NA BASHIR YAKUB -
Mashauri ya ardhi
yanazo mahakama zake maalum.
Mahakama za mashauri
ya ardhi huanzia
ngazi ya kata , wilaya, na kuendelea. Kisheria mashauri
ya ardhi huanzia
baraza la ardhi
la kata, baraza la ardhi
la wilaya, mahakama kuu
kitengo cha ardhi
hadi mahakama ya rufaa. Kutokana na
hilo upo utaratibu
maalum ambao hutoa
mwongozo wa wapi shauri fulani
likafunguliwe. Suala la
kufungua shauri katika ngazi
ya kata wilaya
au vinginevyo hutegemea
na mambo ya
msingi ya kisheria.
Moja ya mambo
hayo ni sehemu
mgogoro ulipotokea. Ikiwa mgogoro
umetokea katika kata fulani
au
wilaya fulani basi
baraza la ardhi
la kata hiyo
au wilaya hiyo
ndilo lenye mamlaka
kuamua shauri hilo. Pili
kufungua kesi hutegemea
na aina ya
mgogoro hasa kuzingatia
thamani ya eneo
la mgogoro. Kwa mfano
mgogoro wenye thamani
ya shilingi milioni 100
hauwezi kuamuliwa na
baraza la ardhi
la kata hata kama mgogoro
huo umetokea katika
kata hiyo. Haya na
mengine ndiyo husimama
kama mwongozo wa
namna ya kufungua shauri.
Kimsingi kufungua shauri
kunahitaji ushauri wa kitaalam
wa kisheria kwakuwa kukosea
kwa namna yoyote katika
kufungua shauri kisheria
hupelekea kushindwa kesi
tena katika hatua za
awali kabisa.
Aidha kwakuwa kila
ngazi utakayoamua kufungua
shauri la ardhi
inao utaratibu wake ambao
hutofautiana na ngazi
nyingine basi makala haya
yataangalia kufungua shauri
katika ngazi ya wilaya ambapo
kimsingi ndiyo hupokea
mashauri mengi ya
ardhi kuliko ngazi nyingine
yoyote. Pia ni muhimu
zaidi kujua kuwa mabaraza ya
ardhi ya wilaya
kisheria ndio mahakama
za ardhi za
wilaya.Hivyo tunapoongelea baraza la ardhi la wilaya
tunaongelea mahakama
za ardhi za
wilaya.
1.KUJAZA FOMU
MAALUM.
Hatua ya kwanza kabisa
unapotaka kufungua shauri
la ardhi katika
baraza la ardhi
la wilaya ni
kujaza fomu maalum
ambayo huwa na maelekezo
ya mwongozo wa nini
kinahitajika katika baraza. Fomu
hiyo hupatikana kwa
wanasheria wa kujitegemea, mashirika
ya
msaada wa sheria na hukohuko kwenye mabaraza
ya ardhi.Fomu hii ndio hutumika
kufungulia shauri baada ya
kujazwa vyema.
Hata hivyo mbali na fomu
hii yawezekana mlalamikaji
kuandaliwa maombi(application/plaint) maalum
na mwanasheria ambayo
nayo hutumika kufungulia
kesi. Unapotumia maombi maalum
kutoka kwa mwanasheria
hauhitaji tena kujaza
fomu hii badala
yake maombi hayohayo
ndiyo yatatumika kufungulia
kesi.
2..HAKIKISHA KUWA MGOGORO
UMETOKEA KATIKA WILAYA HUSIKA.
Mahakama ya
wilaya inayotakiwa kutumika
ni lazima iwe ni ile
iliyo katika eneo ulikotokea
mgogoro. Nyumba, shamba au kiwanja kinachogombewa hakiwezi
kuwa wilaya ya
ilala halafu mgogoro
ukafunguliwa wilaya ya
kinondoni. Au shamba linalogombewa lipo
wilaya ya karagwe
halafu mgogoro ufunguliwe
wilaya ya misenyi. Hilo
likitokea litakuwa ni
kosa ambalo si
tu litapelekea usumbufu
kwa aliyefungua shauri
bali pia litapelekea
kushindwa kesi na kuamuliwa kulipa
gharama za mtu aliyekuwa akishitakiwa/akifunguliwa kesi.
Hata hivyo inaweza
kutokea baadhi ya
wilaya zikawa hazina mabaraza ya
ardhi ya wilaya
je mashauri yao yatapelekwa wapi.
Kifungu cha 22 cha
Sheria ya mahakama ya migogoro
ya ardhi sura
ya 216 kinasema
kuwa waziri mwenye
dhamana anatakiwa kutangaza uwepo
wa baraza la
ardhi la wilaya
katika wilaya husika.
Kama hajafanya hivyo basi
anatakiwa kutoa tangazo la
wapi mashauri ya
wilaya ambayo hajatangaza
kuwapo kwa baraza wapi
wapeleke migogoro yao.
Kwahiyo
zile wilaya ambazo
hazina mabaraza ya
ardhi ya wilaya lazima
kuna mwongozo maalum
kutoka kwa waziri
husika kueleza ni
wapi mashauri yao
yapelekwe kwa muda
huo ambao baraza
halijaanzishwa.Hivyo ni wajibu wako
kuulizia katika makao
makuu ya wilaya
yako ni wapi
mashauri yenu yanapelekwa ikiwa hakuna
baraza kwenye wilaya yenu. Bila
shaka utaelezwa.
3. HAKIKISHA
THAMANI YA MGOGORO
HAIZIDI MILIONI HAMSINI
NI SI CHINI
YA MILIONI TATU.
Baraza la ardhi
la wilaya ambalo
ndio mahakama ya ardhi
ya wilaya linavyo
viwango maalum vya
thamani ya kesi
ambazo hupaswa kusikilizwa.
Siku zote hakikisha
unapofungua shauri katika
baraza hili thamani
ya mgogoro kwanza
isiwe chini ya milioni tatu
na ukubwa wake
usizidi milioni hamsini. Thamani ya mgogoro
hupimwa kwa kuangalia
thamani ya eneo. Unaangalia thamani
ya nyumba, shamba au
kiwanja mnachogombea. Ikiwa thamani
yake inaanzia milioni
tatu kwenda mbele
basi utafungua shauri
baraza la wilaya. Ikiwa
chini ya hapo
basi shauri litafunguliwa
baraza la ardhi
la kata. Na pia
ikiwa thamani ya mgogoro
inaanzia milioni hamsini
na kwenda mbele
basi shauri litafunguliwa
mahakama kuu.
Muhimu hapa ni kuwa
thamani ya mgogoro
ianzie milioni tatu
mpaka hamsini isizidi
hapo wala kuwa
chini ya hapo.
Kwa uchche hayo ndiyo
ya msingi ya
kuzingatia iwapo unataka
kudai haki yako
ya ardhi mahakama za wilaya za
ardhi.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment