NA BASHIR YAKUB-
Ukisoma kichwa cha
habari utaona nimeongelea
nyumba lakini kimsingi
mchakato huu unahusisha
mali zote za
wanandoa vikiwemo viwanja,
magari, na kila
kitu ambacho ni
mali ya wanandoa. Kichwa kinajieleza
kuwa ni makosa
benki au taasisi yoyote
ya fedha kuuza
nyumba au mali
yoyote ya wanandoa
ikiwa wakati wa kuchukua mkopo
mwanandoa mmojawapo hakushirikishwa katika
mchakato wa mkopo
huo.
1. MAANA YA MALI
YA WANANDOA.
Mali ya wanandoa
ni mali yoyote
ambayo imepatikana kwa nguvu au
juhudi za pamoja
kati ya mme
na mke walio
kwenye ndoa ya
kikristo, kiislam, ya serikali au
ndoa nyingine yoyote
halali ikiwemo ile
ya kuishi wote
kwa muda wa
miaka miwili ( presumed marriage ). Hizi
zote ni ndoa
ambazo mali ikipatikana
ndani yake huwa
ya wanandoa. Pia
ile mali ambayo
mmoja
wa wanandoa amekuwa
nayo kabla ya
ndoa lakini baada
ya ndoa ikaendelezwa
na wanandoa kwa
kiasi kidogo au
kikubwa nayo
hubadilika kuwa ya
wanandoa wote.
Hii inajumuisha
mali zilizopatikana kabla
ya ndoa lakini
wanandoa wenyewe wakaamua
kwa hiari yao
kuzifanya kuwa zao wote
kwa pamoja kama
familia kwa makubaliano maalum. Nalazimika
kutoa ufafanuzi huu
ili ninaposema mali ya wanandoa
hairuhusiwi kuuzwa ieleweka
hata kwa kiwango
kidogo mali zipi
ni za wanandoa
na hivyo kuhitaji
ridhaa ya wote katika
kuwekwa dhamana.
2. MIVUTANO
KATI YA TAASISI
ZA MIKOPO NA WANANCHI.
Kipindi cha hivi
karibuni hasa baada
ya kuongezeka wito
wa ujasiriamali mali na
wingi wa taasisi
za fedha kumekuwepo na kesi
nyingi sana kati
ya raia na
taasisi hizi za
fedha. Unapoangalia kesi
hizi kwa haraka
unaweza kugundua mambo
mawili, kwanza umakini
mdogo wa taasisi
za fedha hasa
katika ufuatialiaji wa
uhalali wa dhamana
na pili uelewa
mdogo wa raia
kuhusu taratibu na haki
walizonazo katika mikopo. Raia
wanazilalamikia taasisi za mikopo kwa
kuwa wababe , wasio na
subira na wakiuka
taratibu na huku taasisi za
fedha nazo zinawalaumu
raia kwa kuwa wakaidi
,wakorofi na wasiopenda
kurejesha amana wanazopewa. Ni
msuguano mtupu.
3. BENKI HAIWEZI
KUUZA NYUMBA KWA MKOPO
AMBAO MMOJA WA
WANANDOA HAKUSHIRIKI.
Hili liko wazi
kuwa benki au
taasisi yoyote ya
fedha ni makosa
kuuza dhamana au
kitu chochote kilichowekwa
rehani kwa ajili
ya kuchukulia mkopo
ikiwa kitu hicho
ni mali ya
wanandoa na mwanandoa
mmoja kati ya
wanandoa hao hakushirikishwa katika
hatua za kuchukua
mkopo. Mali ya
wanandoa inaweza kuuzwa
iwapo tu wote wawili
walishirikishwa katika kuchukua mkopo lakini
si mkopo achukue
mmoja halafu eti
nyumba au kiwanja cha
familia kipigwe mnada
kwa kushindwa kurejesha. Ikitokea
mali kuuzwa kwa mazingira
kama hayo basi litakuwa
limetendeka kosa sawa na makosa
mengine tunayoyajua.
4. NINI MWANANDOA
AFANYE IKIWA HAKUSHIRIKISHWA NA
MALI INAELEKEA KUPIGWA
MNADA.
Ikiwa wewe ni
mke na mme
wako ndiye alichukua
mkopo bila kukushirikisha au wewe ni mme
na mke wako ndiye
alichukua mkopo bila kukushirikisha basi
unayo nafasi nzuri
na ya kuaminika
kuweza kuzuia uuzwaji
wa nyumba au
mali yoyote isiuzwe kwa
sababu hiyo tu
kuwa hukushirikishwa ukiwa
kama mwanandoa. Ni
rahisi tu kwani inahitaji
kukimbilia mahakamani na
kuomba kusitishwa uuzaji
kwasababu ukiwa kama
mwanandoa haukushirikishwa wakati
wa kuchukua mkopo
na hivyo huutambui.
Ni sababu ya
msingi na ya
kisheria na inakubalika
vizuri mahakamani na
kwasababu hiyo utapata
zuio na mali
haitouzwa.
5. WAJIBU
WA BENKI AU
TAASISI YA FEDHA.
Benki au taasisi
ya fedha inawajibu
kisheria kufanya uchunguzi
na kujiridhisha kabla
haijatoa mkopo kwa
kuangalia ikiwa mali
inayowekwa dhamana ni ya wanandoa
au hapana. Huu ni
wajibu wa benki
na raia hahusiki
nao. Kama wao watafanya uzembe wasichunguze
hili au wachunguze
lakini wasilione hili
basi waliobaki hawahusiki
na benki wawe
tayari kupoteza iwapo
mwanandoa ataibuka kupingana
nao.
6. NINI UFANYE KAMA TAYARI MALI IMESHAUZWA.
Hapo juu nimesema
kuwa kama wewe
ni mwanandoa na
hili limekukuta basi
kimbilia mahakamani uzuie uuzaji.
Zaidi nitoe hamasa kuwa kama tayari nyumba
imeshauzwa basi hujachelewa fungua kesi ya kuomba kurejesha nyumba
kwa sababu hii hii ya
kutoshirikishwa na katika
hili huna haja
ya kutia shaka nyumba itarejeshwa
vizuri tu. Badilika
na chukua hatua.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
KUONA BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
VIWANJA NA NYUMBA ZINAUZWA.
-WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
-UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
-UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
-IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
0 comments:
Post a Comment