NA BASHIR YAKUB -
Watu wengi wanaonunua
ardhi wamekuwa wakipata usumbufu mkubwa
katika kubadili majina yaani kutoka mmiliki
wa mwanzo kwenda kwa mmilki mpya aliyenunua.
Upo usumbufu ambao husababishwa kwa makusudi
na maafisa wanaohusika lakini pia upo
usumbufu ambao husababishwa na watu
wenyewe wanaotaka kubadili majina. Wengi huanza
muamala huu bila
kuwa na taarifa
kamili za nini kinahitajika kwa maana
ya nyaraka ikiwemo
ada au malipo ya
kisheria jambo ambalo huwapotezea
muda mwingi. Kwa wanaofanya
kazi hizi kama
mimi watajua ni usumbufu
wa aina gani mtu
huupata anapoanza mchakato huu
bila taarifa. Unaposoma
makala haya ni
vema basi ukajua
inatakiwa ujiandae na
nini na hasa
ada ili unapoanza mchakato
huu usijikute unaishia
njiani.
1.UMUHIMU WA KUBADILI JINA
HARAKA BAADA YA MANUNUZI.
Nimewahi kuandika kuwa sheria iko wazi
kuwa ambaye jina lake linaonekana kwenye hati ndiye mmiliki.
Kwa kauli hii
mnunuzi anatakiwa kufanya jitihada za
haraka na za makusudi kubadili jina mara tu
baada ya kununua kiwanja au nyumba. Sikatai
kuwa kunakuwa na mkataba wa mauziano lakini
lazima ieleweke kuwa mbele ya macho
ya sheria jina lililo kwenye hati
lina uzito kuliko mkataba wa mauziano.
Usiridhike kukaa na mkataba wa mauziano
ikiwa hujabadili jina. Hii ni kwa ajili
ya ulinzi wako na wa ardhi yako.
Utakapotokea mgogoro
wa umiliki ikiwa hujabadili jina waweza
kuwa katika hatari kubwa ya kupoteza
hasa kama mgogoro huo umeanzishwa na aliyekuuzia.
Huu ndio ukweli na lazima tuonyane
ili tuwe salama na mali zetu. Lakini
pia hata ukitokea mgogoro mwingine wowote wa
umiliki kuna mambo ndan ya sheria
yataufanya kuwa mgumu kutokana na sababu tu
kuwa ulikuwa hujabadili jina. Hapo
sijaongelea faida nyingine za kubadili jina kama
kukopa n.k. Nishauri tu kwa ufupi kuwa
unapojiandaa kununua nyumba au kiwanja jiandae
pia na kubadili jina moja kwa moja.
Hakikisha haya mawili yanakwenda pamoja.
2. ADA
ZA KUBADILI HATI ZA
NYUMBA/VIWANJA HIZI HAPA.
Nimesema
hapo juu kuwa
usipojiandaa na ada
vyema mara nyingi
utajikuta unaishia njiani
kwa kushindwa kukamilisha
mchakato huu. Lakini
utaandaaje ada bila
kujua kinahitajika kiasi
gani . Hili ndilo lengo
la makala haya. Malipo ya ada
tunaweza kuyagawa mara mbili.
Kwanza
kuna ada inayolipwa manispaa. Hii
hulipwa katika manispaa
ile ambayo kiwanja au
nyumba ilipo. Kama temeke
basi ada italipwa
manispaa ya temeke
halikadhalika maeneo mengine hivyohivyo. Na hapa
ndipo unapoanzia katika ulipaji
wa ada. Ada
inayolipwa katika manispaa huwa ni
asilimia moja ya mkataba
wa kununulia au
ya taarifa ya
tathmini (valuation report). Unapokwenda
kulipa ada manispaa
ni lazima uambatane
na mkataba wako
ulionunulia kiwanja/nyumba pamoja
na valuation report
kwakuwa hivi ndivyo
wanavyotumia kama vipimo vya
ada. Ikiwa mkataba wa
kununulia una bei
kubwa kuliko valuation report
basi wanachukua asilimia
moja ya mkataba
huo na ndio itakuwa
ada. Lakini ikiwa pia
valuation report ina bei
kubwa kuliko mkataba basi
wanachukua asilimia moja ya
valuation report. Kwa ujumla
wao huchukua asilimia moja
ya chenye bei
kubwa kati ya
valuation report na
mkataba wa kununulia
na huifanya hiyo
ndio ada.
Pili
baada ya kulipa
manispaa faili lako hupelekwa mamlaka
ya mapato Tanzania ( TRA) kwa ajili
ya kodi. Hawa wao
hutoza asilimia kumi
ya taarifa ya
tathmini( valuation report). Kama
valuation inasema
eneo lako lina
thamani ya milioni
kumi bila shaka asilimia kumi
yake ni milioni moja. Hiyo ndio itakuwa
kodi. Angalizo hapa ni kuwa
hizi valuation report
hutakiwa zile mpya. Kwa
mfano mtu anayo valuation
yake aliyofanyiwa mwaka
2000 na sasa anataka
kupata au kubadili hati
leo 2015. Hii ya
mwaka 2000 haiwezi kutumika kutathmini
kodi itahitajika mpya ya mwaka 2015. Hii
ni kwasababu thamani
ya ardhi ya
mwaka 2000 si sawa
na ya sasa
mwaka 2015. Hizi ndizo ada
unazotakiwa kujiandaa nazo.
2. PIA
ANDAA NYARAKA HIZI.
( a ) NYARAKA ZA UHAMISHO
Nayaraka za uhamisho
zinajumuisha fomu namba 29 ijulikanayo kama
fomu ya kusudio la uhamisho( notification of
disposition) ambayo hueleza nia na lengo la
muuzaji kutaka kubadili jina au kuondoa
jina lake katika hati. Hii utaandaa nakala
tatu . Pili ni fomu namba 30 ambayo
hujulikana kama fomu ya idhibati ya
uhamisho ( application for approval of disposition).
Katika fomu hii muuzaji pia atakuwa
anatoa idhini kwa mamlaka za ardhi kuidhinisha
hiari yake ya kuachia umiliki kutoka
kwake kwenda kwa mtu mwingine ambaye ndiye
mnunuzi.
Mwisho ni fomu
namba 35 ijulikanayo kama fomu rasmi ya
kuhamisha umiliki ( transfer of a right of occupancy)
ambayo ndiyo rasmi sasa huhamisha umiliki
kutoka kwa muuzaji kwenda kwa mnunuzi. Hii
ndiyo humpa mnunuzi umiliki rasmi . Pia
mkataba wa mauziano ni nyaraka ambayo
itaambatanishwa hapa.
Kwa kiwanja au
eneo ambalo halijaendelezwa ( halijajengwa)
huandaliwa kitu kiitwacho commitment
bond kikiwa kama ziada ya nilivyotaja
hapo. Fomu zote hizo pamoja commitment
bond hupatikana katika ofisi za wanasheria
na huandaliwa na wanasheria.
( b ) URAIA
Sheria iko wazi kuwa
wanaotakiwa kumiliki ardhi ni raia wa nchi
hii tu. Hivyo unapotakiwa kupata hati ya
umiliki lazima pia uthibitishe Utanzania wako.
Hapa utatakiwa kuandaa nakala(copy) ya
cheti cha kuzaliwa ambayo imethibitishwa(
certified) na wakili au nakala ya
pasipoti ambayo imethibitishwa na wakili au
kama huna hivyo vyote basi yakupasa
kuandaa kiapo( affidavit).
Mwisho niseme kuwa
ikiwa utajiandaa vyema na haya utapata
hati kwa urahisi au kama unabadili
jina utabadili kwa urahisi pia. Jiandae epuka
usumbufu.
MWANDISHI WA MAKALA
HAYA NI MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO KILA JUMANNE ,
GAZETI JAMHURI KILA JUMANNE NA GAZETI
NIPASHE KILA JUMATANO.
0784482959,
0714047241
bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA
NYUMBA ZINAUZWA.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment