NA BASHIR YAKUB -
Kupekua( search) ni
tendo ambalo hufanywa
na mamlaka za
usalama katika maeneo
mbalimbali hasa katika makazi ya
watu. Mbali na
makazi ya watu
kupekua pia kwaweza
kufanyika katika magari, treni, na
vyombo vyote vya
usafiri zikiwemo ndege
na meli. Pia kupekua kwaweza kufanywa kwa
mtu kwa maana kuwa mtu
kama mtu naye anaweza
kupekuliwa(search). Iwe
mifukoni au wapi
lakini mtu naye
hupekuliwa. Kwa jina la
mtaani kupekua hujulikana
kwa jina la
kupiga sachi. Hivyo basi
kupekua na kupiga
sachi ni kitu
kilekile. Mbali na kuwa
upekuzi waweza kufanyika sehemu nyingi
kama tulivyoona makala haya
yatagusa upekuzi katika maeneo ya nyumbani kwa maana kwenye
makazi au maofisi. Suala la upekuzi
kwa ujumla wake
huongozwa na Sura
ya 20, Sheria ya
Mwenendo wa Kesi
za Jinai kama
ilivyofanyiwa marekebisho 2002
na wakati mwingine
Sheria ya Jeshi
la Polisi Sura ya 322.
1.SABABU ZA
KUPEKUA.
Kisheria sababu za
kupekua lazima iwe
ni katika kutafuta
ushahidi ambao utawezesha kupatikana
kwa ukweli wa
jambo fulani ambalo
lipo katika ngazi
za upelelezi katika mamlaka
fulani. Hauwezi kufanyika
upekuzi nyumbani kwa mtu kwa
lengo jingine na
hilo likitokea basi
itakuwa ni kinyume cha
sheria. Sehemu inayopekuliwa ni
lazima kuwepo na
tetesi au uhakika
wa kuwa eneo hilo
upo ushahidi unaotafutwa
kwa ajili kuanzisha,kuendeleza au
kukamilisha upelelezi fulani. Kwa
hiyo sababu kubwa
ya upekuzi(search) ni kutafuta
ushahidi. Hakuna upekuzi kwa ajili ya sababu
binafsi.
2. NANI
HUTAKIWA KUFANYA UPEKUZI (SEARCH).
Askari polisi anayo
mamlaka ya kufanya
upekuzi katika nyumba
ya mtu. Nyumba
yaweza kuwa ya
makazi au ya biashara
kama duka, mgahawa, hoteli, nyumba
za wageni, na
vyuoni na mashuleni. Zaidi maafisa
wengine kama taasisi
ya kuzuia na
kupambana na rushwa
au wale wa
mamlaka ya chakula
na dawa ( TFDA) n.k.nao wanaweza
kufanya upekuzi . Isipokuwa
maafisa hawa wengine kama
mamlaka ya chakula
na dawa wanaruhusiwa
kufanya upekuzi katika
yale maeneo yanayohusu
ile kazi yao
tu, kwa mfano
dukani kukagua bidhaa basi
na si kuingia
mpaka chumbani kwa
mtu. Hata hivyo wanashauriwa
kuambatana na afisa wa
polisi mara zote wanapoamua kufanya
upekuzi.
3. HAIRUHUSIWI
KUFANYA UPEKUZI USIKU
BILA KIBALI CHA MAHAKAMA.
Kifungu cha 40
cha Sheria ya
Mwenendo wa Kesi
za Jinai kinasema
kuwa hati ya
upekuzi inaweza kutolewa na kutekelezwa
siku yoyote na
inaweza kutekelezwa kati
ya muda kuchomoza au
kuchwa kwa jua lakini mahakama
inaweza kwa maombi
ya afisa polisi
au mtu mwingine
yeyote ambaye imeelekezwa
kwake kumruhusu kutekeleza muda
wowote. Katika
tafsiri ya kifungu
hiki kuna mambo
mawili ya msingi.
Kwanza tunaona kuwa upekuzi
kawaida unatakiwa ufanyike
siku yoyote kati
ya jua kuchomoza
na jua kuchwa. Jua
kuchwa ni jua
kuzama. Kawaida muda wa
jua kuchomoza maeneo
mengi ya Tanzania
ni kuanzia Sa 12
za asubuhi na ,maeneo mengine
saa 11 za
asubuhi. Na muda
wa jua kuzama
maeneo mengi ni kati ya
saa 12 za
jioni hadi saa
moja jioni. Kwahiyo huo
ndio muda wa
kawaida ambao upekuzi
unatakiwa kufanyika kwenye
nyumba za watu. Kimsingi ni
muda wa mchana( day time).
Pili, tafsiri inayofuata
katika
kifungu hicho ni pale
kinaposema kuwa kwa
kibali maalum cha
mahakama upekuzi unaweza
kufanyika muda wowote. Hapo
juu tumeona upekuzi
unatakiwa kufanyika katika
muda maalum ambao
kimsingi ni asubuhi
mpaka jioni (mchana). Hapa sasa tunaona
kuwa upekuzi unaweza
kufanyika muda wowote ikiwemo usiku
wa manane lakini
hii itakuwa kwa
kibali maalum cha
mahakama. Kwahiyo tunaona
wazi kuwa ili upekuzi ufanyike
usiku yapaswa kuwepo
kibali cha mahakama
ambacho kimeruhusu kufanya
hivyo vinginevyo upekuzi wote
hutakiwa kufanyika masaa ya mchana. Kwa
maana hii unapogongewa
usiku na askari
wanaojitambulisha kuhitaji kufanya upekuzi kwako basi kabla ya kuruhusu zoezi
hilo kufanyika omba
kuona kibali cha
mahakama hata kupitia
dirishani kwanza. ACHA KUNYANYASWA, CHUKUA HATUA.
MWANDISHI WA
MAKALA HAYA NI
MWANASHERIA NA MSHAURI
WA SHERIA KUPITIA
GAZETI LA SERIKALI
LA HABARI LEO
KILA JUMANNE , GAZETI
JAMHURI KILA JUMANNE
NA GAZETI NIPASHE
KILA JUMATANO. 0784482959, 0714047241 bashiryakub@ymail.com
TANGAZO MUHIMU
VIWANJA NA NYUMBA
ZINAUZWA.
·
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
WANASHERIA WETU WATAKUANDALIA MIKATABA YOTE BURE NA KUKUSIMAMIA MPAKA MANUNUZI YAKAMILIKE BURE.
·
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
UHALALI WA NYARAKA NA UMILIKI UMETHIBITISHWA NA WANASHERIA WETU.
·
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
UTAPEWA MTU WA KUKUSAIDIA KUFANYA TRANSFER KWA HARAKA BURE.
·
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
IKIWA UTATOKEA MGOGORO NDANI YA MWAKA TANGU TAREHE YA MANUNUZI UTAPEWA WAKILI WA KUSIMAMIA MGOGORO BURE
0784482959.
KUONA
BOFYA HAPO JUU MWANZO WA BLOG.
0 comments:
Post a Comment