NA BASHIR YAKUB -
Kisheria ndoa inapokuwa imefungwa
kuna haki za
msingi ambazo huibuka.
Hizi huitwa haki
za moja kwa
moja ( automatic right). Huitwa haki
za moja kwa
moja kwakuwa hazina
uhiari katika kutekelezwa
kwake. Kuwapo kwa
ndoa ndio kuwapo
kwake na hivyo
haihitaji mtu kuziomba. Kimsingi haki
hizi zipo nyingi
ambapo tutaona baadhi
yake hapa huku makala
yakijikita katika haki
moja ya matunzo kwa
wanandoa.
1.BAADHI YA
HAKI ZINAZOIBULIWA NA NDOA.
( a ) Haki
ya tendo la
ndoa. Hii ni haki
ya lazima kwa wanandoa na kutokuwepo kwake
kunaweza kubatilisha ndoa iwapo
mmoja wa wanandoa ataamua kufanya
hivyo. Ni haki ambayo
huchukuliwa kama ndio ndoa yenyewe na
hivyo kuifanya kuwa
na umuhimu wa pekee.
( b ) Haki
ya kutumia jina la mume. Hii ni haki
aliyonayo mwanamke ambapo
anaruhusiwa kutumia jina la
mme wake badala
ya lile la
baba yake. Hata hivyo sheria
haikueleza iwapo
mwanaume naye anaweza
kutumia jina la
mke wake, au
la baba wa
mke wake, au la ukoo
wa mke wake.
Pia si tu mwanamke
ameruhusiwa kutumia jina
la mme wake
isipokuwa hata lile
la ukoo wa mme wake.
( c ) Haki
ya kutumia mali
za familia kwa
pamoja. Haijalishi mali hizo
ni mwanamke mwanaume
ataruhusiwa kutumia na haijalishi
mali hizo ni za
mwanaume mwanamke ataruhusiwa
kutumia. Isipokuwa yawe matumizi
ambayo hayako kinyume
cha sheria.
( d ) Haki
ya kutunza watoto/mtoto kama yupo. Ikiwa
familia imebarikiwa na mtoto/watoto
basi wanadoa kwa
pamoja wanawajibika kuwatunza
watoto hao kila
mtu kwa nafasi yake. Hii
ina maana mwanamke anawajibika
zaidi kuwa mwangalizi
mkuu wa kila siku
wa watoto huku mwanaume
akilazimika kutoa matumizi
hasa yale ya kifedha.
( e ) Haki
ya kugawana mali
pindi ndoa inapovunjika. Hii huhusisha
mali zote ambazo
huitwa mali za
machumo ya pamoja
baina ya mwanamke na
mwanaume.
( f ) Pia
ipo haki ya
kurithi na kurithiana
iwapo kuna kifo
cha mmoja wa
wanandoa. Mwanamke aweza kurithi
mali za mme
wake halikadhalika mwanaume. Hii
huenda mpaka kwa
watoto waliopatikana katika
ndoa ambapo huweza
kurithi mali za
baba, mama au wote
wawili.
( g ) Haki
ya matunzo baina ya
wanandoa. Hii ndiyo
itakayojadiliwa japo kwa
ufupi .
2. MWANAUME
KUMTUNZA MWANAMKE.
Sura ya 29
ya Sheria ya
ndoa kifungu cha 63
( a ) kinasema kuwa
ni wajibu wa
kila mwanaume kumtumza
mke/wake zake kutokana na njia za
kipato chake. Neno
njia za kipato chake
maana yake ni namna anavyopata
kipato ndivyo atavyotakiwa
kutoa matunzo kwa
mwanamke. Haiwi kuwa
mwanaume anapata kipato
kidogo halafu alazimishwe
kutoa matunzo makubwa. Ushahidi
wa namna anavyopata
kipato chake ndio
utakaoainisha kiasi cha
matunzo kwa mke
wake.
Aidha kwa mujibu wa
kifungu hicho matunzo
yanayoongelewa hapa yanahusisha makazi,
mavazi, chakula na huduma
nyingine kama za afya
n.k. Kitu cha msingi
hapa ni kuwa
ni lazima kwa
mwanaume kutoa vitu
hivi kwa mke wake.
3. MWANAMKE
KUMTUNZA MWANAUME.
Kifungu hichohicho cha 63
( b ) kinasema kuwa utakuwa
ni wajibu wa
kila mwanamke lakini
mwenye uwezo
kutoa matunzo kwa
mume wake iwapo
mume huyo ana ulemavu/hajiwezi jumla
au sehemu ya
mwili wake, kiakili au
kimwili na hivyo
kutokuwa na uwezo
wa kuingiza kipato
kutokana na hali
hiyo.
Kwa kifungu hiki
tunaona kuwa mwanamke anao
wajibu wa kumtunza
mume wake lakini iwapo
tu kwanza ana uwezo,
pili mwanaume awe na
tatizo ambalo kwalo
hawezi kuingiza kipato
na tatizo hilo
liwe la kimwili au
kiakili. Kumbe basi tunaona
kuwa mwanaume kumhudumia mwanamke ni
lazima hata mwanamke
awe mzima wa
afya huku hafanyi
kazi wakati mwanamke
kumhudumia mwanaume ni
pale tu atapokuwa
ana tatizo ambalo
linamfanya asiweze kufanya
kazi. Lakini pia sheria imesema
mwanamke atatoa huduma
iwapo ana uwezo
wakati neno iwapo
ana uwezo haikuliwekwa
kwa mwanaume.Kwa mwanaume kutoa
ni kutoa tu.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment