NA BASHIR YAKUB -
Suala
la mirathi popote
linapotokea hutokea iwapo
kuna mtu amekufa
na ameacha mali .
Mtu akishakufa akaacha
mali hata kama
hakuna ndugu wa kurithi suala la mirathi
lazima liibuke. Huibuka kwakuwa lazima
zile mali ziende
pahali iwe kwa
mtu au kwa mamlaka.
Hata hivyo suala
la mirathi huibua
hisia zaidi hasa
panapokwa hamna wosia.
Marehemu asipoacha wosia lakini
akaacha mali mambo
huwa sio mepesi
sana labda iwe vinginevyo. Ifahamike
kuwa mirathi huhusisha mambo
mengi. Lakini pia huhusisha sheria
nyingi. Sheria za kiislam huhusika, sheria za kimila
huhusika na pia
sheria za nchi
ambayo ni sura
ya 352.
1.USIMAMIZI WA MIRATHI
KAMA KUNA WOSIA.
Kama
marehemu ameacha wosia
basi ni vema
kuangalia wosia huo
umemtaja nani awe msimazi wa
mirathi. Hili ni muhimu watu
walijue hata wale
walioandika wosia tayari au
wanaotarajia kuandika wosia.
Wengi wamekuwa wakiandika
wosia na kugawa
mali lakini wakisahau
kuteua na kumtaja
msimamizi wa mirathi
wakiamini kuwa kila
mtu atakapochukua chake mambo
yataishia hapo. Laa hasha
mambo si mepesi
kiasi hicho. Kwa
hiyo yafaa kuangalia
nani ametajwa kama
msimamizi wa mirathi
katika wosia na
huyu ndiye atakuwa
msimamizi wa mirathi. Ikiwa wosia
upo lakini haukumtaja
msimamizi wa mirathi
basi taratibu za
kimahakama nitakazoeleza hapa
chini zitafuata.
2. KUMTHIBITISHA MSIMAMIZI
WA MIRATHI MAHAKAMANI.
Ikiwa
wosia umemtaja msimamizi
wa mirathi basi hilo tu halitoshi. Sheria inataka
msimamizi wa mirathi
athibitishwe pia na mahakama. Hii
ni kwasababu mahakama
hutoa hati maalum
kwa aliyethibitishwa kuwa msimamizi wa
mirathi ambayo hutum ika
sehemu zote za
kisheria kwa mfano
kuchukua hela za
marehemu benki, kuchukua hisa za
marehemu, kuuza na kununua
mali za marehemu,kubadilisha vitu
kama hati na kila kitu
ambacho huhusisha taratibu
maalum za kisheria. Kwakweli isingewezekana kutumia wosia
kwa kuuonesha kila ofisi unayoingia
katika kufanya michakato hii yote.
Na hapa ndio mahitaji
ya kuthibitishwa na
mahakama na kupata hati maalum ambayo ni
kama utambulisho yalipotokea.
Pili
kama wosia upo
lakini haukumtaja msimamizi wa
mirathi napo ndugu
watakaa kikao watamteua msimamizi
wa mirathi na
atakwenda kuthibitishwa na
mahakama ili kupata
hati hiyo. Utaratibu
ni huu huu
hata panapokuwa hakuna
wosia wowote ulioachwa
na marehemu. Ndugu watakaa
kikao watamteua msimamizi wa mirathi na
atapelekwa mahakamani kuthibitishwa
na kupata hati
hiyo maalum. Kwa ujumla ninachotaka kueleza
ni kuwa hatua
ya kwenda mahakamani
kumthibitisha msimamizi wa mirathi ni
katika mazingira yote,
yaani wosia uwepo na
umemtaja msimamizi mirathi, wosia uwepo
lakini haukumtaja msimamizi
wa mirathi na
wosia usiwepo kabisa.
3. NANI HUSIMAMIA
MALI ZA MTOTO/WATOTO
WADOGO.
Marehemu anapoacha
watoto/mtoto mdogo akiwa ndiye
mrithi pekee nani
ana haki ya
kusimamia mali zake ndicho
ninachomaanisha. Na hapa
ni katika mazingira
yote yaani kuna wosia
au hakuna. Kwanza
tumjue mtoto ni nani. Mtoto
mdogo kwa maana hii ni yule
ambaye hajafikisha umri
wa miaka 18
na hivyo kutoruhusiwa
kuwa msimamizi wa mirathi.
Aidha wengine huacha
watoto wa mwaka
mmoja, miezi na
hata siku. Kifungu
cha 36( 1 ) cha
Sheria ya Mirathi
kinasema kuwa iwapo
kuna mtoto/watoto wanaostahili
kuwa wasimamizi wa
mirathi lakini hawawezi
kutokana na umri wao basi
mamlaka ya usimamizi
wa mirathi atapewa
mlezi wao au
mtu mwingine ambaye
mahakama itamuona anafaa.
Wakati mwingine mlezi
anaweza kuonekana si
mwadilifu na hivyo
kuziweka mali za
marehemu katika hatari ya kupokwa.
Ikiwa wasiwasi huo
utajitokeza basi mahakama
itamteua mtu mwingine
yeyote kusimamia mirathi mpaka
watoto/mtoto huyo akue ili
asimamie mwenyewe.
4. NANI HUSIMAMIA MALI ZA ASIYE
NA AKILI TIMAMU.
Natumia neno
asiye na akili
timamu japo ni
refu kwa kuhofia kutumia
neno chizi au kichaa
kutokana na ukali
wake. Hata hivyo namaanisha
hivyo. Kifungu cha 37
cha Sheria ya Mirathi
kinasema kuwa iwapo
mtu asiye na
akili timamu alitakiwa
kusimamia mirathi lakini
akashindwa kutokana na hali yake hiyo
basi mtu
anayemtunza au
mwingine atakayeonekana kufaa
zaidi atateuliwa kusimamia mirathi
hiyo mpaka akili
yake itakaporejea.
Hawa
wote mtoto mdogo
na asiye na
akili timamu mali
zao zinaweza kusimamiwa hata na wakili au
kabidhi wasii mahakama
ikiamua hivyo. Na haijalishi
wakili au mtu mwingine
atakayeteuliwa kama atakuwa
ndugu au vinginevyo
suala la msingi ni
uadilifu wake na uwezo wa
kutunza mali kwa
maslahi mema ya watu
hao.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment