
pia ni kosa hata kwa
waislamu ambao pengine wamefunga
ndoa ya kiserikali
kwa sharti kuwa
mwanaume hataoa mke
wa pili au zaidi. Pia
ni kosa kwa mwanamke kwakuwa
kwa namna yoyote ile
mwanamke hutakiwa kufunga
ndoa moja tu. Kwa
hiyo ikiwa mtu
ataoa au kuolewa
wakati kuna ndoa
nyingine aliyofunga na haijatolewa talaka
basi hiyo ndoa mpya
itakuwa ni haramu.
( d ) Zaidi ndoa zote
zinazohusisha ndugu wa damu ni
ndoa haramu za
haziruhusiwi. Ndugu wa damu wameainishwa na kifungu
cha 14 cha sheria
ya ndoa ambapo
kinazuia mtu kumuoa bibi
yake au babu
yake, mjomba wake, shangazi yake, baba
au mama, kaka au
dada, kuoa au kuolewa na
wazazi wa mke
au mme wako, kuoa
au kuolewa na
mtu uliyem-asili (adopt), n.k.
( e ) Pia
ikiwa ndoa imefungwa
bila ridhaa ya
mmoja kati ya
wahusika bado uharamu
katika ndoa hiyo
unazaliwa na hivyo
kubatilika. Yatakiwa
wanaofunga wawe wameridhia
tena ridhaa huru
ambayo haikutokana na kulazimishwa au
kubanwabanwa.
Kwa mujibu wa sheria, hizi
zote ni ndoa
haramu na hazikubaliki.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
habari ya leo mie niko na langu swali.... endapo wawili wamezaa pamoja kisha mama akafa akaacha watoto ila mmoja alikuwa kwa baba na mwingine kwa mama.... wakati huo walitengana mda mrefu na mke alivyofariki aliacha wosia wa mdomo kuwa mtoto alonae asikae kwa yeyote isipokuwa kwa dada yake,,,, hapo inakuaje kisheria? na pia mme anamtaka
dini wako tofauti.... na ndoa yeyote hawakutimiza