NA BASHIR YAKUB -
Kwa wale ambao
tayari wana hati za
majumba au viwanja
wanajua wazi kuwa hati
hizo zimeandikwa muda maalum .
Tofauti na wengi wanavyofikiria hasa
wale ambao pengine
hawajamiliki ardhi au
wanamiliki ardhi lakini hawamiliki nyaraka hii . Hati unayopewa
ina muda maalum
wa kuishi. Sio kweli
kwamba ukishapata hati
basi ndio umemaliza,
hapana. Kama ilivyo kwa bidhaa
nyingine au nyaraka
nyingine kwa mfano
leseni za kuendeshea vipando vya
moto ambazo huisha
muda (expire) ndivyo ilivyo
kwa hati za nyumba/viwanja pia ambazo
nazo huisha muda wake ( expire).
MUDA WA
KUISHI KWA HATI.
( A ) KUPEWA HATI
BILA CHAGUO LA KUPEWA TENA (RENEWAL).
Kifungu cha 32 cha sheria ya
ardhi kinasema kuwa
mtu anaweza kupewa
hati bila kupewa
chaguo la kupewa
tena. Hii ina maana unapewa
hati kwa
muda maalum na
muda huo ukiisha basi
ardhi hiyo inakuwa si
mali yako tena. Inapokuwa si
mali yako tena
ardhi hurudi mikononi mwa
mamlaka za ardhi
ambapo waziri mwenye
dhamana na kamishna
mkuu wa ardhi
wanaweza kumpatia mtu
mwingine ardhi hiyo
akiwa kama mmiliki
mpya. Kifungu hicho
kimezungumzia kupewa ardhi
kwa muda wa
miaka 99. Hata hivyo wengine hupewa kwa muda miaka
66 na wakati mwingine
33.
( B ) KUPEWA HATI KWA CHAGUO
LA KUPEWA TENA.
Kifungu hichohicho
cha 32 kimeeleza pia
kupewa hati ya
ardhi inayokupa chaguo
la kuongeza muda
iwapo wa awali ukiisha. Hii ina
maana kama hati
yako imeandikwa miaka
99 basi muda
huo ukiisha unaweza
kuomba kuongezewa muda
kama huo tena au
chini yake. Halikadhalika
kama umepewa miaka
33 au 66
kama chaguo lipo
unaweza kuomba kupewa
muda uleule tena
au zaidi lakini usiozidi
miaka 99. Lililo kubwa
unalopaswa kuzingatia katika
haya ni kuwa
unapopewa hati ni lazima
ujue umepewa hati ya aina
gani. Tofauti ya nilichoeleza
hapo juu na
hiki hapa ni kuwa
hapo juu muda
wowote unaopewa ardhi hauwezi
kuongezeka tena ambapo
ukiisha ardhi inakuwa
si mali yako tena. Wakati hapa
unapopewa unaweza kuongeza tena
ukiamua kufanya hivyo.
( C ) Pia ipo
ardhi unaweza kupewa
na ukatakiwa kurenew kila
mwaka. Hii nayo ipo
katika kifungu hichohicho
cha 32( c ) cha Sheria
ya Ardhi. Unapewa haki ya kumiliki
lakini kwa sharti
kuwa kila mwaka
utaomba tena. Usipoomba
maana yake umiliki
wako unakufa. Aidha kwa
mujibu wa kifungu
hicho umiliki wa ardhi
inayomilikiwa kwa mwaka hauwezi
kufa mpaka kamishna
wa ardhi atoe
taarifa maalum (notice) kwa
mhusika . Hata hivyo wanaomilikishwa ardhi
kwa mtindo huu
wakati mwingine wanaweza
kupewa muda maalum
wa awali ambao
hauzidi miaka minne. Yaani
unapewa miaka minne
ya awali ambayo hutatakiwa
kurenew kila mwaka
halafu ikiisha hiyo ndio sasa unaanza kumilikshwa
mwaka mmoja mmoja
huku ukitakiwa kurenew
kila mwaka. Zaidi ya
hayo, lipo swali ambalo
wengi huuliza ambalo ni iwapo
inawezekana kupunguziwa muda wa umiliki
uliopewa kwenye hati
hata kabla ya
muda huo kuisha. Jibu
lake tutaona hapa chini.
KUPUNGUZIWA MUDA WA
UMILIKI WA HATI.
Kifungu cha
32(2) cha Sheria Ya Ardhi
kinasema kuwa pale
ambapo mtu anakuwa
amepewa umiliki wa ardhi
kwa kipindi maalum muda
wake aliopewa hauwezi
kupunguzwa bila kufanya makubaliano naye. Maana
yake ni kuwa
kama umepewa miaka
33, 66, 99 muda huo
hauwezi kupunguzwa bila
kufanya makubaliano na
wewe. Kitu kingine ambacho
watu wangependa kujua ni
kwanini umiliki wa ardhi
unatofautiana muda. Jibu ni kuwa
serikali hutoa muda
tofauti wa umiliki
kutegemea sera na mipango
ya maendeleo ya eneo husika.
Yapo
maeneo ambayo wasingependa
watu wakae kwa muda
mrefu sana kutokana na mipango ya baadae.
Maeneo kama hayo watu
watamilikishwa kwa muda
mfupi. Na yapo
maeneo ambayo tayari
mipango yake imekamilika na si
vibaya watu kuishi
kwa muda mrefu . Maeneo hayo watu watamilikishwa hata
miaka 99. Kwa ufupi hizi
ndio sababu za
utofauti wa miliki
ya miaka.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment