NA BASHIR YAKUB-
Rufaa ni hatua
ya kisheria ambayo
hufikiwa na mhusika
katika shauri fulani
iwapo hakurushishwa na
maamuzi. Rufaa sio mpaka
uwe umeshindwa kabisa,
hapana. Yawezekana ukawa umeshinda
kesi lakini hukuridhishwa
na kiwango ulichoshinda.Kwa mfano
uliomba wavamizi waondoke
katika nyumba yako na
hapohapo wakulipe fidia. Mahakama ikatoa
hukumu kuwa umeshinda
wavamizi waondoke katika
nyumba yako lakini
ikasema wasikulipe fidia. Mazingira
kama haya unakuwa
umeshinda lakini ukitaka unaweza
kukata rufaa kulalamikia kutolipwa fidia.
Kwa hoja hii tunaona
kuwa kumbe kukata rufaa
si lazima uwe
umeshindwa badala yake unaweza
kuwa umeshinda lakini ukawa
hukuridhishwa na vitu fulani
katika
hukumu ambavyo unaweza
kuvikatia rufaa ili
navyo uvipate.
1.AINA ZA
RUFAA KATIKA MASHAURI
YA ARDHI.
Kisheria rufaa hutofautiana
kutokana na aina
ya mgogoro ulio
mbele. Mgogoro wa kimkataba
unazo namna zake
na masharti yake katika
rufaa, halikadhalika
migogoro ya kudai
fidia, migogoro ya kikazi, migogoro ya kifamilia na
talaka, migogoro ya jinai,
migogoro ya kibiashara n.k. Hii
ina maana hata
migogoro ya ardhi
nayo inazo namna
zake za rufaa. Katika
mashauri ya ardhi
mara nyingi migogoro huanzia baraza
la ardhi la
kata huenda mabaraza ya
ardhi ya wilaya, mahakama kuu
ya ardhi hadi
mahakama ya rufaa. Hizi
zote ni mamlaka zinazoweza
kuamua mashauri ya ardhi.
Aidha aina za
rufaa huweza kutokana
na mpangilio huu kimahakama. Ipo rufaa
inayotoka baraza la ardhi
la kata kwenda
baraza la ardhi la wilaya. Ipo rufaa
kutoka baraza la ardhi la
wilaya mpaka mahakama
kuu ya ardhi. Na
ipo itokayo mahakama
kuu ya ardhi
mpaka mahakama ya rufaa.
2. NAMNA
YA K UKATA RUFAA.
( a ) KUTOKA BARAZA
LA ARDHI LA
KATA KWENDA BARAZA
LA ARDHI LA
WILAYA.
Shauri lako la
ardhi linapoamuliwa katika baraza
la ardhi la
kata na ikawa
hukuridhishwa na maamuzi
ya baraza hilo
rufaa yako inatakiwa iende
baraza la ardhi la wilaya.
Hii ni
kutokana kifungu cha 19
cha Sheria ya
mahakama ya migogoro ya ardhi sura
ya 216 . Zingatia
sana kuwa rufaa
yako lazima iwasilishwe
baraza la ardhi
la wilaya ndani
ya siku 45
tokea siku hukumu iliposomwa. Aidha muda
wa siku 45
unaweza kuongezwa ikiwa
kuna sababu za
msingi zilizomfanya muomba
rufaa kuchelewa kuwasilisha
rufaa yake kwa
muda.
Moja ya sababu
za msingi inayozingatiwa ni ikiwa umechelewa kukata
rufaa kutokana na
nakala ya hukumu au
agizo(decree) kutokuwa tayari
na hivyo kumfanya muomba
rufaa kushindwa kuomba rufaa
kwa wakati. Ijulikane pia kuwa
rufaa itakayoandaliwa itatakiwa kuwasilishwa
baraza la ardhi
la wilaya lililo
katika wilaya lilipo
baraza la kata
lililotoa hukumu. Kwa hiyo kata zote
zilizo katika wilaya
fulani rufaa zao huenda
baraza la ardhi la wilaya hiyo
na si wilaya
nyingine. Jambo jingine la
msingi ni kuwa wakati
unapeleka rufaa yako baraza
la wilaya hakikisha
umeambatanisha na nakala
ya hukumu ya baraza
la kata.
( b ) RUFAA KUTOKA
BARAZA LA ARDHI
LA WILAYA KWENDA
MAHAKAMA KUU YA ARDHI.
Sheria ya
mahakama ya migogoro
ya ardhi kifungu
cha 38( 1 ) inasema
kuwa ikiwa mtu
hakuridhika na maamuzi ya baraza
la ardhi la
wilaya basi anaweza
kuomba rufaa kwenda Mahakama kuu
kitengo cha ardhi.
Rufaa hutakiwa kuwa
imewasilishwa ndani siku
sitini toka siku
ya kutolewa kwa
hukumu. Aidha lipo
jambo la msingi
sana la kuzingatia
hapa. Ikiwa shauri lilianzia
baraza la kata
na rufaa yake
ikaenda baraza la wilaya na
sasa rufaa yake
tena inakwenda mahakama
kuu basi rufaa
hiyo haitakiwi kupelekwa
moja kwa moja
mahakama kuu ya ardhi. Kitakachofanyika ni
kuwa utandaa rufaa
yako na utaiwasilisha
palepale mahakama ya wilaya
iliyotoa hukumu na
mahakama ndiyo itakayowajibika kupeleka
rufaa yako mahakama
kuu.
( c ) RUFAA KUTOKA
MAHAKAMA KUU YA
ARDHI KWENDA MAHAKAMA
YA RUFAA.
Ikiwa shauri linaloombewa
rufaa kwenda mahakama
ya rufaa lilianzia
baraza la ardhi
la kata basi
kabla kukata rufaa
hiyo ni lazima
mhusika kupata hati
kutoka mahakama kuu itakayoonesha kuwa kuna jambo
la kisheria ambalo
mahakama ya rufaa
inatakiwa kulitolea ufafanuzi. Na
ikiwa shauri lilianzia mahakama ya wilaya basi kabla ya
kuomba rufaa kwenda
Mahakama ya rufaa
mhusika lazima apate
ruhusa kutoka mahakama
kuu. Nyaraka zinazoambatanishwa ni
sababu za rufaa nakala
tano, kumbumkumbu za rufaa
nakala tano, na risiti
kuonesha malipo ya
ada husika.
Nimalizie kwa kusema
kuwa rufaa katika mashauri ya
ardhi ni tofauti
na rufaa katika mashauri mengine kama
tulivyoona.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA
NA MSHAURI WA
SHERIA KUPITIA GAZETI
LA SERIKALI LA
HABARI LEO KILA
JUMANNE , GAZETI JAMHURI
KILA JUMANNE NA
GAZETI NIPASHE KILA
JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment