NA BASHIR YAKUB -
Mara kadhaa kwenye familia
mbalimbali kumekuwa hakuna maelewano juu ya nani
asimamie mirathi. Unakuta wapo
wanaomkubali fulani asimamie
na wapo wanomkataa
wakimtaka fulani mwingine
ndiye asimamie. Hii huwa na
athari kubwa sana kwa
warithi hasa watoto
kama wanasoma ambao
kimsingi hutakiwa kutumia
mali zile katika mahitaji
ya msingi kama
ada na mahitaji
mengine muhimu ya kiustawi. Tumeshashuhudia mara
nyingi watoto wakiacha
kwenda shule kwa
kukosa ada na mahitaji
mengine muhimu kwa
ustawi wao sababu kubwa
ikiwa mgogoro wa
nani awe msimamizi
mirathi. Naamini huwa hakuna
sababu za msingi
za kufikia huko kwakuwa
tayari sheria imetoa mwongozo
wa nini kifanyike
katika mazingira kama hayo. Utata
huu mara nyingi
husababishwa na kutokuaminiana hasa
kama ndugu wana
utofauti wa mmoja wa wazazi mama
au baba. Makala yataeleza lipi la
kufanya.
1.MAMBO YANAYOZINGATIWA NA MAHAKAMA KUTEUA MSIMAMIZI MIRATHI.
( a ) Kwanza mahakama
huangalia kama kuna wosia.
Iwapo kuna wosia
basi huangalia iwapo
wosia ule umemtaja
msimamizi wa mirathi. Ikiwa umemtaja
msimamizi wa mirathi
na hakuna shauri
lolote lililofunguliwa
kupinga au kuhoji
uhalali wa wosia
huo basi msimamizi
wa mirathi aliyetajwa ndani
ya wosia huo ndiye
atakayethibitishwa rasmi na mahakama
kama msimamizi halali
wa mirathi.
( b ) Uadilifu wa
mwombaji ni jambo
jingine muhimu linalozingatiwa sana na
mahakama kabla kumteua
msimamizi wa mirathi. Yawezekana mtu
akawa ni ndugu
wa karibu na
wa pekee wa marehemu aliyebaki
lakini si mtu
muadilifu. Ni mtu ambaye kukabidhiwa
amana kubwa ya mirathi ambayo
hukusanya magari ,majumba , mashamba
viwanja n.k itakuwa ni
sawa na kuzitupa
mali hizo. Lakini
pia uadilifu asiwe
ni mtu ambaye
ana upendeleo kiasi
akikabidhiwa mirathi hawezi kutenda
haki baina ya
warithi. Watu wenye sifa hizo
hawatateuliwa kusimamia mirathi. Hata
hivyo hayo yatatakiwa kuibuliwa na kuoneshwa na
wanaompinga msimamizi aliyependekezwa kwa kupeleka
pingamizi mahakamani.
( c ) Jingine
linaloangaliwa ni maslahi
ya muombaji kwa
marehemu au kwa
mali za marehemu.
Maslahi kwa marehemu huangaliwa ukaribu
wa udugu kwa
mfano huyu ni mjomba
wa marehemu na huyu
ni mtoto wa
marehemu. Kimsingi mtoto wa
marehemu atakuwa na nafasi
kubwa ya kuwa
msimamizi wa mirathi kuliko mjomba
wa marehemu. Aidha maslahi
kwa mali za
marehemu huhusisha wadeni
wanaomdai marehemu kwa
mfano mabenki n.k. Hawa nao
wanaweza kuomba na kukubaliwa
kuwa wasimamizi wa mirathi.
2. KAMA HAMUELEWANI JUU
YA MSIMAMIZI MIRATHI INARUHUSIWA
NYOTE KUOMBA
KUSIMAMIA MIRATHI.
Ikiwa kama wanafamilia
mmeshindwa kuelewana kuhusu
nani awe msimamizi wa
mirathi au baadhi wamemteua
msimamizi wa mirathi
na baadhi hawakuridhika
naye basi inaruhusiwa
kwa wale ambao
hawakuridhika nao kuomba
kuwa wasimamizi wa
mirathi au kumpendekeza
msimamizi wao wa
mirathi. Yeyote ambaye
anahisi haikuwa sawa
kumteua fulani kusimamia
mirathi badala
ya fulani basi
anaweza naye kuomba
huyo fulani wake naye
awe msimamizi wa mirathi. Hakuna haja
ya kugombana ukiona
wamelazimisha msimamizi wao
wa mirathi basi
na nyie teua
wa kwenu na peleka jina
lake mahakamani.
Huko mahakama kwa
amani kabisa itateua
yule anayefaa zaidi
kati ya hao
wawili, watatu au wanne. Hii ni
kutokana na kifungu
cha 33( 2 ) cha
Sheria ya Mirathi
sura ya 352 ambacho kinasema
kuwa ikiwa watu
zaidi ya mmoja wataomba
kuteuliwa kuwa wasimamizi
wa mirathi basi
itakuwa ni katika
uhuru wa mahakama( court discretion) kuamua
nani kati ya hao
awe
msimamizi wa mirathi
huku maslahi ya
mapana na mafupi
ya kila upande
yakizingatiwa. Wakati mwingine mahakama
yaweza kuteua msimamizi
wa mirathi zaidi
ya mmoja . Si lazima
msimamizi wa mirathi
awe mmoja wanaweza
kuwa wawili, watatu
kadiri mahakama itakavyoona
inafaa na kupendeza.
Yote kwa yote kubwa
ninalotaka watu kuelewa
ni kuwa hakuna
haja ya kugombana
kwakuwa wamemteua msimamizi
wa mirathi usiyemtaka. Ukiona wamefanya
hivyo basi na wewe pendeleza
wa kwako na
peleka jina lake
mahakamani kuomba naye kuteuliwa kuwa msimamizi mirathi. Mahakama itaamua
kati ya huyo
wa kwao na
huyu wa kwako
nani asimamie mirathi.
Au ikiona wote
wanafaa basi wote wanaweza kuteuliwa .
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment